Askofu Shoo na Askofu Bagonza wakitoa maoni yao hakuna shida, Askofu Pengo na Askofu Malasusa wakitoa maoni wanaambulia matusi

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
680
1,338
Siku za hivi karibuni nimeshuhudia jambo moja la hovyo sana kwenye mitandao ya Kijamii Nchini Tumeanza kuingilia Uhuru wa watu pindi pale wanapotoa maoni yao na zaidi kwa kuegemea upande mmoja.

Kuna baadhi ya Maaskofu wakitoa maoni kwa kuikosoa Serikali wanashangiliwa na kupongezwa lakini wakati huo huo kuna baadhi ya Maaskofu wakielezea mazuri ya Serikali wanaambulia matusi na kebehi

Abraham Lincoln alipata kusema hivi namnukuu:Hurusiwi kuingilia Uhuru wa mtu pasipo ridhaa yake

TCRA kama wasipokuwa makini na kizazi hiki ambacho hakitaki kufanya kazi lakini kinashinda mitandaoni kwaajili ya lengo moja tu nalo, Matusi tu

Nadhan ni wakati muafaka Tcra kuangalia hili swala kwa upana ili isije kuleta madhara siku za usoni, Tuheshimu Uhuru wa watu pindi wanapotoa maoni yao

Alex Fredrick
 
WaTanzania hatuna uvumilivu wa kisiasa. Mtu analilia demokrasia bila kujua kua demokrasia ni kumuacha mwenzio akupinge unachokiamini.

Mimi nilishangaa nyuzi za kuisema Katoliki zimetamalaki humu kisa somebody Nyaisonga alitoa maoni yake.

Sasa unavyoshindwa kumvumilia Nyaisonga anapokupinga ndiyo na wewe wanavyoshindwa kukuvumilia unapopinga.
 
Tuheshimu Uhuru wa watu pindi wanapotoa maoni yao
Kutukana sio sawa, lakini mtu akitoa maoni yake ama ataungwa mkono, au hayatatugusa tutanyamaza, vinginevyo atapingwa.

Haijalishi awe nani. Sidhani kumjibu mtu kwa hoja ni kuingilia uhuru wake, ikiwa hivyo basi jukwaa litakuwa jukwaa mfu-tunasoma tunasepa.

Kwenye majibizano kuna lugha ya kiungwana, matusi na lugha kali. Matusi yana onyesha tulivyokosa ustarabu bahati mbaya kwa wengine wanafikiri lugha kali ni matusi.
 
Maneno ya wapiga kelele hayana uwezo wa kumdhuru Askofu Pengo wala Malasusa.

Hao ni watu wawili ambao wamekuwa wakiombewa na mamilioni ya wakristo kila mara misa inapoadhimishwa.

Vinyongo vya wanaharakati havina uwezo mahali ambapo ulinzi wa Mungu upo.
 
Two differents this;-
""Hawa ni watumishi wa mungu waliotoharishwa,KAULI ZAO NI LAZIMA ZISIMAME SAWASAWA NA IMAGE YA MUNGU,WAWE WAKWELI KWA YALE WAYAONAYO,NA PIA WAWEZE KUSEMA HAPANA KWA KILE KISICHO SAWA.WAWE NA UTHUBUTU WA KUKEMEA PIA UTHUBUTU WA KUSIFU LILE LOLILO JEMA DHAHIRI.
""

LOI ELOI LAMA SABAKTWANI,SELAHIE!... ona watawa wako kile wakifanyacho, uliumba serekali za kibinadamu ili ziheshimiwe, pamoja na kuwajali watu wake pamoja na kuziheshimu sheria hizo hizo tuliojipangia, basi na JINA LAKO LITUKUZWE;Amen.
73474975_107895397313613_3928430887129055232_o.jpg
 
Wanafiki hao maoni yao huwa ni kutetea matumbo yao sii kwa maslahi ya watanzania. Pengo na Malasusa na Sheikh Alhad Musa ni watu hovyo sana
 
Vijana mbadilike, muipende nchi yenu, ndiyo zawadi pekee ya uhakika aliyowapa Mungu, ikiharibikia mikononi mwenu hakuna mahali pengine mtaweza kupaita nyumbani. Here is our home, our motherland.
 
Wewe Alex Fredrick una uwezo wa kusimama na kubwabwaja chochote unachofikiri ni sahihi kwako, na hiyo ni haki yako. Askofu ni binadamu, lakini si binadamu kama wewe kutokana na dhamana aliyopewa kwa jamii. Anaposimama Askofu kuzungumza jambo, anapaswa (na wewe unapaswa kufahamu) atuweke bayana ikiwa ANAONGEA KAMA INDIVIDUAL au KWA DHAMANA YA NAFASI YAKE.

