samweli wa pili
JF-Expert Member
- Mar 21, 2018
- 400
- 272
Mbona hakukemea wakati wa mauaji ya kibiti. Aidha, sijasikia akikemea wanaotukana na kukejeli viongozi wa nchi kupitia mitandao ya kijamii.Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo
TABIA ya utekaji, utesaji, unyongaji haki, dhuluma na kiburi inayolalamikiwa nchini, imekemewa vikali na Dk. Frederick Shoo, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Anaripoti Mwandishi Wetu, Moshi … (endelea).
Kiongozi huyo wa dini amesema, watu waliompokea Yesu mioyo yao haina kiburi wala majivuno. Amesema, kuna watu wanaotesa wenzao wasiokuwa na hatia jambo ambalo halimfurahishi Mungu.
“Yesu Kristo akatuguse mioyo yetu, tubadilike, tuache kiburi, tuache kuwatesa binadamu wenzetu na tuache kufurahia kuwatesa wenzetu wasio na hatia,” amesema Dk. Shoo.
Licha wateswaji kukumbana na matuio ya kikatili kutoka kwa wenye mamlaka, Dk. Shoo amewatia moyo kwamba, mateso yao hayapotei na kwamba ipo siku mateso ya watesaji yatafika ukomo wake.
“Katika kuteseka kwenu, kwa namna yoyote ile, hata tunapoteswa bila hatia, tujue kwamba Mungu yupo pamoja nasi, hivyo usiogope na usikate tamaa wala kuondoa tumaini lako kwa Mungu, kwani mateso unayokutana nayo kwenye maisha, jua hakika yana mwisho wake,” amesema Dk. Shoo.