Askofu: Serikali ya Kikwete imejaa wababaishaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu: Serikali ya Kikwete imejaa wababaishaji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fangfangjt, Mar 7, 2011.

 1. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Askofu wa dayosis ya Pare ya KKKT Charles Mjema, amesema ubabaishaji katika uendeshaji wa nchi unaofanywa na baadhi ya watendaji wakuu serikalini ndio unaoitafuna nchi kwa sasa.

  Wakati Askifu Mjema akitoa kauli hiyo, Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Karanga wa KKKT mjini Moshi, Fred Njama amesema mkakati wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete wa kufikia maisha bora kwa kila mtanzania unatia shaka kuliko matumanini.

  Viongozi hao waandamizi wa KKKT walitoa kauli hizo mjini Moshi mwishoni mwa wiki iliyopita katika mkutano mkuu wa 14 wa usharika wa Karanga, uliopo Soweto ambapo mgeni rasmi alikua asjofu Mjema.

  Kauli za viongozi hao zimekuja kipindi ambacho kuna mjadala mkali nchini kuhusu hali ngumu ya maisha inayotokana na kupanda gharama za mafuta, mgawo wa umeme na ongezeko la bei za bidhaa na huduma mbali mbali.

  Source: Mwananchi
   
 2. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Aisee, mbona alikipigia CCM kura wakati wa uchaguzi? Well, ujumbe umefika.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,457
  Likes Received: 81,708
  Trophy Points: 280
  Kauli hii haina udini bali huo ndiyo ukweli mtupu. Serikali yote imejaa wababaishaji tu ndiyo sababu kubwa ya matatizo mbali mbali ambayo ni sugu na yanashindwa kutatuliwa mwaka nenda mwaka rudi.
   
 4. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  ni kweli ubabaushaji ni mwingi sana...........tena sana
   
 5. U

  Uswe JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  aisee hakuipa ccm kura aisee!
   
 6. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,200
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  Serikali inavyojitetea kwamba kupanda kwa maisha kunachangiwa sana na kupanda kwa bie ya mafuta duniani, mbona haijawahi kutueleza kama imefanya jitihada za kuwapunguzia wananchi wake ugumu wa maisha kwa kuondoa kodi ya foroza kwenye mafuta achilia mbali VAT na kodi nyinginezo nyingi walizoweka kwenye hayo mafut?
  Badala yake wanatupiga changa la macho kwa kuondoa ushuru wa forodha kwenye sukari ambayo kimsingi sukari siyo kisababishi kikuu cha ugumu wa maisha.
  .
   
 7. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  kweli ubabaishaji umezidi yaani kila sekta ni bala bla tu hakuna chochote cha mhimu kabisa.
  2015 naona ni mbali sana sijui wanannchi watafika.
   
 8. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #8
  Mar 7, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wavue majoho sasa waingie kwenye siasa sio kujificha katika joho la dini.

  Kumbe wametokea kule chimboko la Chadema. lakini Prof Maghembe
   
Loading...