Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
AMANI IWE NAWE MHE. LOWASA
Naona kumekuwa na mahangaiko mengi juu ya uamuzi wa Mhe. Edward Lowasa kurudi CCM. Huo ni uamuzi wa hiari lakini pia ni uamuzi wa kisiasa. Uamuzi wa kisiasa siku zote una maslahi. Kimaadili hatuna madai makubwa katika maamuzi ya kisiasa kwa sababu maamuzi hayo mara nyingi hayatokani na hoja za kimaadili bali yanatokana na malengo binafsi na ya kisiasa. Ndio sababu upo usemi ambao naunukuu toka kitabu changu kiitwacho “Kati ya Siasa na Amani” ukurasa 80. Kwa nukuu hii naleta fikra za jumla pasipo kumlenga mtu yeyote binafsi. Sasa nanukuu: “Kuna semi nyingi za utani hasa juu ya wana siasa. . . . Mmoja wa semi hizo ni ule usemao kwamba mwanasiasa kudai kuwa mwaminifu (honest) ni sawa na kahaba kudai kuwa bikira. . . . Ni sawa na nukuu niliyowahi kutoa juu ya Wiston Churchill aliposema kwamba mwanasiasa mzuri na mahiri ni yule ambaye anaweza kuwaambia watu juu ya mambo ambayo atayafanya katika siku zijazo na baada ya muda yasipotimilika awe na uwezo wa kurudi na kuwaambia kwa nini hayakufanyika.” Maelezo yangu yanaendelea katika kurasa zinazofuata za kitabu hicho.
Ni muhimu wakati mwingine kuyasoma na kuyajua mambo haya ambayo labda hatuyapendi lakini yanahitajika kuyajua. Siasa inagusa maisha yetu sote na kamwe si busara kuifungia milango ya maisha yetu ya kila siku. Kujua hayo kunasaidia kupunguza mishtuko pale mambo yafananayo na hili la Mhe. Lowasa yanapotokea. Hakuna jipya chini ya jua ; na asomaye na afahamu. Nenda kwa amani Mhe. Lowasa. Uamuzi wako ni sahihi maadam umeufanya wewe mwenyewe. Maisha yamejaa hatua nyingi za kufanya maamuzi na kila tunapofanya maamuzi makubwa kuna gharama zake. Bila shaka njia uliyoendea ndio uliyorudia. Nanyi mlioumia farijianeni kwa maneno hayo.