Askofu Renatus Nkwande asikitishwa na uongo wa Polisi kuhusu wana CHADEMA waliokamatwa ndani ya Kanisa

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Mpaka sasa hivi tunaendelea kushughulikia sakata la kukamatwa kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA walipokuwa kwenye misa jana Kawekamo, Mwanza. Waliopo mahabusu ni katibu wa kanda ya Victoria, Mwenyekiti wa Ilemela, katibu wa Nyamagana na wanachama wengine jumla yao ni 20.

OCD asubuhi ya leo, alitueleza wanatuhumiwa kwa kufanya vurugu kanisani na kwamba alipigiwa simu na viongozi wa kanisa. Ilibidi tukauone uongozi wa kanisa Katoliki jimbo la Mwanza, tumeonana na msaidizi wa baba Askofu na akatuwezesha kuongea na askofu Mkuu Renatus Nkwande.

Askofu mkuu jimbo katoliki Mwanza, Renatus Nkwande amesikitishwa sana na uongo wa jeshi la polisi na kuthibitisha kwamba hakukuwa na vurugu yoyote kwenye misa hiyo. Na alipokea matoleo ya wanachama hao wa Chadema na kusali pamoja nao. Akawakaribisha wale chakula pamoja nae.

Wakati wanakwenda kunawa polisi wakavamia eneo hilo na kuanza kukamata kila aliyekuwa na sare za Chadema. Awali asubuhi, walikwishakamata wanachama watano akiwemo mama yake mzazi na John Pambalu ambaye naye alikuwa anaigia kanisani hapo kwa ajili ya ibada hiyo.

Baba askofu Renatus Nkwande kamuelekeza msaidizi wake tukaenda naye hadi Kirumba na ameongea na OCD, sasa OCD akageuza kwa si kanisa lilimpigia simu bali ni waumini wawili mmojawapo anaitwa Gerald Joseph na kusema kanisani kuna wana CHADEMA wanaleta vurugu, hivyo wanataka msaada.

Msaidizi wa Askofu Renatus Nkwande, kawasiliana na (OCD) sasa Askofu mkuu jimbo katoliki Mwanza, Nkwande amemtuma katibu wake, Padre Nyanda na tunaendelea kumsubiri hapa Kirumba.

Tumemueleza Baba Askofu masuala kadhaa, lakini pia jinsi ambavyo tunaona inapendeza watu kutendewa

1. Jeshi la polisi liwaachie wote bila masharti yoyote (kwa kuwa hakuna kosa kisheria ambalo wamevunja)

2. Au ikiwezekana, baba Askofu, jimbo katoliki Mwanza, Renatus Nkwande, akawadhamini waumini wake.

Tutaendelea kuwajulisha kila hatua. Ahsante.
 
Kwanini Chadema wamejitoa kuwadhamini watu wao? hata kama wamekamatwa kwa kuonewa kama Mbowe lakini bado jukumu la kwanza lilikuwa ni Chadema wenyewe kuwadhamini watu wao, sio kuelekeza hiyo kazi kwa Kanisa Katoliki, au polisi wawaachie bila masharti, vipi kama wasipoachiwa?
 
Naona Sirro anamdip mjeswit. Hapo taarifa zitakuwa mbali sana aisee wanamwangalia tu. Kawapiga watanzania kimya Sasa kaimgia duniani. Yetu macho.
 
Mimi ni Mkatoliki ila nawaomba sana Kanisa Katoliki nchini Tanzania wasiingizwe katika Mtego huu wa Mzozo wa Kisiasa baina ya CHADEMA na Mamlaka zote zilizo chini ya Serikali ya Chama Tawala cha CCM. Kuna Hatari naanza Kuiona.
Sijawahi kusikia mkristo ameingia kanisani hata na kanzu akaambiwa ameleta fujo. Ila wahudu wa misa wanahakikisha Kuna usalama. Kama kutakuwa na hali ambayo haieleweki wanataratibu zao zinafuatwa wakisaidiana na mkuu wa kanisa akiwa m/kiti, paroko, wasimamizi na waumini. Sio mmoja wa waumini anaita askari na askari wanakuja kukamata tuu. Nini maana ya uongozi wa mahali au taasisi.

Kutumia nguvu kubwa bila akili utaangukia pua.
 
Back
Top Bottom