Askofu Shoo akemea utekaji na utesaji wa raia, uvunjifu wa haki na kiburi kilichopo kwa viongozi wa nchi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,094
2,000
Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo
TABIA ya utekaji, utesaji, unyongaji haki, dhuluma na kiburi inayolalamikiwa nchini, imekemewa vikali na Dk. Frederick Shoo, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Anaripoti Mwandishi Wetu, Moshi … (endelea).
Akitoa salamu za Krismasi kwenye ibada iliyofanyika katika Kanisa la KKKT, Usharika wa Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro leo tarehe 25 Desemba 2019, Dk. Shoo amewataka watu waliojaa viburi vinavyojengwa na nafasi zao za uongozi, waache ili wawe salama mbele ya Mungu.
Kiongozi huyo wa dini amesema, watu waliompokea Yesu mioyo yao haina kiburi wala majivuno. Amesema, kuna watu wanaotesa wenzao wasiokuwa na hatia jambo ambalo halimfurahishi Mungu.

“Yesu Kristo akatuguse mioyo yetu, tubadilike, tuache kiburi, tuache kuwatesa binadamu wenzetu na tuache kufurahia kuwatesa wenzetu wasio na hatia,” amesema Dk. Shoo.

Licha wateswaji kukumbana na matuio ya kikatili kutoka kwa wenye mamlaka, Dk. Shoo amewatia moyo kwamba, mateso yao hayapotei na kwamba ipo siku mateso ya watesaji yatafika ukomo wake.

“Katika kuteseka kwenu, kwa namna yoyote ile, hata tunapoteswa bila hatia, tujue kwamba Mungu yupo pamoja nasi, hivyo usiogope na usikate tamaa wala kuondoa tumaini lako kwa Mungu, kwani mateso unayokutana nayo kwenye maisha, jua hakika yana mwisho wake,” amesema Dk. Shoo.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
35,655
2,000
Ilitakiwa hiyo speech itolewe na padre ambaye anaongoza ibada kwenye kanisa ambalo jiwe ameenda kusali leo

Hilo haliwezekani, padre yoyote anayeongoza ibada aliyopo jiwe anawekewa mazingira kabisa ya hotuba yake, na hawa viongozi wa aina ya kina Bagonza, Shoo nk hawapewi hiyo nafasi, na wala jiwe hayuko tayari kushiriki kwenye hafla walizopo.
 
Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
13,769

Kwaufupi ni kwamba padre anamuogopa jiwe kuliko anavyomuogopa shetani ambaye anamuhubiri
 
LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
6,317
2,000
Mussa alipo tumwa kwa Herode kuwakomboa wana wa Israel hakuamini kama kuna mtu mwenye mamlaka zaidi yake kwa kipindi kile. Hata Mussa alipofanikiwa kutoka nao bado Herode aliamini maaskari wake wana nguvu ya kuwarudisha. Roho yake ilipigwa upofu. Ndivyo hata Sasa wamekuwa watawala badala ya viongozi. Tunayo yaona yana mwisho.. Hawa wasikii hata wawakilishi wa Mungu ambao ndio Mussa wa leo. Wamejaa viburi..
Ilitakiwa hiyo speech itolewe na padre ambaye anaongoza ibada kwenye kanisa ambalo jiwe ameenda kusali leo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
11,715
2,000
Ilitakiwa hiyo speech itolewe na padre ambaye anaongoza ibada kwenye kanisa ambalo jiwe ameenda kusali leo
Ibada anazohudhuria Jiwe hadi Masomo ya Misa huwa yanaandaliwa kutoka Makumbusho

Sent from my SM-A207F using Tapatalk
 
List 255

JF-Expert Member
Oct 26, 2019
271
1,000
Ujumbe Huu ukamfikie Mh. Mbowe na genge lake.

Waache hiyo michezo ya maigizo
 
Danny Jully

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
4,264
2,000
Mussa alipo tumwa kwa Herode kuwakomboa wana wa Israel hakuamini kama kuna mtu mwenye mamlaka zaidi yake kwa kipindi kile. Hata Mussa alipofanikiwa kutoka nao bado Herode aliamini maaskari wake wana nguvu ya kuwarudisha. Roho yake ilipigwa upofu. Ndivyo hata Sasa wamekuwa watawala badala ya viongozi. Tunayo yaona yana mwisho.. Hawa wasikii hata wawakilishi wa Mungu ambao ndio Mussa wa leo. Wamejaa viburi..

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ni Farao siyo Herode.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
13,769
2,000
Ibada anazohudhuria Jiwe hadi Masomo ya Misa huwa yanaandaliwa kutoka Makumbusho

Sent from my SM-A207F using Tapatalk
Kwaiyo hapo kiujumla ni kua jiwe ndio padre mwenyewe maana anaandaa misa kuliko padre
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom