Askofu Stephen Munga: Shetani ameongeza bajeti yake ya 2019/2020 kwa kitengo cha ukiukwaji wa haki za binadamu, ukandamizaji, uonevu na maangamizi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
munga.jpg

Shetani ameongeza bajeti yake ya 2019/2020 kwa kitengo cha ukiukwaji wa haki za binadamu, ukandamizaji, uonevu na maangamizi ulimwenguni. Hizi sio habari njema hata kidogo lakini mwenye masikio ya kusikia na asikie. Kila wakati tunapovuka kutoka mwaka mmoja kwenda mwingine tunakuwa na matumaini kwamba mwaka ujao utakuwa na maisha nafuu kuliko uliotangulia. Ni vema sana kuishi katika matumaini na tunamshukuru Mungu kwa kutupa tunu hii ya matumaini. Mwaka wa 2018 umekuwa na matukio makubwa katika mataifa mbalimbali. Umekuwa mwaka wa furaha za hapa na pale lakini pia umekuwa mwaka wa maumivu na manung'uniko. Tumepata kidogo lakini tumepoteza vingi. Hapa napo tunamshukuru Mungu kwamba ametupa matumaini ya kusonga mbele na maisha. Tena tunamshukuru Yeye kwa sababu ametupa kipawa cha kusahau. Sijui kama maisha yangekuwaje ikiwa kila jambo gumu lingebaki mioyoni na nguvu zake zilezile! Tunakutana na mambo magumu ambayo yanatupiga nafsi na miili yetu lakini baada ya muda tunasahaulishwa. Asante Mungu kwa kipawa hiki cha kusahalishwa. Ni zawadi kubwa sana.

Siye Mungu anayetusababishia mateso bali ni shetani akitumia mawakala wake walioko duniani. Mara nyingi shetani huwakamata watawala, wenye mamlaka, matajiri wenye uwezo wa kupanga na kugharimia mateso ya wengine. Herode katika biblia, kwa kuwa alikuwa na mamlaka aliona ni jambo rahisi tu kumfunga gerezani Yohana Mbatizaji; na tena aliona ni rahisi zaidi kukata kichwa cha Yohana na kumpatia binti yake kama zawadi. Mamlaka na nguvu vyaweza kuwa mkono wa shetani wa kutesa wengine. Watawala na wenye uwezo wengi mara kadhaa wametumia nguvu zao kusababishia wengine mateso na vifo. Ole wao wenye hulka hiyo! Hata hivyo, kwa kuwa "nguvu" (power) ni istilahi ya uwiano (relative) hata miongoni mwa waonekanao kuwa wanyonge wapo wenye nguvu zaidi ya wengine basi hata wanyonge wanaweza kuoneana na kutesana. Mateso, umaskini na machungu mengi ya maisha ni ya kusababishiwa. Lakini ole wao wasababishao hayo kwa wengine!

Tunapoingia mwaka 2019 ndio hivyo shetani ameongeza bajeti yake katika kitengo hicho cha mateso na maangamizi. Dunia yetu haitakuwa mahali salama sana na pa furaha. Kutakuwa na mahangaiko mengi na mateso mtawanyiko. Nyanja za siasa na biashara zitakuwa kwenye pepo za kisulisuli. Damu itamwagika kwa wingi. Hayo mateso yatakuwepo kiasi cha kuzoeleka. Kelele za mabishano na ushabiki zitakuwa nyingi na maridhiano bandia yataongezeka. Mioyo ya wengi itakata tamaa na wengi watakumbwa na wimbi la usaliti wa haki na kweli. Asomaye na afahamu!

Kwa wale wana wa Mungu ni vema kujizoesha kupiga magoti na kuomba. Mambo hayo hayaepukiki na hatutayashinda kwa nguvu zetu. Bwana Yesu ambaye alituaga akitutakia amani ni Yeye pekee ambaye atakuwa amani ndani yetu. Hata pale machafuko yatakapokuwa makali huko nje, Yeye atakuwa amani yetu ndani yetu. Wakati tunapambana ulimwenguni na mifumo kandamizi kwa vitendo ni vema pia kupambana huku tukiomba. Na tena tukumbuke kwamba Bwana alitupa silaha hii ya maombi ili kwa hayo tuweze kuzibomoa mamlaka angamizi, lakini pia ili tuweze kusimama katika vipindi vya mateso na kujaribiwa. Bwana Yesu ametuahidi akisema, "Mpaka sasa hamjaomba chochote kwa jina langu. Ombeni nanyi mtapata ili furaha yenu ikamilike." (Yohana 16:24).Furaha yetu mojawapo ni kuishi katika ulimwengu wenye amani kwa njia ya watawala watawalao kwa haki. Inawezekana tulikuwa tunaomba vitu vya ovyo ambavyo Bwana alivifananisha na kama vile hatukuomba. Sasa tuombe kwa ajili ya amani na utengemano wa watu na mataifa ya ulimwengu. Umefika wakati wa kuacha maombezi ya kibiashara na kuingia katika maombezi ya kuihifadhi amani ya ulimwengu ikiwemo na nchi yetu. Haya sio maombi ya mpito bali ya kudumu kama Mtume Paulo anavyotuhimiza akisema, "Ombeni bila kukoma." Tukifanya hivyo litakuwepo tumaini la Mungu kutukumbuka na rehema zake. Nawatakia Mwaka Mpya 2019 wa matumaini
 
Baada ya wana sayansi kugundua kuwa binadamu wa kwanza aliishi Tanzania, nawashauri wapanue wigo wa alikotupiwa ibilisi.
Ni vizuri kujua jehenum alipotupiwa shetani ipo nchi gani, ukute ni Tanzania, maeneo ya Ukerewe au Chatho au Gambosh
 
Hii ni falsafa ya kiwango cha juu sana. Itafutwe ithibati yake watu tukae kwa amani kwamba hata tukifa hatutaenda mbali!!
 
Baada ya wana sayansi kugundua kuwa binadamu wa kwanza aliishi Tanzania, nawashauri wapanue wigo wa alikotupiwa ibilisi.
Ni vizuri kujua jehenum alipotupiwa shetani ipo nchi gani, ukute ni Tanzania, maeneo ya Ukerewe au Chatho au Gambosh
Mwana wa ibilisi alishajitangaza pale alipo tamka kuwa anataka watu waishi kama mashetani na sio kama malaika
 
Barikiwa sana Mtumishi. May our almight God bless you
View attachment 983006

Shetani ameongeza bajeti yake ya 2019/2020 kwa kitengo cha ukiukwaji wa haki za binadamu, ukandamizaji, uonevu na maangamizi ulimwenguni. Hizi sio habari njema hata kidogo lakini mwenye masikio ya kusikia na asikie. Kila wakati tunapovuka kutoka mwaka mmoja kwenda mwingine tunakuwa na matumaini kwamba mwaka ujao utakuwa na maisha nafuu kuliko uliotangulia. Ni vema sana kuishi katika matumaini na tunamshukuru Mungu kwa kutupa tunu hii ya matumaini. Mwaka wa 2018 umekuwa na matukio makubwa katika mataifa mbalimbali. Umekuwa mwaka wa furaha za hapa na pale lakini pia umekuwa mwaka wa maumivu na manung'uniko. Tumepata kidogo lakini tumepoteza vingi. Hapa napo tunamshukuru Mungu kwamba ametupa matumaini ya kusonga mbele na maisha. Tena tunamshukuru Yeye kwa sababu ametupa kipawa cha kusahau. Sijui kama maisha yangekuwaje ikiwa kila jambo gumu lingebaki mioyoni na nguvu zake zilezile! Tunakutana na mambo magumu ambayo yanatupiga nafsi na miili yetu lakini baada ya muda tunasahaulishwa. Asante Mungu kwa kipawa hiki cha kusahalishwa. Ni zawadi kubwa sana.

Siye Mungu anayetusababishia mateso bali ni shetani akitumia mawakala wake walioko duniani. Mara nyingi shetani huwakamata watawala, wenye mamlaka, matajiri wenye uwezo wa kupanga na kugharimia mateso ya wengine. Herode katika biblia, kwa kuwa alikuwa na mamlaka aliona ni jambo rahisi tu kumfunga gerezani Yohana Mbatizaji; na tena aliona ni rahisi zaidi kukata kichwa cha Yohana na kumpatia binti yake kama zawadi. Mamlaka na nguvu vyaweza kuwa mkono wa shetani wa kutesa wengine. Watawala na wenye uwezo wengi mara kadhaa wametumia nguvu zao kusababishia wengine mateso na vifo. Ole wao wenye hulka hiyo! Hata hivyo, kwa kuwa "nguvu" (power) ni istilahi ya uwiano (relative) hata miongoni mwa waonekanao kuwa wanyonge wapo wenye nguvu zaidi ya wengine basi hata wanyonge wanaweza kuoneana na kutesana. Mateso, umaskini na machungu mengi ya maisha ni ya kusababishiwa. Lakini ole wao wasababishao hayo kwa wengine!

Tunapoingia mwaka 2019 ndio hivyo shetani ameongeza bajeti yake katika kitengo hicho cha mateso na maangamizi. Dunia yetu haitakuwa mahali salama sana na pa furaha. Kutakuwa na mahangaiko mengi na mateso mtawanyiko. Nyanja za siasa na biashara zitakuwa kwenye pepo za kisulisuli. Damu itamwagika kwa wingi. Hayo mateso yatakuwepo kiasi cha kuzoeleka. Kelele za mabishano na ushabiki zitakuwa nyingi na maridhiano bandia yataongezeka. Mioyo ya wengi itakata tamaa na wengi watakumbwa na wimbi la usaliti wa haki na kweli. Asomaye na afahamu!

Kwa wale wana wa Mungu ni vema kujizoesha kupiga magoti na kuomba. Mambo hayo hayaepukiki na hatutayashinda kwa nguvu zetu. Bwana Yesu ambaye alituaga akitutakia amani ni Yeye pekee ambaye atakuwa amani ndani yetu. Hata pale machafuko yatakapokuwa makali huko nje, Yeye atakuwa amani yetu ndani yetu. Wakati tunapambana ulimwenguni na mifumo kandamizi kwa vitendo ni vema pia kupambana huku tukiomba. Na tena tukumbuke kwamba Bwana alitupa silaha hii ya maombi ili kwa hayo tuweze kuzibomoa mamlaka angamizi, lakini pia ili tuweze kusimama katika vipindi vya mateso na kujaribiwa. Bwana Yesu ametuahidi akisema, "Mpaka sasa hamjaomba chochote kwa jina langu. Ombeni nanyi mtapata ili furaha yenu ikamilike." (Yohana 16:24).Furaha yetu mojawapo ni kuishi katika ulimwengu wenye amani kwa njia ya watawala watawalao kwa haki. Inawezekana tulikuwa tunaomba vitu vya ovyo ambavyo Bwana alivifananisha na kama vile hatukuomba. Sasa tuombe kwa ajili ya amani na utengemano wa watu na mataifa ya ulimwengu. Umefika wakati wa kuacha maombezi ya kibiashara na kuingia katika maombezi ya kuihifadhi amani ya ulimwengu ikiwemo na nchi yetu. Haya sio maombi ya mpito bali ya kudumu kama Mtume Paulo anavyotuhimiza akisema, "Ombeni bila kukoma." Tukifanya hivyo litakuwepo tumaini la Mungu kutukumbuka na rehema zake. Nawatakia Mwaka Mpya 2019 wa matumaini
 
  • Thanks
Reactions: PNC

Ujumbe mzuri sana baba askofu ,Mungu akubariki naamini ujumbe umefika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom