Assad: Sifahamu na wala sikuwai kufikiria kama ningetengeneza maadui katika kazi yangu ya CAG, ila nimesamehe mimi ni binadamu

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,873
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) aliyemaliza muda wake, Profesa Mussa Assad amesema hafahamu na wala hakuwahi kufikiria kama angeweza kutengeneza uadui wakati wa utekelezaji wa majukumu yake akiwa CAG, ila amesema kusamehe ni jambo muhimu kwa kila binadamu.

“I have never intentionally made an enemy, Sijawahi hata siku moja kufikiria ninatengeza uadui, inawezekana kuna watu niliwakwaza lakini ni kwa sababu ya kutosimamia misingi ya kazi” - Profesa Mussa Assad.

=================

Dar es salaam. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) aliyemaliza muda wake, Profesa Mussa Assad amesema hafahamu na hakuwahi kufikiri kama angeweza kutengeneza adui wakati wa utekelezaji wa majukumu yake akiwa katika ofisi hiyo.

Profesa Assad amesema huenda waliotengeneza uadui kwake ni kundi la watumishi waliokuwa wanakwenda kinyume na misingi yake ya kazi.

“I have never intentionally made an enemy, Sijawahi hata siku moja kufikiria ninatengeza uadui, inawezekana kuna watu niliwakwaza lakini ni kwa sababu ya kutosimamia misingi ya kazi,” amesema Profesa Assad.

Ametoa kauli hiyo leo Novemba 4, 2019 alipoulizwa na Mwananchi kama amesamehe wote aliokwazana nao wakati wa majukumu yake akiwa CAG.

Alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa walioshiriki Kongamano la sita la Taasisi za Kifedha za Kiislamu barani Afrika lililofanyika leo Jumatatu, Novemba 4, 2019 Jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, hakutaka kuzungumzia chochote kuhusu changamoto za ofisi hiyo, uteuzi wa anayerithi mikoba yake, wala kugusia tofauti zake na muhimili wa Bunge.

Amesema kutokana na misimamo yake ya kujali misingi ya kazi, amewahi kuwafukuza kazi watumishi wanne akiwamo rafiki yake baada ya kuthibitisha tuhuma za wizi.

“Sasa hao ndiyo wanaweza kunichukulia kama adui yao lakini kwa sababu ya misingi ya kazi, nafikiri kusameheana ni muhimu sana kwa watu wote,” amesema Profesa Assad.


Chanzo: Mwananchi
 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) aliyemaliza muda wake, Profesa Mussa Assad amesema hafahamu na wala hakuwahi kufikiria kama angeweza kutengeneza uadui wakati wa utekelezaji wa majukumu yake akiwa CAG, ila amesema kusamehe ni jambo muhimu kwa kila binadamu.
Amesemea wapi?....... Weka ushahidi!
 
CAG amestaafu kwa mujibu wa sheria. Kama wapinzani wanampenda wamwajiri maana kila mwaka wanapata hati chafu ya ubadhirifu wa pesa.

CAG Mstaafu aache kutafuta huruma ya wananchi. Yeye sio wa kwanza kushika hicho cheo, kila Mtanzania mwenye sifa alistahili kuwa CAG. Muda wake wa utumishi umeisha apumzike amefanya kazi yake.
 
Mzenji bado anaendeleza mipasho!
Akabidhi ofisi, atulie. Dunia inamjua atapata kazi nyingine tena si ajabu ikawa tamu, nene, nzuri ya heshima kuliko hii ambayo mkataba wake umeisha

Ni Mtanganyika mwenzetu huyu, mtoto wa Tanga. Mswahili alietokea Uswahilini hadi akawa Profesa.

Ajira yake ni ya kitaaluma sio za matokeo ya kukimbiza Mwenge.
 
Ninachompendea MAGU ni kitu kimoja, unaweza kudhani kakutumbua,kumbe anakuandalia nafasi nzuri zaidi. Unaweza kudhani kakulazimisha ung'atuke, kumbe lengo lake akupate akuweke sehemu tamu zaidi.

Magu hajawahi acha mtu active (kama Assad) eti akakae tu nyumbani kizembe kisa kastaaafu, labda Assad aanze porojo porojo amfanye Mkuu aghairi dhamira yake, ila I believe Assad ataenda pumzishwa somewhere pazuri sana.
 
CAG amestaafu kwa mujibu wa sheria

Kama wapinzani wanampenda wamwajiri maana kila mwaka wanapata hati chafu ya ubadhirifu wa pesa

CAG Mstaafu aache kutafuta huruma ya Wananchi yeye sio wa kwanza kushika hicho cheo,kila Mtanzania mwenye sifa alistahili kuwa CAG

Muda wake wa utumishi umeisha apumzike amefanya kazi yake
We ni mtu wa ajabu sana
 
Ninachompendea MAGU ni kitu kimoja

unaweza kudhani kakutumbua,kumbe anakuandalia Nafasi nzuri zaidi

unaweza kudhani kakulazimisha ung'atuke,kumbe lengo lake akupate akuweke sehemu tamu zaidi

Magu hajawahi acha mtu active (kama Assad) eti akakae tu nyumbani kizembe kisa kastaaafu

Labda assad aanze porojo porojo amfanye mkuu aghairi dhamira yake,ila i believe Assad ataenda pumzishwa

somewhere Pazuri sana.
Pazuri ni peponi mkuu, kwa dhihaka hii kwa Asad, hawezi kuomba hisani kwa mkuu.
 
Ninachompendea MAGU ni kitu kimoja

unaweza kudhani kakutumbua,kumbe anakuandalia Nafasi nzuri zaidi

unaweza kudhani kakulazimisha ung'atuke,kumbe lengo lake akupate akuweke sehemu tamu zaidi

Magu hajawahi acha mtu active (kama Assad) eti akakae tu nyumbani kizembe kisa kastaaafu

Labda assad aanze porojo porojo amfanye mkuu aghairi dhamira yake,ila i believe Assad ataenda pumzishwa

somewhere Pazuri sana.
Issue ni kukwepesha ukaguzi wa pesa ambazo ni kodi zetu, hayo ya kuwekwa sehemu tamu zaidi ni maswala ya tumbo la mtu binafsi.
 
Wakuu embu tulizeni ball, Rais ni Rais, tulimpa nchi sisi wenyewe, embu tumuache afanye kazi yake. Kila mtu anapenda kufanya kazi na watu anaowaamini, nadhani tumwache afanye kazi na wale anaowaamini.
 
CV ya CAG inamfanya aishi popote na kupata kazi ya taaluma zake. Au hata asipoajiriwa anaweza akajiajiri.
Hana njaa.
Wasomi smart kuikimbia Afrika na kufanya kazi kunufaisha mataifa ya nje si kwamba si wazalendo, la, hawataki kutumika na wanasiasa kudhalilisha taaluma zao. Unawaacha vipi wataalamu smart kina Muhongo unakumbatia waliozungusha darasani?
 
CAG amestaafu kwa mujibu wa sheria. Kama wapinzani wanampenda wamwajiri maana kila mwaka wanapata hati chafu ya ubadhirifu wa pesa.

CAG Mstaafu aache kutafuta huruma ya wananchi. Yeye sio wa kwanza kushika hicho cheo, kila Mtanzania mwenye sifa alistahili kuwa CAG. Muda wake wa utumishi umeisha apumzike amefanya kazi yake.

Siyo wapinzani, Watanzania kwa umoja wetu tunampenda na tutaendelea kumpenda maana amesimamia kikamilifu taaluma yake.
 
Back
Top Bottom