Assumption: Tanzania tuna electoral college ya watu aina Pascal Mayalla,je itaweza kutupatia kiongozi bora?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
41,454
2,000
Nimewaza sana mpaka kuleta hii mada:

Wakuu,Pascal tunamsoma sana hapa JF na ninafikiri mpaka sasa imekuwa ni vigumu kwa wengi kuelewa huyu mwenzetu anasimamia upande gani ingawa mwenyewe ameshaweka wazi kuwa ni mtu neutral kwa maana ya kuwa hana chama katika siasa za nchi hii ingawa sometimes anatuchanganya sana.

Binafsi naamini mtu unapompima kiongozi inabidi uangalie mazuri yake na mapungufu yake alafu ufanye uamue katika mizani kama kiongozi husika anafaa au hafai ili umchague au uwe unamuunga mkono.

Sasa kwa jinsi tunavyomsoma Pascal alafu tuka-assume tuna electoral college yetu hapa nchini kama ile ya Marekani alafu watu hao wakatakiwa kupiga kura kuamua nani awe kiongozi wa nchi hii,unadhani watu wenye fikra na mitazamo kama ya Pascal juu ya viongozi wetu wanaweza kuchagua kiongozi bora?

Kwa maneno mengine,watu wasio na upande wowote na wanaowapima viongozi kwa kwenda na matukio,wanaweza kuwa wapiga kura wazuri kwa maana ya kufanya maamuzi sahihi kwenye sanduku la kura kuliko sisi wengine?

Karibuni kwa mjadala.
 

KIDUDU

JF-Expert Member
Sep 17, 2012
2,569
2,000
Huyu Jamaa hana tofauti na zitto.
Double agent balaa,si wa kumsikiliza sana ingawa anajielewa.
"Mayalla maana yake ni njaa"Watanzania daini katiba mpya ccm itoke vinginevyo mtapata tabu sana.
Yaani hapa mkulu alitoa msg safi kwamba jamaa ana shida ya tumbo
 

wanaojulikana

JF-Expert Member
Sep 14, 2017
577
1,000
Brother usihangaike na huyo anauma na kupuliza wakati huo malengo yake makubwa ni kupata chakula kutoka kwa yule Mungu mtu
 

sir mweli

JF-Expert Member
Feb 8, 2017
495
1,000
Huyu jamaa ni mmoja ya wale wanaojipendekeza kwa big zuzu...hana tofauti na Jeri muro
 

YALE

JF-Expert Member
Apr 20, 2017
308
500
Sasa mtu kama huyu anaweza kuwa mpiga kura mzuri wa kusaidia kupata kiongozi bora?
Ni ngumu Kusema Yes or No, mayalla kumbuka yuko neutral kulinda Masilahi yake pia kwa vile ni mwandishi wa Habari ni vyema kuwa hivo, Lakini Kwa mtazamo wa haraka Jamaa yuko vizuri kichwani na anajua kuzichanga vyema karata
 

cblhbn

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
369
500
Mbona mnamlazimisha kila mtu kuwa mwasiasa, awe anafikiria kama nyie pumbavu kabisa mnataka tyfikirie kwa chuki,ngilibha na roho mbaya, Pascal anasema when black it's black and not white,shame on you
 

ngozimbili

JF-Expert Member
Jul 28, 2011
1,371
2,000
Hatuwezi kumuelewa leo lkn Nina uhakika cku moja tutamuelewa.yéyé na zitto wanatumia vichwa na siyo mioyo kufikiri
.time will tell
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
41,454
2,000
Mbona mnamlazimisha kila mtu kuwa mwasiasa, awe anafikiria kama nyie pumbavu kabisa mnataka tyfikirie kwa chuki,ngilibha na roho mbaya, Pascal anasema when black it's black and not white,shame on you
Swali ni je,mtu wa aina hii anaweza kuwa mpiga kura mzuri?
 

bigmind

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
12,326
2,000
Paschal team Lowassa alijichanganya, ndiyo maama anajitahidi kura kona kijanja!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom