Askofu RC atishiwa bastola madhabahuni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu RC atishiwa bastola madhabahuni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Geza Ulole, Jan 11, 2011.

 1. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,071
  Likes Received: 4,008
  Trophy Points: 280
  Askofu RC atishiwa bastola madhabahuni Send to a friend Monday, 10 January 2011 21:36 0diggsdigg

  Devotha John
  MWANAMKE ambaye jina lake halikufahamika, amevamia madhabahuni na kuchomoa bastola kisha kutishia kumwua askofu wa Jimbo Kuu la Njombe, Alfred Maluma aliyekuwa akiendesha ibada katika Kanisa la Mtakatifu Joseph jimboni humo.

  Jaribio hilo la mauaji lililozua tafrani kubwa kanisani hapo na hata kuvuruga kwa muda mwenendo wa ibada, lilidhibitiwa na padri mmoja aliyekuwapo madhabahuni hapo ambaye alimrukia mama huyo na kuikamata bastola hilo.

  Habari zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza kuwa tukio hilo la kwanza kutokea katika Kanisa la Mtakatifu Joseph lililoko Jimbo Kuu la Njombe, lilitokea Alhamisi iliyopita wakati wa ibada ya kusimika mashemasi.

  Kwa mujibu wa habari hizo, mwanamke huyo awali alikuwa ameketi kwenye mabenchi kama mumini wa kawaida aliyekuwa akifuatilia ibada hiyo, lakini ghafla alisimama na kufuata askofu huyo na kumnyoshea bastola hiyo.

  "Wakati wa kipindi cha mageuzo, mwanamke huyo alienda altareni na kumnyoshea bastola Askofu huyo akitaka kumuua," mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, alilieleza gazeti hili na kuongeza. Baada ya kutoa bastola hiyo huku askofu akiendelea na mageuzo, padri aliyefamika kwa jina la Ngiri, alimrukia kwa haraka na kumpokonya bastola hiyo."

  Hata hivyo, habari zaidi zilieleza kuwa baada ya kuikagua bastola hilo ilikuwa haina risasi, lakini mwanamke huyo alikutwa na risasi kwenye begi lake la mkononi.

  Mashuhuda wengine walilieleza gazeti hili kuwa bastola hiyo ilifahamika kuwa ya mmoja wa mapadre wa parokia za Jimbo la Njombe (jina la parokia na padre vimehifadhiwa), lakini haikufahamika mwanamke huyo aliipataje. "Ni Mungu tu aliyesaidia kwa kuwa huyo mtuhumiwa alikuwa amedhamiria kuja kuua na akasahau kuweka risasi hivyo inatakiwa polisi litupe ufafanuzi zaidi," alisema shuhuda mwingine wa tukio hilo.

  Jumapili iliyopita, baadhi ya mapadre walielezea tukio hilo kwenye ibada zao na kufafanua kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa mwanamke huyo ana matatizo ya akili.
  Katibu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Njombe, Erasmo Mligo alithibitisha tukio hilo, lakini akaeleza kuwa hawawezi kuzungumza chochote kwa kuwa suala hilo sasa liko mikononi mwa polisi. "Suala hilo sasa liko kwa mkuu wa upelelezi Wilaya ya Njombe hivyo sisi kama kanisa hatuwezi kuzungumza chochote zaidi ya kuthibitisha kuwa tukio limekuwapo," alisema Mligo.

  Kamanda wa Polisi wa Iringa, Everist Mangara aliliambia Mwananchi jana kuwa ana taarifa ya tukio hilo, lakini bado anafuatilia taarifa zake. "Tukio hilo nimelisikia, lakini sijalipata vizuri ila ninaendelea kulifuatia kwa karibu," alisema Mangara Ends
  http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/8263-askofu-rc-atishiwa-bastola-madhabahuni
  Send to a friend

  NB: Mie naanza kutafsiri haya yanayotokea kama ni njia ya kunyamazisha msimamo wa kanisa juu ya Arusha na yanayotokea sasa, maana najiuliza huyo mwanamke amepataje hiyo silaha ilhali ni punguani? Na hata kama ana uhusiano na Padre inakuwaje anaweza kuipata silaha yake mie nathani ni kazi ya UWT wakipitia mafunzo ya Zimbabwe! maana kule Bob alipokuwa amebanwa sana na wanamegeuzi na kanisa kuingilia; tuliona zilitoka picha za utupu za maaskofu huku tukijiuliza walizipataje kama sio through framing skofu kupitia hawara wake kwa kuagizwa na state intelligency ya Zimbabwe?

   
 2. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  duh
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Sasa kama yeye ni mtu wa Mungu kwa nini aogope bastola? kwi kwi kwi.

