Askofu Shoo na Bagonza waanza mkakati wa kuwaondoa maaskofu, wachungaji wasiojihusisha na siasa. Wavunja Katiba kumuondoa Dk. Mwakitali Jimbo la Konde

Askofu Dk Shoo na Bagonza wanajitambulisha kama vinara wa kupenda haki na kutii katiba, katika Jimbo la Konde, wamedhihirisha rangi yao, wamevunja katiba ya kanisa ili kumuondoa Askofu Dk. Mwakitali.

Dk Mwakitali ni moja ya maaskofu wa KKKT ambao wamejikita katika kazi ya kichungaji zaidi na sio udalali wa kisiasa wa kutafutia wanasiasa nafasi za uongozi.

Kuna madai kwamba Bagonza na Dk Shoo wameandaa mkakati wa "kufagia" viongozi wa dini katika kanisa Hilo ambao wanajifanya wanashughulika na kazi ya uchungaji zaidi kuliko Siasa. Na wanataka wanasiasa, hasa viongozi wa CHADEMA, wapate nafasi ya kuhubiri Siasa Kila jumapili katika makanisa yote nchini ili chama hicho kichukue dola, na kisaidie kanisa Hilo kujiimarisha dhidi ya makanisa mengine.

Kama wanashindwa kutii katiba ndani ya kanisa, hawana mamlaka ya kusemea katiba ya nchi, charity begins at home. Hata katiba mpya wanayosemea Kila siku, wakipewa uongozi wa nchi pamoja na wenzao wa chadema, wataikiuka tu.
Stop meddling into religious affairs. You are a hopeless creature who has put partisanship above everything on earth.
 
Mwaikali mshenzi tu askofu gani anataka kujiona yeye ni zaid ya taasisi inayo mlipa? Kajaa kiburi, jeuri , majivuno na kila aina ya uchafu.

Huenda mnao mtetea mwaikali hamumjui au mlikuwa na maslahi naye lakini hafai kuwa askofu yule ana mambo ya hovyo kabisa namfamu kwa sababu nimesha fanya naye kazi .
Aende mahakamani! Huko nako atasema mtu wa Mungu hachangamani na sheria za kiubinadamu!
Simfahamu ila kwa kiburi alichopandikizwa na shetani, nafikiri ni ngumu sana kufanya naye kazi, dikteta Fulani! Alitakalo ndilo lazima litendeke
 
Askofu, mchungaji na siasa wapi na wapi? Wameacha kutengeneza mioyo ya watu Sasa wamehamia mwilini, Mungu atazidi kuwapa masomo.
 
Ni kweli kabisa, shoo na bagonza ni wafuasi wa upinzani wanamuunga mkono freeman mbowe. Shoo kwa kiasi kikubwa ni ukabila na utabaka. Mabwanyenye wa kimachame wanatumia ukabila kujaribu kuwavuta wachagga wafikiri wanatengwa na kubaguliwa na ccm. Kitu hicho sabaya alifanikiwa kukipiga vita hadi hai wakagundua njama hizo kwa kuona jinsi mabwanyenye wa kimachame wanawanyonya na kuwadhulumu wanyonge.
Bagonza kwa hakika simuelewi sana ila naona ni kibaraka wa makabaila na mabepari uchwara na anatumiwa na nje.
Inasikitisha kuona kanisa la pili kwa ukubwa nchini kkkt linageuzwa kichaka cha wapinga maendeleo nchini.
Hilo kanisa hata nafasi ya Pili halina kwa Tanzania,waumini wake ni wa kaeneo fulani tu Kuna sehemu hawapo kabisaaa,Mimi huku kwetu niliko Mkoa mzima nilishaona makanisa ya Kkkt matatu tu Mkoa mzima
 
Binafsi napenda kupongeza juhudi mbalimbali za mkuu wa KKKT Askofu Dr Frederick Shoo kwa kuchukia na kukemea vitendo viovu katika jamii. Ni mmoja wa viongozi wachache sana wa watu - iwe wa kisiasa, kidini au kijamii waliopaza sauti hata katika kipindi kigumu sana cha awamu ya 5 cha JPM na kina Sabaya na Makonda: watu wakiporwa mali zao, wakibaguliwa kikabila kidini na kikanda, wakipigwa marisasi, wakipotezwa na hata kuuwawa na Kanisa kuwekwa katika misukosuko huku mwenyewe Shoo akijihatarisha maisha yake kuipambania haki, amani, utu, usawa na ustawi wa Taifa letu. Aliwahi kusema mtu yoyote anayekwamisha kazi ya Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakuwepo! Kuhubiri injili peke yake kunafaa nini ikiwa watu hawatendewi haki? Sasa leo Dr Shoo anasimama kama Mkuu wa KKKT kunyoosha mambo yasiyoenda Sawa katika Kanisa analoliongoza sehemu mojawapo kwa kuwashirikisha watu wa Konde waamue hatma yao na wamefanya tena kwa amani halafu watu wachache wanamnyooshea kidole? Serious? Baba Askofu wewe ni shujaa wa Mungu, endelea kusaka haki popote pale, usieogopa shetani & co, nakuombea Mungu akutunze sana. Haki huinua Taifa.
 
Haj

Hakuna kanisa takatifu linaloonekana kwa macho.
Na isitoshe hujui historia ya kanisa katoliki au umesahau machache ya juzijuzi walivyofanywa watoto huko ulaya?
Mi sijadili historia nazungumza Sasa. Kwani haya ya akina shoo ni historia au Sasa!!!
 
Mwaikali ndie alieanzisha mgogoro dayosisi ya konde. Dayosisi kaikuta imetulia. Amekuja na agenda zake za kulazimisha kuhamisha makao makuu. Baada ya kukataliwa,akaanza kuvunja katiba. Akawa hataki kutii mamlaka yoyote. Akajiona yeye ni mkuu kuliko taasisi Lutheran. Amepewa haki yake kwa jeuri yake
 
ama wanashindwa kutii katiba ndani ya kanisa, hawana mamlaka ya kusemea katiba ya nchi, charity begins at home. Hata katiba mpya wanayosemea Kila siku, wakipewa uongozi wa nchi pamoja na wenzao wa chadema, wataikiuka tu.
Mleta mada huwezi kuaminika hata chembe kwa uandishi wako wa hovyo kabisa!
Sijui mamabo ya kanisa na katiba yao na CDM yamekujaje hapa.
Ni bora ungekaa kimya kuficha upuuzi na mihemko yako isiyotumia akili.
 
Wewe

Ukitaka angalau kushawishi watu kwa uongo, basi tafuta ukweli kwanza halafu ubadilishe kulingana na matakwa yako.
KKKT, dayosisi ni eneo linaloongozwa na Askofu na Jimbo huwa linaongozwa na Mchungaji tu.
Jimbo Ni sehemu ya eneo dogo ndani ya dayosisi linaloundwa na sharika chache ndani ya dayosisi.
Kwa hiyo umesema uongo KKKT haina Askofu wa Jimbo.
Ndio hasara ya kuchanganya Siasa na dini, wanavurugwa
 
BARAZA la Vijana wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT, Dayosisi ya Konde, limemtupia lawama Mkuu wa kanisa hilo nchini, Askofu Dk. Fredrick Shoo, likidai kuongoza mkutano wa kumwondoa Askofu wa dayosisi hiyo, Dk. Edward Mwaikali, badala ya kutafuta njia sahihi ya kumaliza mgogoro ....

[https://res]

unaofukuta.

Akisoma taarifa ya msimamo wa vijana wa dayosisi hiyo jana, Marko Mahenge, alidai Askofu Dk. Shoo amekuwa sehemu ya kukuza mgogoro huo badala ya kutafuta njia sahihi ya kujadili namna ya kushughulika na jambo hilo ambalo linaendelea kuyumbisha Dayosisi ya Konde.

Alisema kwa muda mrefu vijana walikuwa kimya wakifuatilia mwenendo ya mgogoro huo huku wakitarajia kufanyika kwa hekima na busara katika kushughulikia maridhiano ya kuhamisha makao makuu ya dayosisi hiyo kutoka mjini Tukuyu katika Wilaya ya Rungwe na kupelekwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

“Sisi vijana wa Jimbo hili la Mbeya na maeneo mengine ya dayosisi hii tunapinga vikali uamuzi wa Mkuu wa Kanisa kumwondoa Askofu Mwaikali kwenye kiti chake kwa sababu mkutano uliofanyika Machi 22, katika Ushirika wa Uyole ulikuwa batili, tunamtambua Dk. Mwaikali kuwa ndiye askofu wetu na hapa jimboni haondoka wala mchungaji au Mkuu wa Jimbo,” alisema Mahenge.

Aidha, Mahenge aliliomba Baraza la Maaskofu wa kanisa hilo nchini kuingilia kati mgogoro huo kwa kuiita halmashauri kuu ya dayosisi na viongozi wengine ili kukubaliana mambo ya kufanya.

Akizungumza wakati wa ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Ruanda, yalipo makao makuu ya Dayosisi ya Konde, Mkuu wa Jimbo, Mchungaji Nyibuko Mwambola, alisema Halmashauri Kuu haitambui mkutano ulioitishwa na Askofu Dk. Fredrick Shoo kwa madai kuwa ulikuwa batili.

Alimtupia lawama Askofu Dk. Shoo kama mkuu wa kanisa kwa kushindwa kusuluhisha mgogoro huo na kuwa sehemu ya kuchochea hali ambayo alidai inazidi kuongeza chuki na mfarakano.

Kadhalika, alisema baada ya mkutano wa kumchagua askofu mwingine, Geofrey Mwakihaba, Askofu Dk. Shoo alituma waraka kwa taasisi zote za kifedha kufunga akaunti za dayosisi.

Alisema hatua hiyo imewasababishia kushindwa kufanya malipo yoyote ikiwamo mishahara ya wachungaji na watumishi wengine wa dayosisi hiyo.

Vile vile, alidai kuwa Dk. Shoo amewatumia barua wachungaji wote wa Dayosisi ya Konde kuhudhuria kikao kinachofanyika kesho jijini Dodoma, bila kumpa taarifa Askofu wa Jimbo Dk. Mwaikali, na kwamba Halmashauri Kuu imesema naye atashiriki kikao hicho.

