Askofu Tibanenason aunga mkono Rais kusaini Muswada wa Marekebisha ya Katiba 2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu Tibanenason aunga mkono Rais kusaini Muswada wa Marekebisha ya Katiba 2011

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mnyamahodzo, Dec 3, 2011.

 1. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Askofu Tibanenason wa Kanisa La Pentekoste Tanzania (KLPT) akiwa katika kutoa Tamko la Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara amesema "Sisi tunaunga mkono hatua ya Rais kusaini Muswada wa Marekebisha ya Katiba". " Rais ni kiongozi wa juu wa nchi, yeye ndiye anayeamua tufanye nini ..., ninyi mnasoma Biblia, hebu fikiri Mungu angekuja kuwaambia anataka kutunga amri 10 halafu akawaambia ataweka Usizini, Usiibe, Usiseme uongo,... Semeni, nani angekubali?

  Source: Patapata ya Redio WAPO.

  My take: Askofu Tibanenason, umekosea sana, umetufadhaisha wengi. Hamlielewi jambo hili, basi nyamazeni kimya kuliko kuja na kauli mbovu (siyo tata) kama hizi.

  Kuipa nguvu hoja yake mfano aliotoa kwanza ni wa kiwango cha chini lakini pili hauhusiani na hoja ya msingi. Mungu ni Mungu, na wanadamu ni wanadamu. Utawala wa Mungu ni tofaut na utawala wa wanadamu. Utawala wa wanadamu unajaribu kucopy ule wa Mungu lakini bado gap ni kubwa mno. Askofu amesahau kuwa faida nyingine za Mungu kuweka amri hizo ni kurahisha utawala wa wanadamu miongoni mwao.

  Pili, Askofu kasahau kuwa awali katika Biblia Mungu alitaka Israel watawaliwe na Yeye na kuongozwa Waamuzi aliowachagua Yeye. Israel baadaya miaka walitaka na wao wawe na wafalme kama mataifa mengine. Jambo hili halikumfurahisha Mwamuzi Samwel, hata alipokwenda kuomba kwa Mungu.

  Mungu alikubali waisraeli kuwa na mfalme wao lakini akimwambia Samwel, hawajakukataa wewe bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao. Ndipo Samwel alipomtawaza Sauli mwana wa Kishi akatawazwa kuwa mfalme wa kwanza.

  Kikwete si Mungu, kama Mungu aliruhusu Israel wawe na mfalme wanayemtaka kwa kutawazwa na Samwel sembuse Kikwete, ili sisi tuwe na Rais wa haki kwa kutengeneza Katiba nzuri?

  Nitarudi tena.
   
 2. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #2
  Dec 3, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,075
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280

  Askofu kaongea maneno ya busara sana.. wenye masikio wasikie....

   
 3. MANAMBA

  MANAMBA Senior Member

  #3
  Dec 3, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii miaskofu uchwara injili ikiwashinda inahubiri siasa wasizozijua. Wawasaidie waumini wao kumjua Mungu na kumtii ili pamoja na shida wanazopata hapa duniani wafike mbinguni kuliko kuwafanya wakose vyote.
   
 4. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #4
  Dec 3, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Tufafanulie ubusara wa maneno yake uko wapi? Je! Kama angenyamaza kimya si angeoneka ana busara na hekima zaidi?
   
 5. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #5
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Maneno ya busara kwa mlengo wa chama tawala lakini si kwa maslahi ya taifa.
  Hakuna kiongozi wa dini kwenye biblia amepata kujikomba kwa watawala.

  Mzee Tiba anazeeka akubali hilo. Kumlinganisha JK na Mungu ni kumkufuru huyo Mungu anayemhubiri.
   
 6. prakatatumba

  prakatatumba JF-Expert Member

  #6
  Dec 3, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  He is just a layman let hm say because his mind cannot go beyond reasonable doubt.AKILI ZA MBAYUWAYU CHANGANYA NA ZAKO.
   
 7. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #7
  Dec 3, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Sasa Leo ndio nimeamini kuwa haya makanisa yanayojiita ya kipentekoste wengi wa viongozi ni vilaza hata kwenye Biblia yenyewe achilia mbali mambo ya siasa, uchumi, na kijamii. Kufananisha utendaji wa Mungu ni tusi na dharau kubwa, anathibitisha ni kwa namna gani alivyo maimuna kwenye Bible.
   
 8. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #8
  Dec 3, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Tanzani tukipata Maskofu kumi kama Askofu Tibanenason, Watanzania tutaishi kwa amani sana..

