Askofu Stephen Munga: Amani iwe nawe Mhe. Lowassa mwanasiasa kudai kuwa mwaminifu (honest) ni sawa na kahaba kudai kuwa bikira

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,260
2,000
AMANI IWE NAWE MHE. LOWASA
Naona kumekuwa na mahangaiko mengi juu ya uamuzi wa Mhe. Edward Lowasa kurudi CCM. Huo ni uamuzi wa hiari lakini pia ni uamuzi wa kisiasa. Uamuzi wa kisiasa siku zote una maslahi. Kimaadili hatuna madai makubwa katika maamuzi ya kisiasa kwa sababu maamuzi hayo mara nyingi hayatokani na hoja za kimaadili bali yanatokana na malengo binafsi na ya kisiasa. Ndio sababu upo usemi ambao naunukuu toka kitabu changu kiitwacho “Kati ya Siasa na Amani” ukurasa 80. Kwa nukuu hii naleta fikra za jumla pasipo kumlenga mtu yeyote binafsi. Sasa nanukuu: “Kuna semi nyingi za utani hasa juu ya wana siasa. . . . Mmoja wa semi hizo ni ule usemao kwamba mwanasiasa kudai kuwa mwaminifu (honest) ni sawa na kahaba kudai kuwa bikira. . . . Ni sawa na nukuu niliyowahi kutoa juu ya Wiston Churchill aliposema kwamba mwanasiasa mzuri na mahiri ni yule ambaye anaweza kuwaambia watu juu ya mambo ambayo atayafanya katika siku zijazo na baada ya muda yasipotimilika awe na uwezo wa kurudi na kuwaambia kwa nini hayakufanyika.” Maelezo yangu yanaendelea katika kurasa zinazofuata za kitabu hicho.

Ni muhimu wakati mwingine kuyasoma na kuyajua mambo haya ambayo labda hatuyapendi lakini yanahitajika kuyajua. Siasa inagusa maisha yetu sote na kamwe si busara kuifungia milango ya maisha yetu ya kila siku. Kujua hayo kunasaidia kupunguza mishtuko pale mambo yafananayo na hili la Mhe. Lowasa yanapotokea. Hakuna jipya chini ya jua ; na asomaye na afahamu. Nenda kwa amani Mhe. Lowasa. Uamuzi wako ni sahihi maadam umeufanya wewe mwenyewe. Maisha yamejaa hatua nyingi za kufanya maamuzi na kila tunapofanya maamuzi makubwa kuna gharama zake. Bila shaka njia uliyoendea ndio uliyorudia. Nanyi mlioumia farijianeni kwa maneno hayo.
FB_IMG_1551583166158.jpg
 
kirengased

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
3,949
2,000
Upinzani hakuna plan zozote za maana wala hamfanyi ubunifu wowote katika kuboresha maisha ya mnaowaongoza. Kiukweli MTU making na anayeujua uongozi na miiko yake kuendelea kukaa upinzani nijambo la kustaajabisha.
Chama no chamtu,maamuzi ni yake na ubabe nimwingi,kupelekeshana na kujikombakomba kunakopelekea kukatana hela na rushwa za ngono kumejaa! Hivi vitu vinakatisha tamaa nasasa nadhani sheria yavyama vya siasa in muhimu kuwepo. Watu watazidi kuhama na sio big deal wakifanyahivyo kwani nikuhama tuu kikundi kimoja nakuingia kingine. Hakuna cha itikadi hapa maana ccm yasasa nikama chadema ya zamani na cuf yasasa nitofauti nails tuloijuaga. Poor politics maneno meeengi maadili hakuna
 
Shirikisha ubongo
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
55,919
2,000
Upinzani kufa ni pigo kubwa, sawa tu na kufiwa na mke. Mnunuzi wa wapinzani akae akijua akiiua CHADEMA, atahamishia upinzani chumbani kwake CCM
 
Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
12,341
2,000
Upinzani hakuna plan zozote za maana wala hamfanyi ubunifu wowote katika kuboresha maisha ya mnaowaongoza. Kiukweli MTU making na anayeujua uongozi na miiko yake kuendelea kukaa upinzani nijambo la kustaajabisha.
Chama no chamtu,maamuzi ni yake na ubabe nimwingi,kupelekeshana na kujikombakomba kunakopelekea kukatana hela na rushwa za ngono kumejaa! Hivi vitu vinakatisha tamaa nasasa nadhani sheria yavyama vya siasa in muhimu kuwepo. Watu watazidi kuhama na sio big deal wakifanyahivyo kwani nikuhama tuu kikundi kimoja nakuingia kingine. Hakuna cha itikadi hapa maana ccm yasasa nikama chadema ya zamani na cuf yasasa nitofauti nails tuloijuaga. Poor politics maneno meeengi maadili hakuna
Hii inapaswa kuwa comment ya mtu asiye na kichwa kabisa, nashangaa wewe umewezaje kucomment katika hali hiyo. Hebu tupe uzoefu wako unawezaje kutoa maoni bila kuwa na kichwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
27,367
2,000
Soma hiyoooooo bikiraaaa!
Huyu Askofu hajui kitu kahaba anaweza kuwa bikira mbona wapo wanawake makahaba kibao ambao hufanya mapenzi kinyume na maumbile siku ya kuolewa anakutwa bikira kabisa hajawahi guswa.I hate this bishhop.Mahubiri yake ya kijinga jinga
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom