Assasination of President of Liberia Samuel Doe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Assasination of President of Liberia Samuel Doe

Discussion in 'International Forum' started by WA-UKENYENGE, Jul 25, 2012.

 1. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  WanaJF, nilikuwa napitia pitia documentary kazaa na kichwani nilikuwa nawaza tu kwanini viongozi wetu hawajifunzi kutokana na hawa watawala walivyofanyiwa? Au ni ukiziwi ama nini? Saizi kila kukicha vilio haviishi, kuna tofauti gani wakati wa biashara ile ya utumwa na kipindi hiki cha ufisadi?
  Tafadhali sikiliza kwa makini maswali aliyokuwa anaulizwa Samuel Doe kabla hawajamliza. Kumbuka this was more than 2 decades ago kipindi ambacho technolojia ya habari ilikuwa bado lakini watu walikuwa na hasira naye vibaya sana. Sasa hivi ambapo kuna kila aina ya vyanzo vya habari bado viongozi wetu wanaona nii njia nzuri kuficha ukweli, ni vizuri kufanya mambo yasiyowanufaisha wananchi! bado viongozi wetu wanaishi kwa propaganda hadi lini?

  Bofya hapa SAMUEL DOE
   
 2. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Huyu jamaa nafikiri hakutegemea siku kama hiyo ingefika,ubabe siku zote mwisho wake siyo mzuri. Kuna moja niliiona walivyokata sikio.Duh!Jamaa walikuwa na machungu nae sana.Tatizo viongozi wetu wanajisahau sana.
   
 3. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Sijui kama viongozi wetu huwa wanakumbuka jinsi watu wanavyokuwa na matumaini wakati wa kampeni, na hiyo ndiyo dhambi kubwa inayowatafunaga wengi! Utakuta ahadi chungu nzima kumbe ni za kilaghai!! We are all human being, why treating others like dogs and others like angles who never go the toilets? Why if you are a leader can't help the people sorrounding you to improve their living standards? Viongozi wana nguvu za kufanya mabadiliko lakini hawzitumii hizo nguvu. Watu wako tayari kwa mabadiliko, viongozi hawako tayari!!
   
 4. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Tatizo la hawa viongozi hasa hasa wa ki Africa huwa wanadhani watakaa madarakani milele. So arobaini yao ikifika huwa ni aibu na fedheha kubwa kwao. Doe anaulizwa : 'I am asking you, what happened to our economy? Tell the Liberian people! Majibu ya msingi hakuna! Alafu DOE yuko uchi wa nyama. Aibu kweli kweli.
   
 5. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Kaulizwa swali hilo kashindwa hata kujibu!! Matokeo yake hasira zikawapanda zaidi. He didn't know what he was doing at the state house zaidi ya kuibia raia maskini na wasiokuwa na uwezo wa kupata milo 3. This is very similar to our leaders, ukimuuliza mbunge swali kama hilo wengi hawata jibu zaidi ya kuanza kujiuma uma na kusema serikali mmmmhhh serikali!! Matokeo yake unakuta sehemu moja isipotoa raisi wa ncho au kiongozi wa juu wa nchi inaendelea kuwa nyuma.
   
 6. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  [​IMG][video=youtube_share;Cx76eOBHTVs]http://youtu.be/Cx76eOBHTVs[/video]
   
 7. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Duh,pressure imenipanda.Hii wampelekee baba Ritz,akumbuke anavyoitumbukiza nchi shimoni huku umasikini ukizidi kuwaandama watz, huku wao CCM waking'ang'ania madaraka.Hii hali naiona TZ haiko mbali sana.Ngoja huu mfumuko ufike50% mishahara ileile, ndio watakapojua kuwa "Usimuamshe aliyelala,ukimuamsha utalala wewe"
   
 8. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
 9. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  kwa hiyo unataka kusema kuwa yanaweza kumkuta nani? kama ya samuel doe
   
 10. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Wapo viongozi wengi, ni vogumu kumkuta kama ya Samuel Doe kwa sasa kutokana na ustarabu wa watu uliopo kwa sasa! Ila ukifanya transformation ya yaliyomkuta kipindi hicho utaweza kupata ile equivalence yake.
   
 11. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kadiri unavyokuwa juu kabisa na kujisahau ndivyo kuanguka kwako kunavyokuwa kwa maumivu na aibu zaidi. Inauma kuona hali kama hiyo inamfika mtu aliyebeba dhamana ya kuongoza nchi, iwe kwa kujichukulia madaraka kwa mtutu wa bunduki, wizi wa kura au kwa ridhaa ya wananchi.

  Natamani Doe na Gaddaffi wangeshitakiwa mahakamani, lakini viongozi wakumbuke si kila siku ipo fursa ya kufikishwa mahakamani kabla ya wananchi kukuhukumu wenyewe - na wao wanajua kuhukumu kuliko mahakama. Ole wao wasikumbwe na ghababu za wananchi.
   
 12. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Usisahau yaliyowakuta Sadam Hussein, Gaddaffi na Abdalla Saleh wa Yemen tena hivi karibuni. Hakuna ustaarabu kiasi hicho, kama ambavyo wananchi wanamchoma moto kibaka na kumbonda kwa matufali, wanaweza kumfanyia yeyote wakipata fursa. Tuombe tu petu yasifikie huko.
   
Loading...