  Cha msingi tu ndugu wa huyo mtuhumiwa ndio watatoa ushuhuda wa kweli kama huyo mama ana historia ya matatizo ya kiafya au la. Hizo speculations zingine ni kutengeneza mazingira yakutoaminiana. Wacha wenye kuchunguza na wenye ushahidi sahihi wajiotokeze kuclarify hii kadhia.
   
 4. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Kamanda wa Polisi wa Iringa, Everist Mangara aliliambia Mwananchi jana kuwa ana taarifa ya tukio hilo, lakini bado anafuatilia taarifa zake. "Tukio hilo nimelisikia, lakini sijalipata vizuri ila ninaendelea kulifuatia kwa karibu," alisema Mangara Ends


  hapo hata ukweli ukijulikana watakaa kimya...hatutajua source kamwe
   
 5. Mbwiga_Plus

  Mbwiga_Plus Senior Member

  #5
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo umeconclude kuwa hii ni habari ya kisiasa, na si kwa maoni yako tu?
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kiswahili kwenye hiyo makala kimechukiza. Mhariri alikuwa kalala?
   
 7. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,071
  Likes Received: 4,008
  Trophy Points: 280
  naona turn of events zinashaabiana na yanayoendelea ukikaa chini na kutafakari unaweza ona si tukio dogo hilo! aidha lilikuwa kwa ajili ya kuwatisha kanisa (kutishia kwa bastola unloaded) au kwa dhamira ya kuua kabisa ila kwa kudra ya Mwenyezi Mungu haikuwezekana! Napia hata kama Padre ana uhusiano na huyo mwanamke, hawezi kuacha bastola kwake (kwa sie tunaomiliki hii kitu tunajua) ilhali hawa watu (mapadre) hawaishi nje ya mazingira ya kanisa kusema ilikuwa nyumbani! Mi naona Zimbabwe foot marks are all over Tanzania now....
   
 8. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mkuu hili halielekei kuwa ni suala la siasa, nashawishika kuwa huyu mwanamke na Askofu wanafahamiana hawa, na inaelekea Askofu alimtenda vibaya huyo mwanamke.
   
 9. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  MASWALI
  1. Je, hiyo bastola anaimiliki kihalali?
  2. Ana ugomvi gani na Baba Askofu?
  3. Alipojionyesha kuwa si muumini wa kawaida tunamwitaje?
  4. ................
  5. ................
  6. ................
   
 10. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,071
  Likes Received: 4,008
  Trophy Points: 280
  tutajua ukweli soon ila mi naona zimbabwe style in the picture... haswa ukizingatia timeframe!
   
 11. Kibaraka

  Kibaraka JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 245
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muuaji alisahau ku'load risasi ktk hiyo bastola??!!
  Hapana nakataa.
   
 12. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Ongeza pale kwangu kama swali. Tutafika tu!
   
 13. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #13
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Laiti wauaji kwa niaba ya watawala wangejua maana ya madhabahuni!
   
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hivyo vivyo ndivyo alivyopanga muuaji ili Watanzania mauaji yakitokea na basi tuamini hivyo. Naona wewe ndiyo mmoja kati ya wengi ambao tayari wamefanikiwa kukupata kwa mstari wao waliokwishauchora tangu mwanzo.
   
 15. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #15
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,071
  Likes Received: 4,008
  Trophy Points: 280
  umeona enhee...ni kutia jambajamba kwa makanisa kitakachofuata na kelele zao hehehe!
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hii hatari aisee!!
   
 17. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #17
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Uchunguzi wa kiafya unafanyika hospitali,kupita daktari wa magonjwa ya akili!
   
 18. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #18
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,071
  Likes Received: 4,008
  Trophy Points: 280
  jiulize uchunguzi wa Dr anayefanya katika serikali ya nani? nathani jibu unalo, heheh hivi nyie hamjui jinsi serikali ya kidhalimu inavyoweza operate! ni kiasi cha Mganga Mkuu kuambiwa report iwe vp ama sivyo unamwaga unga na ukitekeleza matakwa unapandishwa cheo!
   
 19. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #19
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  dula,waumin wa kuogopa kufa,hyo ilikua enz za m2me muhammad saw
   
 20. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #20
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  its unforgivable. ana akili zote huyo katumwa na mtu im sure of this.ndugu zangu kuchezea madhahabu haisameheki hata kidogo bora angemtishia nje ya ibada.mtaona mwishowe yatakayomkumba.mahala pa kuabudia si pakuchezea.wakristo mnajua wazi dhambi zote zinasameheka isipokuwa kumchezea roho mtakatifu haisameheki kamwe hapa ni sawa na kumtukana roho mt kupitia kwa wachungaji.Matthew 12:31-32
   
Loading...