Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam, Dr. Valentino Mokiwa avuliwa uaskofu

BVR 2015

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
315
634
Askofu wa Kanisa la Anglikana dayosisi ya Dar es Salaam ,amevuliwa uaskofu kwa utovu wa maadili ya kanisa na kukiuka miiiko ya kanisa.
==========

Sakata la Mgogoro wa Kanisa Anglikana Tanzania Dayosisi ya Dar es salaam, linazidi kuchukua sura mpya,kufuatia Askofu wa Dayosisi hiyo,Dokta Valentino Mokiwa,kugoma kujiuzulu na kustaafishwa kwa manufaa ya Kanisa hilo kama alivyotakiwa na Mhasham Askofu wa Jimbo kuu la Tanzania,Dokta Jacob Erasto Chimeledya.

Hatua ya Dokta Mokiwa,kutakiwa kufanya hivyo,ni agizo la nyumba ya maaskofu la kuundwa tume ya Askofu Mkuu wa Kanisa hilo,kuchunguza tuhuma kumi zilizokuwa zinamkabili Dokta Mokiwa,pamoja na nyinginezo, za ukosefu wa maadili,ikiwemo kufuja mali za kanisa na kuingia mikataba kiholela yenye viashiria vya rushwa katika maeneo ya Buza,ikiwemo pia kutoa daraja la Ushemasi,Upadre,na Ukanon,kwa katibu wa Dayosisi,Mkristo ambaye ametengana na mkewe na kuoa mke mwingine kiserikali kinyume na kanuni ya kanisa kuhusu ndoa.

Waandishi wa Channel Ten,wamefika katika nyumba zinazodaiwa kutelekezwa na Dokta Mokiwa ikiwemo Silver Oak ya Upanga,na ya Mtaa wa Uganda Ostabei, ambapo imedaiwa kuwa ameiacha na kwenda kupanga huku kanisa likimlipa pango la shilingi milioni 3 kwa mwezi miaka zaidi ya miaka sita.

Dokta Mokiwa jana aligoma kupokea barua yake kutoka kwa Dokta Jacob Erasto Chimeledya,na baadhi ya waamini wa kanisa hilo katika nyakati tofauti,wamezungumzia hatua ya kutakiwa kujiuzulu na kustaafishwa Dokta Mokiwa.

Katika hatua nyingine,Dokta Valentino Leonard Mokiwa,kupitia kwa Afisa habari wake,Yohana Sanha,amedai kuwa mchakato uliotumika kumuhukumu ni batili na kwamba bado yeye ni Mkuu wa Dayosisi ya Dar es salaam.

CHANZO: Muungwana
======

Maoni ya WanaJF yamesomwa kwenye kipindi hiki cha JAMII LEO
 

Attachments

  • Barua Makanisani -KAT 07-Jan-2017 16-39-17.pdf
    9.3 MB · Views: 262
Sio Kweli, naomba mwe na taarifa sahihi kwanza kabla ya kuzileta maeneo kama haya!

Hayo ni maelezo ya Askofu Mkuu ambaye pia amevunja katiba wazi kabisa!

Kwanza alitakiwa apokee mashitaka kutoka kwa standing committee, au au wajumbe 5 wa chapters ama synod ya kanisa la Dar na sio kwa wakristo 32 kama anavyodai!

Pili hata namna ya kupokea hayo mashitaka na kuyashughulikia hakufuata katiba kwa maana kuwasiliana na vyombo halali vya kisheria katika kanisa.

Tatu hata nyumba ya maaskofu haikuamua hivyo kama anavyodai na kwa ukweli alitakiwa kama Mokiwa amekaidi ushauri wa nyumba ya maaskofu basi angerudi kwanza katika nyumba ya maaskofu na kuwapa taarifa na nyumba ingeamua!

Pia tukumbuke kikatiba Askofu mkuu ni mwenyekiti tu wa nyumba ya maaskofu na kiongozi kwa First among equals!

Hata maamuzi yako hatakiwi kuyapeleka kwa washarika na kuzisambaza humu lakini anatakiwa aziwasilishe katika nyumba ya wahudumu yaani wachungaji, kamati kuu ambayo ndio chombo kikuu cha kusimamia diocese na kisha kuitisha synod ya dharura!

Ndivyo ilivyotokea kwa Baji tanga na huko Kondoa kama alivyonukuu!

Akumbuke pia amekiri kwamba amepelekewa barua ya wachungaji wote wa Dar kasoro wawili waliotengwa kumuunga mkono Askofu wao, Amepelekewa barua ya Synord nzima Kumuunga mkono Askofu wao, amepelekewa barua na mashemasi na wainjilisti wote kumuunga mkono Askofu wao, Amepelekewa barua na idara zote za uongozi diocese kumuunga mkono Askofu wao na amepelekewa barua na standing committee kumuunga mkono Askofu wao sasa yeye hata akiichukua diocese atafanya kazi na nani?!

Tukumbuke kwamba Askofu Mokiwa aliwahi kuwa askofu mkuu na waligombania cheo kimoja na huyu wa sasa na kushindwa kwa kura tatu tu! Na mwakani 2018 tutakuwa na uchaguzi wa askofu mkuu ambapo dalili zinaonyesha wazi kwamba Mokiwa angegombania na ana nafsi kubwa ya kushinda kwa hiyo hoja rahisi tu huyu mshindani wake wa cheo ndio leo amegeuka hakimu wa issue yake na anaishuughulikia na papara na haraka bila hata kufuata kanuni!

La mwisho kanisa la Dar haina mgogoro! Na Mokiwa bado ni Askofu Mkuu mstaafu na askofu wa Dar. Barua ya askofu mkuu imeshajibiwa na kamati kuu ya diocese. Kwa hiyo aendelee na siasa zake na mnaopotosha endeleeni kupotosha na Kanisa na idara zake Dar zinaendelea na kazi kuu ya utume! Wakicheza tu basi Tanzania tutakuwa na majimbo mawili. Maana ndiko tunakoelekea sasa.
 
Askofu wa Kanisa la Anglikana dayosisi ya Dar es Salaam ,amevuliwa uaskofu kwa utovu wa maadili ya kanisa na kukiuka miiiko ya kanisa.
Ngoja avuliwe tu! yaani Kanisa limejaa madudu tupu utasikia Askofu wa Tanga Kajiuzulu ooh mara Askofu mwingine alikufa kwa Ukimwi! dah! hadhi unajiuliza hili ni Kanisa au Danguro?
Hapa sasa nimekubaliana na baba yangu kwa nini alikataa kuwa Askofu wa hili Kanisa Chafu!!
 
Back
Top Bottom