“Mkuu wa Kanisa ameonyesha dhahiri upande alipo kwa sababu ameshindwa kutukutanisha pamoja viongozi wa dayosisi na kujadili pamoja namna bora ya kumaliza huu mgogoro badala yake ameonesha wazi kushindwa kusimamia jambo hilo na kuchangia kuchochea suala hili, sisi tunamtambua bado Askofu Mwaikali ndiyo anasimamia dayosisi yetu ya Konde,” alisisitiza.

“Haiwezekani Mkuu wa Kanisa aitishe mkutano na kufanya uchaguzi wa kumchagua askofu mwingine, tena kwa siku moja, inaonyesha dhahiri kuna chuki binafsi na sio suala la kuhamisha makao mkuu ya dayosisi.”

Machi 22 mwaka huu Mkuu wa Kanisa la KKKT nchini, Askofu Dk Fredrick Shoo, pamoja na wajumbe 201 walifanya mkutano katika Usharika wa Uyole jijini Mbeya kwa lengo la kumaliza mgogoro huo ambapo liliibuka suala la wajumbe kutokuwa na imani na Askofu Dk. Edward Mwaikali.

Katika mkutano huo ambao uliendeshwa na Askofu Dk. Shoo na kudumu kwa saa 10, ulitumika kumchagua Askofu mwingine Mchungaji Geofrey Mwakihaba, ambaye alitangazwa mbele ya wajumbe wa mkutano.

Kutokana na uamuzi huo baadhi ya vijana wa KKKT mkoani Mbeya walieleza kuwa mchakato uliotumika kuwa ulikuwa batili.

Hata hivyo, Askofu Dk. Shoo alipotafutwa na Nipashe kwa simu jana, muda wote hakupatikana kuzungumzia suala hilo.

Mgogoro wa kwanini yahamishwe makao makuu ya dayosisi kutoka mjini Tukuyu katika Wilaya ya Rungwe na kwenda Halmashauri ya Jiji la Mbeya, ulianza kufukuta tangu mwaka 2017 hadi sasa.

Askofu Dk Shoo na Bagonza wanajitambulisha kama vinara wa kupenda haki na kutii katiba, katika Jimbo la Konde, wamedhihirisha rangi yao, wamevunja katiba ya kanisa ili kumuondoa Askofu Dk. Mwakitali.

Dk Mwakitali ni moja ya maaskofu wa KKKT ambao wamejikita katika kazi ya kichungaji zaidi na sio udalali wa kisiasa wa kutafutia wanasiasa nafasi za uongozi.

Kuna madai kwamba Bagonza na Dk Shoo wameandaa mkakati wa "kufagia" viongozi wa dini katika kanisa Hilo ambao wanajifanya wanashughulika na kazi ya uchungaji zaidi kuliko Siasa. Na wanataka wanasiasa, hasa viongozi wa CHADEMA, wapate nafasi ya kuhubiri Siasa Kila jumapili katika makanisa yote nchini ili chama hicho kichukue dola, na kisaidie kanisa Hilo kujiimarisha dhidi ya makanisa mengine.

Kama wanashindwa kutii katiba ndani ya kanisa, hawana mamlaka ya kusemea katiba ya nchi, charity begins at home. Hata katiba mpya wanayosemea Kila siku, wakipewa uongozi wa nchi pamoja na wenzao wa chadema, wataikiuka tu.
 
Afadhali umesema wakati muafaka mkuu .View attachment 2166770View attachment 2166771
FB_IMG_1646302822928.jpg
 
Askofu Dk Shoo na Bagonza wanajitambulisha kama vinara wa kupenda haki na kutii katiba, katika Jimbo la Konde, wamedhihirisha rangi yao, wamevunja katiba ya kanisa ili kumuondoa Askofu Dk. Mwakitali.

Dk Mwakitali ni moja ya maaskofu wa KKKT ambao wamejikita katika kazi ya kichungaji zaidi na sio udalali wa kisiasa wa kutafutia wanasiasa nafasi za uongozi.

Kuna madai kwamba Bagonza na Dk Shoo wameandaa mkakati wa "kufagia" viongozi wa dini katika kanisa Hilo ambao wanajifanya wanashughulika na kazi ya uchungaji zaidi kuliko Siasa. Na wanataka wanasiasa, hasa viongozi wa CHADEMA, wapate nafasi ya kuhubiri Siasa Kila jumapili katika makanisa yote nchini ili chama hicho kichukue dola, na kisaidie kanisa Hilo kujiimarisha dhidi ya makanisa mengine.

Kama wanashindwa kutii katiba ndani ya kanisa, hawana mamlaka ya kusemea katiba ya nchi, charity begins at home. Hata katiba mpya wanayosemea Kila siku, wakipewa uongozi wa nchi pamoja na wenzao wa chadema, wataikiuka tu.
Mkuu jaribu kuwa unarudia kusoma uliyoandika kabla ya kubonyeza "post".
 
Back
Top Bottom