  Hongera sana Askofu Tibanenason, mpenda amani wewe ni msomi then ni mtumishi wa Mungu
   
 9. Beso

  Beso JF-Expert Member

  #9
  Dec 3, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  he is just a drug master!!try to paint himself white! Not every body "askofu" should be seen wise!
   
 10. S

  Straight JF-Expert Member

  #10
  Dec 3, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  unaona raha kabisa kwa kiongoz wa dini tena wa juu anatoka huko anamfanisha MUNGU na binadamu... Isitoshe binadamu mwenyewe ni m.k.w.e.r.e
   
 11. E

  ESAM JF-Expert Member

  #11
  Dec 3, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Askofu Tibanenason wa Kanisa La Pentekoste Tanzania (KLPT) akiwa katika kutoa tamko la miaka 50 ya Tanzania bara amesema "Sisi tunaunga mkono hatua ya Rais kusaini Muswada wa Marekebisha ya Katiba". " Rais ni kiongozi wa juu wa nchi, yeye ndiye anayeamua tufanye nini ..., ninyi mnasoma Biblia hebu fikiri Mungu angekuja kuwaambia anataka kutunga amri 10 halafu akawaambia ataweka Usizini, Usiibe, Usiseme uongo,... Semeni, nani angekubali?

  Source: Patapata ya Redio WAPO


  Huyu askofu kwa kweli huna namheshimu sana lakini kwa hili amepotosha kabisa sio tu suala la katiba bali hata neno la Mungu alitotumia amelipeleka nje ya context kabisa. Yaani amelinanisha vitu ambavyo hata haviwezi kulinganishwa hata kwa asilimia moja.
   
 12. V

  Vonix JF-Expert Member

  #12
  Dec 3, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  MNYAMAHODZO,nami nimesikiliza kipindi hicho mada umeiandika vizuri sana,inasikitisha,hawa viongozi wa dini kumbe wengi hawajausoma na kujua maudhui yaliyomo kwenye huu mswada na kukimbilia kuunga mkono kwa hatua ya rais kuupitasha,huyu askofu ndio katoa mpya kwa huo mfano wake bado hajaelewa kuwa MUNGU ATABAKI KUWA MUNGU TU,NA MAWAZO YAKE YAKO MBALI SANA NA AKILI ZA KIBINADAMU,kwa ufupi kama Mungu angeruhusu UZINZI,KUSEMA UONGO,UIZI NK,ina maana kuwa hizo na nyinginezo katika amri kumi ZISINGEKUWA DHAMBI wanadamu tusitake kumtangulia Mungu.
   
 13. B

  Bhavick JF-Expert Member

  #13
  Dec 3, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hela mbaya,kumfananisha Mungu na Jk!MUNGU IPONYE NCHI YANGU TZ,Iepushe na laana ya maaskofu WAPUMBAVU kama hawa!
   
 14. E

  ESAM JF-Expert Member

  #14
  Dec 3, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Kaazi kwelikweli, yaani rais akiamua kuwa fisadi basi tukubaliane naye? Huyu askofu simwelewi kabisa. Hata elimu yake sijui ni ya kiwango gani kama hata anashindwa kuweka logic kwenye jambo rahisi ambalo tumeona mfano wake mzuri kwa jirani zetu Kenya hivi karibuni. Jamani jamani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 15. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #15
  Dec 3, 2011
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Huyo askofu inaonekana hata Biblia yenyewe haijui. Ndo matatizo ya kukariri mistari tu.
   
 16. Vmark.

  Vmark. JF-Expert Member

  #16
  Dec 3, 2011
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 1,361
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Who is she?
   
 17. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #17
  Dec 3, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Bado shehe Ponda na Shehe Simba hawajasema hapo....weeeee!! Watumishi wa Mungu hawa.
  Za kuunga unga changanya na za m.kwere.
   
 18. REBEL

  REBEL Senior Member

  #18
  Dec 3, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mikanisa mingine bwana ,naona hata yesu anaichukia wapentekoste,wasabato mashahidi wa yehova,duh!na viongozi wao wasiitwe maaskofu maana wanashushia heshima hicho cheo.
   
 19. E

  ESAM JF-Expert Member

  #19
  Dec 3, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  We acha tu, lakini kuna wapentekoste wako smart kweli kweli, kama Mtumishi wa Mungu Kakobe huwezi kusikia anasifia upuuzi kama huu. Yeye anagonga nyundo tu
   
 20. O

  Omr JF-Expert Member

  #20
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  we kuwa na adabu na Imani za watu. Wewe uliongea na Yesu akakwambia hivyo?
   
Loading...