Askofu wa Kanisa Katoliki-Mbeya, Evarist Chengula: Ujumbe wa maaskofu unawalenga wanafiki ambao wanajidai kuwa Wakristo

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Mbeya, Evarist Chengula kuhusu ujumbe uliotolewa hivi karibuni na maaskofu, Askofu Chengula amewataka Watanzinia kuelewa kwamba maaskofu hawana nia mbaya bali wanachotaka ni kila mtu ashiriki katika kulitakia taifa upendo wa kweli.

Ameeleza ujumbe wa maaskofu unawalenga wanafiki ambao wanajidai kuwa Wakristo lakini hawana misimamo ya Kikristo

IMG_20180330_173159.jpg


Aidha, amewataka waumini wa Kanisa hilo nchini Tanzania kuchagua viongozi sahihi na watakaokidhi mahitaji yao badala ya kufanya makosa kwa kuchagua viongozi wasiofaa na kuanza kulalamika baada ya uchaguzi.

Askofu Chengula ametoa ujumbe huo katika mahubiri aliyotoa kwenye ibada ya Ijumaa Kuu inayofanyika katika Kanisa la Bikira Maria wa Fatima Parokia ya Mtakifu Francisco wa Asizi, Mwanjelwa mkoani Mbeya.

Amesema imekuwa ni kawaida kwa maaskofu na wadau wengine kuanza kukosoa viongozi baada ya uchaguzi, jambo ambalo halina faida sana, na hivyo wao kama maaskofu mwaka huu wameamua kuwataka waumini wao kuwapima kwa umakini watu wote watakaojitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi zijazo kwa kuanzia na uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwakani.

“Ni vita yetu sote, tukipata viongozi wabaya tunaumia wote, tukipata viongozi wazuri tutafurahi wote, kila mmoja aone kiu ya Tanzania hii kuwa nchi ya upendo,” amesema askofu huyo.

Amesema wanachokifanya viongozi wa dini si kuwaelekeza waumini wao chama cha kuchagua, bali kuwapima wagombea kabla ya kuwachagua kwani endapo chama kitaweka mgombea asiyefaa, waumini watalazimika kumchagua hata kama hafai.
 
Hao ndio viongozi wa miili na roho zetu,haiwezekani kumjenga mtu kimwili wakati roho/nafsi ipo kwenye masumbuko ya

.Kisiasa
.Kiuchumi.
.Kijamii
.Kisaikolojia nk

Hongera baba askofu
 
Huyu askofu alikuwa neutral na amesisitiza msianze kupotosha. Hajalenga chama chochote over. Sio mje wale wazee wa civil war muanze kuungaunga viudaku vyenu.
 
Asante Baba kwa kuongea ukweli Pengo hafai kuendelea kuwa Askofu.
Ni vita yetu sote, tukipata viongozi wabaya tunaumia wote, tukipata viongozi wazuri tutafurahi wote, kila mmoja aone kiu ya Tanzania hii kuwa nchi ya upendo,” amesema askofu huyo.
 
Back
Top Bottom