Assistant Accountant experiance ya 10 years!

Mohammed Hamad

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
3,988
1,301
Wadau jana nimeshtuka sana na kustaajabu baada ya kusoma tangazo la kazi lililotolewa na gazeti la Daily News la jana kwenye ukurasa wake wa 5.

TPDC wanatafuta mhasibu msaidizi na awe na sifa zifuatazo;-

1. Holder of Diploma in Accountancy or equivalent qualification from a recognized institution.
2. Holder of Advance Diploma in Accountancy or bachelor degree in accountancy will be an added advantage.
3. Practical experience of not less than ten years in the relevant field.

Hoja yangu ni hapo kwenye red. Hivi mtu anaweza kuwa assistant accountant kwa miaka kumi hapandi? yaani hachukui review classes za CPA wala haongezi nondo? kwa mawazo yangu mtu kama huyo kadumaa. Ulimwengu wa sasa sio wa kulazimisha watu wawe na ujuzi wa miaka kumi na qualification za chini ningewaelewa kama wangetaja ujuzi wa miaka kumi kwa mtu mwenye Masters au CPA.
 
Its true, this does not make any sense. Labda kuna mtu hapo TPDC ana uhasibu wa kuunga unga (katika hiyo miaka 10) wanataka kumpa hiyo nafasi.
 
Usitishike na hiyo mkuu, wewe tuma tu, unaweza ukute wenzako nao wanashangaa hivyo hivyo ukajikuta umetuma mwenyewe na kazi ukalamba!! ilishawahi kumtokea jamaa yangu mmoja!! tuma application mkuu
 
aliye toa tangazo hata afikirii kashapatia jobu nduguye anatangaza basi tuu iwe kigezo cha kumpa ndugu kazi kwavile alikosa aliye kuwa anahitaji
 
Huu ni utapeli,
Huyo mtu aliekaa kwenye Post hiyo miaka kumi bila kupanda atakua alikua mwizi tu,
Na hapo labda kulikua na vi-mrija vyake ambapo alikua hataki kuhama,
Kifupi wanatafuta mtu mwenye hidden qualification ya wizi!!!
 
Tena siyo Assistant Accountant, kazi iliyotangazwa ni Accounts Assistant, hizi ni kazi mbili tofauti. Accounts Assistant is more clerical job, hata ukisoma role atakazokuwa anafanya utagundua.

Hata mimi nimeshtushwa na requirement ya not less than 10 years of experience, nikajiuliza huyu jamaa anaenda kufanya kazi ya u CEO wa CMSA au anaenda kuwa DF?
 
Hawana lolote wanatangaza hiyo nafasi kama kutimiza sheria za ajira,full undugunization na tayari kuna m2 wao hapo washamtengea hiyo post. Nafasi ndogo kama hiyo inatakiwa wawapatie fresh from school ili watafutie experience
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom