Askofu Stephen Munga: Je, Musiba amekuwa Mfalme wa Wafalme, Bwana wa Mabwana?

Mheikungu

JF-Expert Member
Oct 15, 2018
213
446
Anaandika Mheshimiwa baba Askofu Dk. Stephen Munga Mkuu wa KKKT dayosisi ya kaskazini Mashariki

JE, MUSIBA AMEKUWA MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA?!

Ikiwa ni kweli. Narudi a tena: Ikiwa ni kweli kwamba Musiba ameanza kuwashambulia Marais waliotangulia basi tumeingia katika tatizo kubwa. Nasema haya kwa sababu kuu zilizo dhahiri.

Kwanza, niseme kwamba mimi binafsi sijawahi kumsema Rais yeyote wa taifa langu hadharani.! Nimefanya kazi wakati wa Rais Mstaafu Mkapa na Rais Mstaafu Kikwete. Nilikuwa na desturi ya kuwaona kila nilipokuwa na neno la kuongea nao na walinisikiliza kwa uvumililivu wote. Mazungumzo yetu hayakuwa mepesi wakati mwingine lakini tulifikia mwisho mwema. Hawajawahi kunitishia uhai wangu na zaidi sana waliweka ulinzi ili niwe salama. Sijawahi kumvunjia heshima Rais yeyote wa taifa langu na kwa hakika hata Rais wangu Magufuli sitamvunjia heshima. Nimefanya hivyo kwa kuzingatia hatari na athari za zinazoweza kutokea iwapo Rais wa nchi atavunjiwa heshima. Taasisi ya Urais lazima iheshimiwe na lazima ilindwe kwa ajili ya umoja na ustawi wa nchi na taifa. Kwa hali hiyo nimekuwa mtumishi na mwanaharakati wa uzalendo wa nchi na taifa langu kwa miaka mingi kuliko Musiba.

Rais John Pombe Magufuli hakuingia madarakani kwa mapinduzi bali kwa kukabidhiwa ofisi na watangulizi wake wa CCM. Niweke wazi jambo moja. Wakati Rais Mstaafu Kikwete anakwenda Dodoma kwenye Mkutano Mkuu wa kuchagua mgombea wa CCM alitokea Tanga na alifanya mazungumzo nami. Sikilizeni hotuba yake kwa Mkutano Mkuu wa CCM ambapo alitaja kwa kifupi maoni yangu na kunitaja kwa jina. Acheni mambo yenu yanayochanganya wananchi! Nchi hii haikuzaliwa baada ya uchaguzi wa 2015 na naweka mambo haya wazi ili anayetaka kunikamata afanye hivyo. Tena nchi hii haiongozwi na kuwa salama kutoka Ikulu na TISS. Nchi na taifa hili ni moja kwa sababu wananchi wake walishirikishwa katika ulinzi na maendeleo ya taifa lao.

Mimi nikiwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Lund, Sweden nilipanga kuonana na Baba wa Taifa letu Mwalimu Nyerere. Kwa mapenzi ya Mungu alimuita mbinguni kabla hatujaonana na alizikwa wakati ningali nje ya nchi kwa hiyo sikushiriki hata mazishi yake. Nilitaka kuonana naye kwa lengo la kuzungumzia hatma ya nchi yetu kwa wakati ule.

Tunaipenda nchi yetu na sisi ni wazalendo waliokubuhu juu ya taifa hili kuliko huyo Musiba anayejifanya ni mwana harakati wa Rais. Rais wa awamu ya tano hakuingia madarakani kwa mapinduzi bali kwa utaratibu wa vikao rasmi vya CCM vya kuchagua wagombea wake. CCM katika mshikamano na umoja wake wakampigania mgombea wao kushinda nafasi ya urais na akashinda. Nijuavyo mimi hapajawahi kuwa na msuguano juu ya urais wa Mhe. John Pombe Magufuli isipokuwa matatizo yalijitokeza baada ya urais wake akiwa ofisini. Tena niseme wazi kwamba watu walikuwa na matumaini makubwa kwamba Rais Magufuli angeliunganisha na kuliletea maendeleo taifa letu na kujenga ustawi na demokrasia zaidi kuliko tawala zilizopita. Lakini katika kufanya hayo ni pamoja na kutambua kwamba amekalia kiti alichokabidhiwa kwa urithishaji wa madaraka na sio kwa mapinduzi ya nchi. Nimelitetea taifa langu kwenye makongamano mengi ya kitaifa na kimataifa japo si mtumishi wa umma. Jubilee 2000 kudai Afrika ifutiwe madeni nilikuwa mstari wa mbele nikiwa bado nje ya nchi. Asante sana Mhe. Mkapa kwa kutambua mchango wangu na wa makanisa katika kampeni hii kubwa ya kimataifa.

Mimi sasa ni mzee na siogopi kifo. Miaka aliyonipa Mungu kumtumikia na kutumikia taifa langu inatosha na kamwe sina cha kulalamika. Nchi na taifa hili halikustawi toka Ikulu na TISS bali ni matokeo ya mshikamano wa wadau mbalimbali zikiwemo NGO na wananchi wote kwa jumla. Uzalendo wa taifa unajengwa katika mshikamano wa jinsi hiyo na si vinginevyo.

Lakini naona uchungu kuona viongozi wa taifa hili wanadhalilishwa na kunyanyaswa na mtu mmoja anayejiita mwanaharakati wa Rais na eti sisi sote tunatakiwa tuogope na kukaa kimya. HAPANA. Taifa hili limefika tulipo kwa sababu tumekuwa na viongozi waliolifikisha 2015 wakati Rais Magufuli anachaguliwa.

Tanzania ni taifa kubwa kuliko marais wake sembuse kidudu mtu Musiba! Inakuwaje leo Musiba anachafua viongozi waliolibeba na kulivusha taifa hili kwenye mawimbi na misukosuko na tunatakiwa eti tukae kimya! Tanzania isingekuwepo kama sio Mwl. Nyerere, Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na Mzee Kikwete. Hawa wanayo heshima ya kipekee katika Tanzania ya leo na kama hatuoni hivyo basi kuna tatizo kubwa. Musiba anachokifanya analiweka taifa letu mahali pagumu sana na hatuko tayari kwenda safari hiyo.

Mimi sikatai kwamba kama wapo walioihujumu nchi wasichukuliwe hatua. Miaka ya 2010s nilikuwa Ghana na kule aliyekuwa Rais wakati huo ni marehemu Rais Prof. Miller. Huyu alianzisha mahakama maalum ya wahujumu wa uchumi ambapo wote waliotuhumiwa walitokea kwenye jopo la majaji kujibu tuhuma zao. Huu ulikuwa mchakato na mfumo rasmi wa kushughulika na mambo. Nilifuatilia sana kesi zile na niliona kuwa utaratibu uliofuatwa ulikuwa wa wazi (transparent) na ulikuwa rasmi kwa maana ya kwamba ulizingatia taratibu za kisheria katika kutoa haki kwa watuhumiwa. Iwapo hapa kwetu tungefuata taratibu za jinsi hiyo nisingekuwa na neno. Tatizo nilionalo ni kwamba taifa zima tunamtazama Musiba kama mahakama ya kutuhumu na kuhukumu viongozi na watu wengine na kuona kwamba ni sahihi. HAPANA! HAPANA! HAPANA!

Musiba, kwa kuwatuhumu viongozi wakuu wa nchi na wengine, analiweka taifa zima katika mawimbi ya uharibifu. Mimi sijui ni nani anampa kinga Musiba lakini niseme tu kwamba kwa muelekeo huu hakuna aliye salama. Musiba ni kiumbe hatari kwa umoja, usalama, na mshikamano wa taifa. Musiba anafifisha uwezekano wa uzalendo kwa nchi na taifa letu. Iwapo anachokifanya Musiba ni mkakati uliopangwa kwa malengo yeyote, basi malengo hayo yatafeli.

Hatuwezi kuona viongozi wa taifa hili waliotumikia hadi kukabidhi madaraka kwa utawala huu wakinyanyaswa na mtu asiye na heshima. Tumevumiliana mengi kwa ajili ya ustawi na amani ya nchi hii lakini Musiba anavuruga nchi. HAPANA! HAPANA! HAPANA! Hatuna shida ya kuwepo mfumo rasmi wa kushughulikia tuhuma anazosema Musiba lakini Musiba hana cheo na sifa za kuwa hakimu kwa mambo ya viongozi wa taifa letu na CCM waliotangulia. Nimeyasema haya kwa dhamiri yangu safi. Ikiwa itanigharimu kifo niko tayari.

Nasema kama Mchungaji Dkt. Martin Luther: Hapa nasimama, Mungu nisaidie. (Here I stand, God help me).
 
Anaandika Mheshimiwa baba Askofu Dk. Stephen Munga Mkuu wa KKKT dayosisi ya kaskazini Mashariki

JE, MUSIBA AMEKUWA MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA?!

Ikiwa ni kweli. Narudi a tena: Ikiwa ni kweli kwamba Musiba ameanza kuwashambulia Marais waliotangulia basi tumeingia katika tatizo kubwa. Nasema haya kwa sababu kuu zilizo dhahiri. Kwanza, niseme kwamba mimi binafsi sijawahi kumsema Rais yeyote wa taifa langu hadharani.! Nimefanya kazi wakati wa Rais Mstaafu Mkapa na Rais Mstaafu Kikwete. Nilikuwa na desturi ya kuwaona kila nilipokuwa na neno la kuongea nao na walinisikiliza kwa uvumililivu wote. Mazungumzo yetu hayakuwa mepesi wakati mwingine lakini tulifikia mwisho mwema. Hawajawahi kunitishia uhai wangu na zaidi sana waliweka ulinzi ili niwe salama. Sijawahi kumvunjia heshima Rais yeyote wa taifa langu na kwa hakika hata Rais wangu Magufuli sitamvunjia heshima. Nimefanya hivyo kwa kuzingatia hatari na athari za zinazoweza kutokea iwapo Rais wa nchi atavunjiwa heshima. Taasisi ya Uraisi lazima iheshimiwe na lazima ilindwe kwa ajili ya umoja na ustawi wa nchi na taifa. Kwa hali hiyo nimekuwa mtumishi na mwanaharakati wa uzalendo wa nchi na taifa langu kwa miaka mingi kuliko Musiba.

Rais John Pombe Magufuli hakuingia madarakani kwa mapinduzi bali kwa kukabidhiwa ofisi na watangulizi wake wa CCM. Niweke wazi jambo moja. Wakati Rais Mstaafu Kikwete anakwenda Dodoma kwenye Mkutano Mkuu wa kuchagua mgombea wa CCM alitokea Tanga na alifanya mazungumzo nami. Sikilizeni hotuba yake kwa Mkutano Mkuu wa CCM ambapo alitaja kwa kifupi maoni yangu na kunitaja kwa jina. Acheni mambo yenu yanayochanganya wananchi! Nchi hii haikuzaliwa baada ya uchaguzi wa 2015 na naweka mambo haya wazi ili anayetaka kunikamata afanye hivyo. Tena nchi hii haiongozwi na kuwa salama kutoka Ikulu na TISS. Nchi na taifa hili ni moja kwa sababu wananchi wake walishirikishwa katika ulinzi na maendeleo ya taifa lao.

Mimi nikiwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Lund, Sweden nilipanga kuonana na Baba wa Taifa letu Mwalimu Nyerere. Kwa mapenzi ya Mungu alimuita mbinguni kabla hatujaonana na alizikwa wakati ningali nje ya nchi kwa hiyo sikushiriki hata mazishi yake. Nilitaka kuonana naye kwa lengo la kuzungumzia hatma ya nchi yetu kwa wakati ule. Tunaipenda nchi yetu na sisi ni wazalendo waliokubuhu juu ya taifa hili kuliko huyo Musiba anayejifanya ni mwana harakati wa Rais. Rais wa awamu ya tano hakuingia madarakani kwa mapinduzi bali kwa utaratibu wa vikao rasmi vya CCM vya kuchagua wagombea wake. CCM katika mshikamano na umoja wake wakampigania mgombea wao kushinda nafasi ya urais na akashinda. Nijuavyo mimi hapajawahi kuwa na msuguano juu ya urais wa Mhe. John Pombe Magufuli isipokuwa matatizo yalijitokeza baada ya urais wake akiwa ofisini. Tena niseme wazi kwamba watu walikuwa na matumaini makubwa kwamba Rais Magufuli angeliunganisha na kuliletea maendeleo taifa letu na kujenga ustawi na demokrasia zaidi kuliko tawala zilizopita. Lakini katika kufanya hayo ni pamoja na kutambua kwamba amekalia kiti alichokabidhiwa kwa urithishaji wa madaraka na sio kwa mapinduzi ya nchi. Nimelitetea taifa langu kwenye makongamano mengi ya kitaifa na kimataifa japo si mtumishi wa umma. Jubilee 2000 kudai Afrika ifutiwe madeni nilikuwa mstari wa mbele nikiwa bado nje ya nchi. Asante sana Mhe. Mkapa kwa kutambua mchango wangu na wa makanisa katika kampeni hii kubwa ya kimataifa.

Mimi sasa ni mzee na siogopi kifo. Miaka aliyonipa Mungu kumtumikia na kutumikia taifa langu inatosha na kamwe sina cha kulalamika. Nchi na taifa hili halikustawi toka Ikulu na TISS bali ni matokeo ya mshikamano wa wadau mbalimbali zikiwemo NGO na wananchi wote kwa jumla. Uzalendo wa taifa unajengwa katika mshikamano wa jinsi hiyo na si vinginevyo.

Lakini naona uchungu kuona viongozi wa taifa hili wanadhalilishwa na kunyanyaswa na mtu mmoja anayejiita mwanaharakati wa Rais na eti sisi sote tunatakiwa tuogope na kukaa kimya. HAPANA. Taifa hili limefika tulipo kwa sababu tumekuwa na viongozi waliolifikisha 2015 wakati Rais Magufuli anachaguliwa. Tanzania ni taifa kubwa kuliko marais wake sembuse kidudu mtu Musiba! Inakuwaje leo Musiba anachafua viongozi waliolibeba na kulivusha taifa hili kwenye mawimbi na misukosuko na tunatakiwa eti tukae kimya! Tanzania isingekuwepo kama sio Mwl. Nyerere, Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na Mzee Kikwete. Hawa wanayo heshima ya kipekee katika Tanzania ya leo na kama hatuoni hivyo basi kuna tatizo kubwa. Musiba anachokifanya analiweka taifa letu mahali pagumu sana na hatuko tayari kwenda safari hiyo.

Mimi sikatai kwamba kama wapo walioihujumu nchi wasichukuliwe hatua. Miaka ya 2010s nilikuwa Ghana na kule aliyekuwa Rais wakati huo ni marehemu Rais Prof. Miller. Huyu alianzisha mahakama maalum ya wahujumu wa uchumi ambapo wote waliotuhumiwa walitokea kwenye jopo la majaji kujibu tuhuma zao. Huu ulikuwa mchakato na mfumo rasmi wa kushughulika na mambo. Nilifuatilia sana kesi zile na niliona kuwa utaratibu uliofuatwa ulikuwa wa wazi (transparent) na ulikuwa rasmi kwa maana ya kwamba ulizingatia taratibu za kisheria katika kutoa haki kwa watuhumiwa. Iwapo hapa kwetu tungefuata taratibu za jinsi hiyo nisingekuwa na neno. Tatizo nilionalo ni kwamba taifa zima tunamtazama Musiba kama mahakama ya kutuhumu na kuhukumu viongozi na watu wengine na kuona kwamba ni sahihi. HAPANA! HAPANA! HAPANA!

Musiba, kwa kuwatuhumu viongozi wakuu wa nchi na wengine, analiweka taifa zima katika mawimbi ya uharibifu. Mimi sijui ni nani anampa kinga Musiba lakini niseme tu kwamba kwa muelekeo huu hakuna aliye salama. Musiba ni kiumbe hatari kwa umoja, usalama, na mshikamano wa taifa. Musiba anafifisha uwezekano wa uzalendo kwa nchi na taifa letu. Iwapo anachokifanya Musiba ni mkakati uliopangwa kwa malengo yeyote, basi malengo hayo yatafeli. Hatuwezi kuona viongozi wa taifa hili waliotumika hadi kukabidhi madaraka kwa utawala huu wakinyanyaswa na mtu asiye na heshima. Tumevumiliana mengi kwa ajili ya ustawi na amani ya nchi hii lakini Musiba anavuruga nchi. HAPANA! HAPANA! HAPANA! Hatuna shida ya kuwepo mfumo rasmi wa kushughulikia tuhuma anazosema Musiba lakini Musiba hana cheo na sifa za kuwa hakimu kwa mambo ya viongozi wa taifa letu na CCM waliotangulia. Nimeyasema haya kwa dhamiri yangu safi. Ikiwa itanigharimu kifo niko tayari. Nasema kama Mchungaji Dkt. Martin Luther: Hapa nasimama, Mungu nisaidie. (Here I stand, God help me).

Mimi sikatai kwamba kama wapo walioihujumu nchi wasichukuliwe hatua.
Hapana baba Askofu, mende walikuwa wengi sana ndani ya nyumba, hukuna njia rahisi ya kuwaondoa zaidi ya kupuliza dawa kali kila sehemu.

Nchi ilikuwa imeshikiliwa na kikundi cha watu wachache waliotaka kupokezana madaraka wenyewe kwa wenyewe.

Vijana waliharibika na madawa ya kulevya, tembo waliuawa, masikini walionewa bila ya mtetezi.
 
Anajisahau sana huyu Cyprian Musiba, ila kwakua yeye ni mwandishi wa habari acha tumkumbushe historia ya wana-habari wenzake wakiokutana na sekeseke la uchochezi wa machafuko. Waandishi waitwae FERDINAND NAHIMANA (Muasisi wa "Radio Mille Collines") alieshtakiwa sambamba na mwandishi wa gazetti HASSAN NGEZE na JEAN-BOSCO BARAYAGWIZA.

Walishtakiwa kwa kuchochea MACHAFUKO ya nchini rwanda mnamo miaka ya 1994, kwa kuandika habari za uchochezi na machafuko ya kikabila.

Mahakama Ya Uhalifu Ya Rwanda na Burundi (Iliokua Arusha) iliwatia hatiani December 2003 kwa kutenda makosa ya kivita sambamba na mauwaji pamoja na UCHOCHEZI WA MACHAFUKO YA KIMBALI.

NAHAMIA na NGEZE walihukumiwa kifungo cha maisha jela (kifungo ambacho kilishushwa mpaka 30 na 35). BARAYAGWIZA alihukumiwa kifungo cha miaka 35.

#Ipo siku atachagua kunyoa au kusuka tu. Time will tell.
 
Hapana baba Askofu, mende walikuwa wengi sana ndani ya nyumba, hukuna njia rahisi ya kuwaondoa zaidi ya kupuliza dawa kali kila sehemu.

Nchi ilikuwa imeshikiliwa na kikundi cha watu wachache waliotaka kupokezana madaraka wenyewe kwa wenyewe.

Vijana waliharibika na madawa ya kulevya, tembo waliuawa, masikini walionewa bila ya mtetezi.

I quote “Rais John Pombe Magufuli hakuingia madarakani kwa mapinduzi bali kwa kukabidhiwa ofisi na watangulizi wake wa CCM” hao watangulizi wake waliomkabidhi ofisi ndio Wamekua Mende sasa
 
kinachofanyika ni kuliondoa azimio la Zanzibar na kurudisha azimio la Arusha.
 
Asante Baba Askofu.Kutunza amani ya nchi ni pamoja na kuheshimu viongozi wastaafu .Kwa mwendo huu wa kutukana viongozi wastaafu na viongozi wa serikali na chama waliopo kukaa kimya bila kukemea . 2020 kitaeleweka.Tanzania Ina watu wakimya Lakini Sio wapole.Mkinywa na mpole Ni watu wawili tofauti.Mkimywa ni mtu hatari kuliko mpole.
 
Asante sana kiongozi wetu wa kiroho.

Wale wazee waliotoa Waraka walisema, Musiba anakingiwa kifua na kama hakukemewa hata muacha mtu.

Nusiba hakurupuki na haya anayokuja nayo, yanapangwa na anapewa na anaambiwa wakati wa kuyatoa.

Baba tunakushukuru, huu ni wakati muafaka biongozi wote wa kidini kukemea hii tabia inayotuletea mtafaruko nchini kwetu.
 
Anaandika Mheshimiwa baba Askofu Dk. Stephen Munga Mkuu wa KKKT dayosisi ya kaskazini Mashariki

JE, MUSIBA AMEKUWA MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA?!

Ikiwa ni kweli. Narudi a tena: Ikiwa ni kweli kwamba Musiba ameanza kuwashambulia Marais waliotangulia basi tumeingia katika tatizo kubwa. Nasema haya kwa sababu kuu zilizo dhahiri. Kwanza, niseme kwamba mimi binafsi sijawahi kumsema Rais yeyote wa taifa langu hadharani.! Nimefanya kazi wakati wa Rais Mstaafu Mkapa na Rais Mstaafu Kikwete. Nilikuwa na desturi ya kuwaona kila nilipokuwa na neno la kuongea nao na walinisikiliza kwa uvumililivu wote. Mazungumzo yetu hayakuwa mepesi wakati mwingine lakini tulifikia mwisho mwema. Hawajawahi kunitishia uhai wangu na zaidi sana waliweka ulinzi ili niwe salama. Sijawahi kumvunjia heshima Rais yeyote wa taifa langu na kwa hakika hata Rais wangu Magufuli sitamvunjia heshima. Nimefanya hivyo kwa kuzingatia hatari na athari za zinazoweza kutokea iwapo Rais wa nchi atavunjiwa heshima. Taasisi ya Uraisi lazima iheshimiwe na lazima ilindwe kwa ajili ya umoja na ustawi wa nchi na taifa. Kwa hali hiyo nimekuwa mtumishi na mwanaharakati wa uzalendo wa nchi na taifa langu kwa miaka mingi kuliko Musiba.

Rais John Pombe Magufuli hakuingia madarakani kwa mapinduzi bali kwa kukabidhiwa ofisi na watangulizi wake wa CCM. Niweke wazi jambo moja. Wakati Rais Mstaafu Kikwete anakwenda Dodoma kwenye Mkutano Mkuu wa kuchagua mgombea wa CCM alitokea Tanga na alifanya mazungumzo nami. Sikilizeni hotuba yake kwa Mkutano Mkuu wa CCM ambapo alitaja kwa kifupi maoni yangu na kunitaja kwa jina. Acheni mambo yenu yanayochanganya wananchi! Nchi hii haikuzaliwa baada ya uchaguzi wa 2015 na naweka mambo haya wazi ili anayetaka kunikamata afanye hivyo. Tena nchi hii haiongozwi na kuwa salama kutoka Ikulu na TISS. Nchi na taifa hili ni moja kwa sababu wananchi wake walishirikishwa katika ulinzi na maendeleo ya taifa lao.

Mimi nikiwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Lund, Sweden nilipanga kuonana na Baba wa Taifa letu Mwalimu Nyerere. Kwa mapenzi ya Mungu alimuita mbinguni kabla hatujaonana na alizikwa wakati ningali nje ya nchi kwa hiyo sikushiriki hata mazishi yake. Nilitaka kuonana naye kwa lengo la kuzungumzia hatma ya nchi yetu kwa wakati ule. Tunaipenda nchi yetu na sisi ni wazalendo waliokubuhu juu ya taifa hili kuliko huyo Musiba anayejifanya ni mwana harakati wa Rais. Rais wa awamu ya tano hakuingia madarakani kwa mapinduzi bali kwa utaratibu wa vikao rasmi vya CCM vya kuchagua wagombea wake. CCM katika mshikamano na umoja wake wakampigania mgombea wao kushinda nafasi ya urais na akashinda. Nijuavyo mimi hapajawahi kuwa na msuguano juu ya urais wa Mhe. John Pombe Magufuli isipokuwa matatizo yalijitokeza baada ya urais wake akiwa ofisini. Tena niseme wazi kwamba watu walikuwa na matumaini makubwa kwamba Rais Magufuli angeliunganisha na kuliletea maendeleo taifa letu na kujenga ustawi na demokrasia zaidi kuliko tawala zilizopita. Lakini katika kufanya hayo ni pamoja na kutambua kwamba amekalia kiti alichokabidhiwa kwa urithishaji wa madaraka na sio kwa mapinduzi ya nchi. Nimelitetea taifa langu kwenye makongamano mengi ya kitaifa na kimataifa japo si mtumishi wa umma. Jubilee 2000 kudai Afrika ifutiwe madeni nilikuwa mstari wa mbele nikiwa bado nje ya nchi. Asante sana Mhe. Mkapa kwa kutambua mchango wangu na wa makanisa katika kampeni hii kubwa ya kimataifa.

Mimi sasa ni mzee na siogopi kifo. Miaka aliyonipa Mungu kumtumikia na kutumikia taifa langu inatosha na kamwe sina cha kulalamika. Nchi na taifa hili halikustawi toka Ikulu na TISS bali ni matokeo ya mshikamano wa wadau mbalimbali zikiwemo NGO na wananchi wote kwa jumla. Uzalendo wa taifa unajengwa katika mshikamano wa jinsi hiyo na si vinginevyo.