Ikiwa Maaskofu wale waliyoyasema pale waliyasema KAMA MAASKOFU, basi ule ni unafiki. Kusema kuwa FULANI ANAFAA KUMRITHI FULANI ni kumpigia debe kisiasa huyo fulani. Hapo Askofu anakuwa amesahau majukumu yake na amejiingiza kwenye ushabiki wa KISIASA.

Sidhani kama kweli huelewi ni kwa nini watu wamekasirishwa na jambo hili.
 
Mkuu wengi waliopo kwenye mitandao ya kijamii ni mawakala wa mafisadi, vyeti fake, waliotumbuliwa kwa uzembe kazini, waliokuwa wanafanyabiashara haramu kama madawa ya kulevya sasa utawala huu umewabana hawapumui wako ICU. Halafu wala si wengi kiasi hicho ndiyo maana mipango yao haifanikiwi kwa kila hali. Yaache yaendelee kutoa mapovu na kulala sisi tuendelee kupiga kazi yakija kuamka sisi tunavuna!!
Huna akili je na ww ni kundi gani kati ya hayo ukiyotaja?
 
yako kiongozi halisi wa dini ni ngumu kuwa upande wa watawala tena hawa wa kiafrika?? Kuna mmoja tu Desmond tutu, ndio ameweza kutokuwa mnafiki, lakini hao wengine ni viongozi njaa!! Hayo maovu yote yaliyopo kwenye jamii mbona hata siki moja hawajawahi kuyakemea? Kipindi cha jk mbona walikuwa japo kidogo waliweza kukemea?? Huyo kakobe ni kitu gani kimemfanya akabadirisha gia angani ghafla?
 
Wanafiki hao maoni yao huwa ni kutetea matumbo yao sii kwa maslahi ya watanzania.Pengo na Malasusa na Sheikh Alhad Musa ni watu hovyo sana
Usitusi,umekosea,wasamehe,JICHO LA MUNGU HUONA,NDIMI HUNENA YALIYO MEMA.BASI MUENENENDE MKAYAENEZE YALIYO MEMA KOTE ULIMWENGUNI,YA MUNGU MPENI MUNGU NA YA KAISARI MPENI KAISARI,MSIYATIE MACHO YENU UPOFU WA LAZIMA KWA PUNJE MOJA NDOGO YA KIRIDAU,HATA MKAUSAHAU KUTUMIKIA WALE WALIO WENGI NA WALIO TAYARI KUPOKEA NENO.
 
Siku za hivi karibuni nimeshuhudia jambo moja la hovyo sana kwenye mitandao ya Kijamii Nchini Tumeanza kuingilia Uhuru wa watu pindi pale wanapotoa maoni yao na zaidi kwa kuegemea upande mmoja.

Kuna baadhi ya Maaskofu wakitoa maoni kwa kuikosoa Serikali wanashangiliwa na kupongezwa lakini wakati huo huo kuna baadhi ya Maaskofu wakielezea mazuri ya Serikali wanaambulia matusi na kebehi

Abraham Lincoln alipata kusema hivi namnukuu:Hurusiwi kuingilia Uhuru wa mtu pasipo ridhaa yake

TCRA kama wasipokuwa makini na kizazi hiki ambacho hakitaki kufanya kazi lakini kinashinda mitandaoni kwaajili ya lengo moja tu nalo, Matusi tu

Nadhan ni wakati muafaka Tcra kuangalia hili swala kwa upana ili isije kuleta madhara siku za usoni, Tuheshimu Uhuru wa watu pindi wanapotoa maoni yao

Alex Fredrick

1: Umesema vizuri, hao wanaotoa maoni kupinga unasema wanapingwa, wanatumia pia uhuru wao. Si kila unaloona sawa mwingine aone hivyo.

2: Wakati mwingine hata kama mtu ana maoni mazuri, inategemea anayaletaje kwa watu. Unawezaleta wazo zuri lakini watu wakalikataa kutokana na namna ulivyo lileta.

3: Watu ni wajanja sana hivyo wanapima nia ya ujumbe au wazo linalotolewa, na wakigundua lina walakini ndani yake, basi wana uhuru wa kulipinga

4: Unapowataka TCRA kuingilia kati, pia wewe ni mmoja wapo wa wanaoshinda mitandaoni, ndiyo maana umeleta uzi kama hapa mtandaoni.
 
Back
Top Bottom