Askofu Severine Niwemugizi: Kukosekana kwa taarifa na takwimu za kuaminika kuhusu hali ya Korona kuna hasara zaidi kuliko faida

Labda pengine haufahamumtiriiko wa mamlaka ulivyofanya kazi hadi Niwemugizi akafunga kwa muda ibada za Jimboni kwake. Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ndilo lililotoa ruhusa kwa Askofu yeyote kutathmini hali ya ugonjwa jimboni kwake na kuchukua maamuzi ya kufunga au kutofunga ibada. Kwa hiyo kama unatafuta wa kumlaumu kuhusu kufungwa kwa ibada za Jumapili za Jimbo la Rulenge, basi lilaumu Baraza lote la Maaskofu Katoliki (TEC), na sio kumlaumu Askofu Niwemugizi aliyetekeleza maamuzi ya TEC. By the way, kwa sasa kila Jimbo linajua ipi ni pumba na ipi ni mchele
TEC haihusiki alitumia madaraka vibaya kisa tu ohhh Askofu ana mamlaka jimboi kwake kujiamlia chochote!!

Niwemugizi kichwa maji ndio maana alinyimwa kuwa Askofu jimbo kuu la Dar es salaam sababu haivi na wenzie too much know!!!

Angeweza hata kuwa mwenyekiti wa baraza la maaskofu Tanzania au kardinali lakini kaachwa akae na ujuaji wake wanapewa vijana anaachwa na u senior wake wa kijeuri
 
Hawa maaskofu sasa naona bora wawe wanakutana na kutoa tamko moja, hii biashara inayoendelea sasa kila mmoja kusema lake naona itakuwa ngumu kuwatofautisha na wanasiasa, ni kama vile wanaelekea kuwa wanasiasa wa makanisani.
Kuna askofu wa Katoliki kaongea tofauti na huyu jamaa? Lutheran je?
 
Huyo anayezunguka Makanisani kutoa matamko mnamweka kundi gani? Au naye ni Askofu??
Na Askofu kuhubiri kuhusu Corona Ndicho Yesu alichomtuma? Yesu aliwatuma wakahubiri watu kutubu na kuiamini Injili hakuwatuma kuhubiri Corona na takwimu za corona na kuvaa barakoa!!!
 
MTAZAMO WA MHASHAMU BABA ASKOFU SEVERINE NIWEMIGIZI WA KANISA KATOLIKI JIMBO LA RULENGE-NGARA

Nawaza kivyangu kwa sauti. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 katika ibara ya 19 (2) inasema hivi: “Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari la mtu binafsi, na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi”.

Kwa kuwa ni hivyo, kwa maoni yangu:

1)Kiongozi wa dini akisubiri aambiwe na mamlaka ya nchi aendeshe ibada au asiendeshe ibada, kufungua au kufunga kanisa hajui haki na wajibu wake.

2) Katika mazingira ya sasa ya janga la COVID 19 kila kona ya dunia ambapo mikusanyiko ya watu wengi inasemekana kuwa hatari kwa maambukizi ya virusi, mtu kusema mikusanyiko ya makanisani au misikitini siyo hatari kwa maambukizi anaudanganya umma na kuuweka hatarini. Sidhani kama Korona inakuogopa huko.

3) Kiongozi wa dini akifikiri kwamba itakuwa halali tu kwa mamlaka ya nchi kusema mikusanyiko hiyo isitishwe na siyo halali kwa kiongozi wa dini kusitisha kwa muda anaepa wajibu wake.

4) Nyuki wakali wakiingia kwenye nyumba ya ibada, kiongozi wa dini ukawaambia waamini wako ingieni tu kwa ibada hamtaumwa kwa kuwa Mungu yuko humo, utakuwa unawatakia mema waamini? Wakiumwa na hata akafa mtu lawama imwendee nani? Mimi najua hata mshumaa ukiobarikiwa unaungua ukiuwasha!

5) Kuna msemo “don’t copy and paste” (usinakili na kuchapisha), kwa ufupi usiige. Ninamfahamu aliyenakili tamko langu kuhusu mali kwa mapadre wa jimbo na kulichapisha kwenye kitabu chake, tena bila kuomba ruhusa kwangu, nami sijamlaumu. Sijamlaumu kwa sababu siyo kosa kuiga jambo zuri. Wataalamu wanatuambia kuna nadharia ya “the best practices”. Kwamba ukiwa na lako jambo si vibaya kujifunza na kutenda ukifuata njia, miongozo au taratibu nzuri zilizowekwa na mamlaka fulani kadiri ya mazingira. Kutotaka kujifunza kwa wengine ni alama ya kiburi, na unaweza kuangamia kwa kung’ang’ania ujinga wako. Bila shaka mjinga naye huwa anaamini yeye ndiye anajua zaidi ya wote.

6) Naamini taarifa na takwimu sahihi ni muhimu kwa kupanga mipango ya maendeleo ya mtu na taifa. Bila hayo ni vigumu kufanya tathmini na kupanga. Naamini kukosekana kwa taarifa na takwimu za kuaminika kuhusu hali ya Korona kuna hasara zaidi kuliko faida.

7) Viongozi wa dini tutende tulivyojifunza namna ya kufanya kazi zetu badala ya kuambiwa cha kufanya na watu ambao hawajui tulifundishwaje huko chuoni.

Niko tayari kupigwa kwa mawe. Bwana awabariki watakaofanya hivyo, maana alisema: “Naam, saa yaja atakapodhania kila awauaye anamtolea Mungu ibada. Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi” (Yn 16:2).
Chefuuuuuu..l..kwani si ufungue hosp yako uwe unapima crn halafu tukwimu wapelekee waliokutuma kwa faida yenu..
 
Kwahiyo TZ ya Magu ni wachawi, maana tulishakataa lock-down toka mwanzo, akati nchi za wenzetu walifanya lock-down.
Tunaongelea ndani ya nchi wewe mfano ziko nchi hazina katiba wala vyama vingi hatuigi

naongelea ndani ya nchi .Tanzania Maaskofu wako kibao wa kikatoliki na kilutheri lakini waliojitia kufunga ibada wanatoka mkoa wa kagera tu!!! Wegine ibada zikipigwa kama kawaida!!! kuna tatizo.Maaskofu wa Kagera issue ya corporate responsibility wako zero!! They move in Arrogant isolation!!!
 
Afunge tu kanisa lake kama alivyofanya mwanzo kuna maaskofu wawili ambao Mungu hawamjui kabisa wanapatikana mkoa wa Kagera kuna Bagonza wa KKKT na Niwemugizi wa Katoliki hawa ndio pekee waliofunga makanisa yao wakati maaskofu wenzao wote hawakufunga.

Kuna methali inasema anayejitenga na wenzie ni mchawi

Unafungaje kanisa peke yako wakati maaskofu wengine wote kwenye dini yako hawayafungi?.
Si lazima ufuate njia ya wengi,bali fuata njia sahihi hata kama utabaki peke yako.
Nadhani kwa kufanya hivyo walizuia maambukizi makubwa kwa waumini wao,uhai wa binadamu ni wa muhimu kuliko kitu chochote duniani.
Lakini mbona hushangai Tanzania kuwa na approach tofauti na ulimwengu mzima dhidi ya mapambano ya Covid-19 au Tanzania inafuata njia sahihi?.

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
 
Hawa maaskofu sasa naona bora wawe wanakutana na kutoa tamko moja, hii biashara inayoendelea sasa kila mmoja kusema lake naona itakuwa ngumu kuwatofautisha na wanasiasa, ni kama vile wanaelekea kuwa wanasiasa wa makanisani.
Kama ambavyo wanasiasa wanavyopanda kwenye mimbali kutangaza siasa.

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
 
Askofu Shoo alishatoa hilo tamko kwamba tuzingatie kanuni za afya kama tunavyoshauriwa na wataalamu wa afya na siyo wanasiasa wachumia tumbo.
Na neno kubwa ni kuelekezana jinsi ya kukabiliana na majanga kama haya sio KUFOKA FOKA!
 
Labda pengine haufahamumtiriiko wa mamlaka ulivyofanya kazi hadi Niwemugizi akafunga kwa muda ibada za Jimboni kwake. Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ndilo lililotoa ruhusa kwa Askofu yeyote kutathmini hali ya ugonjwa jimboni kwake na kuchukua maamuzi ya kufunga au kutofunga ibada. Kwa hiyo kama unatafuta wa kumlaumu kuhusu kufungwa kwa ibada za Jumapili za Jimbo la Rulenge, basi lilaumu Baraza lote la Maaskofu Katoliki (TEC), na sio kumlaumu Askofu Niwemugizi aliyetekeleza maamuzi ya TEC. By the way, kwa sasa kila Jimbo linajua ipi ni pumba na ipi ni mchele
Ahsante sana kwa ufafanuzi nzuri,wengine wanadandia kanuni nataratibu za kanisa bila kujua undani wake.

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
 
Si lazima ufuate njia ya wengi,bali fuata njia sahihi hata kama utabaki peke yako.
Nadhani kwa kufanya hivyo walizuia maambukizi makubwa kwa waumini wao,uhai wa binadamu ni wa muhimu kuliko kitu chochote duniani.
Lakini mbona hushangai Tanzania kuwa na approach tofauti na ulimwengu mzima dhidi ya mapambano ya Covid-19 au Tanzania inafuata njia sahihi?.

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
unaji contradict mara ohhh fuata njia yako unayoona sahihi kama Niwemugizi mara oh Tanzania ifuate dunia inavyotaka mfano chanjo barakoa nk unasimamia wapi ? msimamo wa hatua za dunia au wa kibinafsi usioiga wengine kama Wa Askofu Niwemugizi asiyeiga Maaskofu katoliki wenzie wengine?
 
Hoja yangu inasimamia kufuata njia sahihi,Niwemugizi alifuata maamuzi ya Baraza la Maasikofu TEC yaliyompa mamlaka kila askofu kutathimini hali halisi ya maambukizi katika jimbo lake,na kuamua accordingly.
Je Tanzania kwa kukaidi na kukejeri maelekezo ya WHO na wataalamu wa Afya tukajielekeza kwenye kupiga nyungu ndiyo kufuata njia sahihi?.

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
 
Hoja yangu inasimamia kufuata njia sahihi,Niwemugizi alifuata maamuzi ya Baraza la Maasikofu TEC yaliyompa mamlaka kila askofu kutathimini hali halisi ya maambukizi katika jimbo lake,na kuamua accordingly.
?.
kwa hiyo kwenye majimbo yote ya Kanisa katoliki Tanzania Tatizo lilionekana kwa Askofu Niwemugizi tu?
 
Askofu NiweMugizi amekwa Rais wa TEC mara mbili hadi mwaka 2006.
ndio maana walimbwaga baada ya kubadilika angeendelea kutulia hadi leo angeendelea na angempokea Kardinali Pengo ukardinali lakini alivyobadilika wakambwaga
 
Usidhani kila mtu ni mbumbumbu kama MATAGA wenzako. Muda wa miaka sita wa NiweMugizi uliisha.

Halafu upumbavu wako unadhani ukardinali unarithiwa.

ndio maana walimbwaga baada ya kubadilika angeendelea kutulia hadi leo angeendelea na angempokea Kardinali Pengo ukardinali lakini alivyobadilika wakambwaga
 
Back
Top Bottom