Lakini naona uchungu kuona viongozi wa taifa hili wanadhalilishwa na kunyanyaswa na mtu mmoja anayejiita mwanaharakati wa Rais na eti sisi sote tunatakiwa tuogope na kukaa kimya. HAPANA. Taifa hili limefika tulipo kwa sababu tumekuwa na viongozi waliolifikisha 2015 wakati Rais Magufuli anachaguliwa. Tanzania ni taifa kubwa kuliko marais wake sembuse kidudu mtu Musiba! Inakuwaje leo Musiba anachafua viongozi waliolibeba na kulivusha taifa hili kwenye mawimbi na misukosuko na tunatakiwa eti tukae kimya! Tanzania isingekuwepo kama sio Mwl. Nyerere, Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na Mzee Kikwete. Hawa wanayo heshima ya kipekee katika Tanzania ya leo na kama hatuoni hivyo basi kuna tatizo kubwa. Musiba anachokifanya analiweka taifa letu mahali pagumu sana na hatuko tayari kwenda safari hiyo.

Mimi sikatai kwamba kama wapo walioihujumu nchi wasichukuliwe hatua. Miaka ya 2010s nilikuwa Ghana na kule aliyekuwa Rais wakati huo ni marehemu Rais Prof. Miller. Huyu alianzisha mahakama maalum ya wahujumu wa uchumi ambapo wote waliotuhumiwa walitokea kwenye jopo la majaji kujibu tuhuma zao. Huu ulikuwa mchakato na mfumo rasmi wa kushughulika na mambo. Nilifuatilia sana kesi zile na niliona kuwa utaratibu uliofuatwa ulikuwa wa wazi (transparent) na ulikuwa rasmi kwa maana ya kwamba ulizingatia taratibu za kisheria katika kutoa haki kwa watuhumiwa. Iwapo hapa kwetu tungefuata taratibu za jinsi hiyo nisingekuwa na neno. Tatizo nilionalo ni kwamba taifa zima tunamtazama Musiba kama mahakama ya kutuhumu na kuhukumu viongozi na watu wengine na kuona kwamba ni sahihi. HAPANA! HAPANA! HAPANA!

Musiba, kwa kuwatuhumu viongozi wakuu wa nchi na wengine, analiweka taifa zima katika mawimbi ya uharibifu. Mimi sijui ni nani anampa kinga Musiba lakini niseme tu kwamba kwa muelekeo huu hakuna aliye salama. Musiba ni kiumbe hatari kwa umoja, usalama, na mshikamano wa taifa. Musiba anafifisha uwezekano wa uzalendo kwa nchi na taifa letu. Iwapo anachokifanya Musiba ni mkakati uliopangwa kwa malengo yeyote, basi malengo hayo yatafeli. Hatuwezi kuona viongozi wa taifa hili waliotumika hadi kukabidhi madaraka kwa utawala huu wakinyanyaswa na mtu asiye na heshima. Tumevumiliana mengi kwa ajili ya ustawi na amani ya nchi hii lakini Musiba anavuruga nchi. HAPANA! HAPANA! HAPANA! Hatuna shida ya kuwepo mfumo rasmi wa kushughulikia tuhuma anazosema Musiba lakini Musiba hana cheo na sifa za kuwa hakimu kwa mambo ya viongozi wa taifa letu na CCM waliotangulia. Nimeyasema haya kwa dhamiri yangu safi. Ikiwa itanigharimu kifo niko tayari. Nasema kama Mchungaji Dkt. Martin Luther: Hapa nasimama, Mungu nisaidie. (Here I stand, God help me).
Wenye masikio na wasikie na wenye macho na waone............

Hakika Taifa linakwenda kubaya kwa huyu mtu anayeitwa Musiba, kujifanya yeye ndiye Prosecutor na wakati huo huo kuwa mahakama na kuhukumu kwa "Ex parte hearing" bila upande wa pili kusikilizwa!

Hiyo ni moja kwa moja inakiuka ile principle kuu ya natural justice, ya kuwa A MAN CAN NOT BE A JUDGE ON HIS OWN CASE
 
173 Reactions
Reply
Back
Top Bottom