Askofu Stephen Munga: Usiogope Lissu! Tunaishi kama zawadi ili tupiganie haki za wanaoonewa

ANAANDIKA KWA UCHUNGU
BABA ASKOFU STEPHEN MUNGA

TUNDU LISSU: Mungu akupe kupona haraka rafiki na mwanangu wa kiroho. Nilikufahamu muda mrefu na tulipambana pamoja katika ufisadi wa madini kabla hujawa Mbunge. Ninajua roho yako ya mpambanaji jasiri, shupavu na mwaminifu.

Umekuwa sauti ya wanyonge kwa muda mrefu. Nimeendelea kukufuatilia hata ukiwa bungeni na kuona ni yuleyule ambaye hawezi kunyamazishwa na vitisho vyovyote. Umeteseka na kuteswa kwa ajili ya kupigania haki za ...wanyonge.

Nilikupigia simu mara kadhaa siku moja kabla ya hiyo siku kushambuliwa kwako lakini sikuweza kukufikia. Nilichotaka kukuambia ni maneno yaleyale ya siku zote: kwamba usiogope Lissu! Tunaishi kama zawadi ili tupiganie haki za wanaoonewa. Nilipigwa na butwaa kwa habari za kushambuliwa kwako. Ngoja damu yako iwe mikononi mwao waliofanya hivyo. Wewe utabaki kuwa shujaa katika kumbukumbu za nchi hii. Ipo siku tutaushinda uovu na haki itatawala.

Hakuna mamlaka inayoshinda nguvu na sauti ya wapigania haki. Yeyote aliyefanya hili amefanya kosa kubwa na la kiufundi. Kama utaishi au kama utakufa ujue kwamba wewe ni shujaa. Lakini nakuhakikishia jambo moja: hatutanyamazia uovu uwao wowote na kamwe hatutaacha kusimama na wale wote wanaotetea kweli na haki.

Hiyo madhabahu iliyoandaliwa kuwachinja watetea haki ipanuliwe maana hiyo iliopo ni ndogo haiwezi kuwabeba wote wenye roho na nia kama yako. Tunakufa mara moja na baada ya kufa ni uzima wa milele.

Kwetu sisi kuishi ni Kristo na kufa ni faida
Kwa mbali kuna kahurufu ka Bishop kupinga abango hili... Tusubiri
 
Mh Baba Askofu wakati ana andika haya alizingatia kuwa mwanae huyu siku hizi ni mmoja wa marubani wa ndege iliyobadili gia angani? Au ufisadi ni kwenye madini tu?

Mchina wa jF.
Na washawasha!
 
Wewe ndo mmoja wa wale aliowataja rais mnaowashwa washwa?

Angalizo usije ukakengeuka lakini. Kabrasha la mvua ya mabomu liko wapi lifutwe angalao vumbi tu. Hapo nimekumbushia marubani tu wa hiyo ndege ya kubadili gea angani bado maflight engineers.

Mchina wa jF.
Na washawasha!
 
image.jpeg
image.jpeg
 
Haya maneno sijui kama yatapita bure.
[Mungu ibariki nchi yangu].

An ant on the move does more than a dozing ox.
 
  • Thanks
Reactions: PNC

Hakika nimeamini kuwa Misahafu ya dini ni maneno ya Mwenyezi Mungu yenye historia ya Kweli. Maneno ya Huyo askofu ni mwendelezo wa haki ipatikanayo kwa njia ya mkono wa Mungu asiyeshindwa.

Askofu hongera kuna watakaokuja baadae kugundua kuwa walisimama na watesi kulinda maslahi yao wakasahau kuwa kazi yao sio kubeba taa tu bali ni kubeba taa inayowaka gizani.


Kuna viongozi wa dini wasiojitambua kuwa wao ni mabalozi wa Mungu duniani na sio mawakala wa wanasiasa na vyama vya siasa.

Kama kuna kiongozi wa dini anayeweza kupuuza roho ya mwanadamu inapoangamizwa kwa sababu ya kulinda na kuficho uovu wa watu fulani basi ajue anashindwa kuchunga kondoo wa Mungu kwa kuchunga mali za dunia na watawala.

Watawala wanalipwa mamilioni ya fedha, wanapewa majumba mazuri ya kuishi , wanapewa heshima kubwa miongoni mwa wanajamii, wanagharamikiwa safari zao, wana mamlaka makubwa waliyopewa ya kusaidia kusidia yeyote wamtakaye, wanalindwa sana lakini wana jambo la ajabu sana HOFU na WOGA wa kukosolewa pale wanapokosea iwe ni kukosea kwa bahati mbaya au makusudi.
Waoambe wa viongozi wamekuwa ni hatari zaidi mana wanajua kuwa jamii haziwakubali hivyo wanajikuta wakiwa wanafanya kazi kwa vitisho.

Kwa nini wale waliofanya uovu na ufisadi unaotajwa na kulitia Taifa hasara za matrilion hawakamatwi na kuwekwa ndani masaa 48 ?
Wao wanaitwa na kuhojiwa kwa heshima lakini wale wanaosema tu bila kulitia hasara taifa hili wanakamatwa kila siku tena kwa kutimiza wajibu wao wa kikatiba.
Haki ni lazima iendane na hukumu ya haki.

Wanasiasa waliohujumu taifa hili kwa miaka mingi ndio wanaopaswa kunyimwa uhuru wa kisiasa lakini tunaona tofauti kabisa na mategemeo yetu tunaona kuwa wanaonyimwa uhuru wa kisiasa ni wale waliopiga kalele miaka yote kuhusu rasilimali zetu na bado wanasema kuwa wale waliouza rasilimali zetu bado wapo na wengine wapo madarakani na wengine ni wabunge. Haki iko wapi ya kuwalinda waliogawa mali zetu halafu tunawaandama na kuwatisha wale wasioridhika na baadhi ya watendaji na utendaji wao?
 
Back
Top Bottom