Askofu Policalp Pengo angekuwa ndie Sheikh Yahya, Julius Nyerere ndie Mzee Kenyatta! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu Policalp Pengo angekuwa ndie Sheikh Yahya, Julius Nyerere ndie Mzee Kenyatta!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NasDaz, May 15, 2009.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  Kuna best wangu mmoja, longtime kidogo!! Huyu best wangu nilikuwa nakaa nae room moja chuoni. Jamaa alikuwa na mpenzi wake, kwahiyo alikuwa na utaratibu kila weekend( mara nyingi ijumaa jioni!), anachomoka anakuja dar kukutana na demu wake na kurudi mji kasaoro bahari siku ya jumapili jioni! Nilishaizoea ratiba yake hii, na jamaa ilikuwa akisharudi hana stori zingine zadi ya zile zilizohusu yeye na demu wake!

  Weekend nyingine ikawadia, mshikaji huyoo akaja zake town! Hii ilikuwa ni jumamosi, na jamaa alitoka Moro asubuhi, huku nikitarajia angerudi siku ya pili yake jioni kabisa kama sio usiku. Hata hivyo, tofauti na kawaida yake, ilipofika jioni ya siku hiyohiyo jamaa akarejea chuoni! Hakuongea wala kumsalimia mtu, badala yake moja kwa moja akapanda kitandani kwake na kujifunika shuka gubigubi!! Hakuongea na mtu hadi siku ya pili yake asubuhi! Nilipomuuliza amekutwa na masahibu gani; akanajibu amekorofishana na mpenzi wake! Namnukuu: “Yule demu kanikera kishenzi, nimemwambia kama anataka kufunga ndoa na mimi basi abadili dini lakini kakataa!” Mwisho wa nukuu!!

  Sio siri, jamaa aliupiga shoti mwili wangu hadi nikahisi nataka kuyeyuka!! Kwavile watu tunafahamiana dini zetu kutokana na majina yetu, nilishangaa sana jamaa aliponiambia kwamba anamtaka demu wake abadili dini! Jamaa anaitwa George na demu wake ni Grace!! Mimi nilishangaa sana kwavile nilichojuwa ni kwamba wote ni Wakristo!! Na pale nilipomuuliza abadili dini gani wakati wote ni wakristo jamaa akanijibu kwamba demu wake ni Lutheran wakati yeye ni RC!! Hapo nikajiuliza, jamaa anaona demu wake si mwenzake kwavile tu yeye ni RC na demu wake ni Lutheran; je mimi kama mshikaji wake ananichukuliaje ambapo mimi ni muislamu na yeye ni mkristo!!

  Hapa ninapoongea, hawapo pamoja ingawaje sina hakika ni u-RC na u-Lutheri ndio uliowatenganisha ingawaje hata kama sio basi naamini umechangia!!

  Anyway, hoja yangu ya msingi si suala la udini kwenye ndoa, bali mtu kujiona bora kwavile tu yeye ana asili fulani!!

  “Utaoaje Mmakonde bwana?!” Usishangae mtu mzima na akili zake akiuliza swali la kipuuzi kama hilo!! Nachojiuliza ni kwamba, inakuwaje mtu anajiona bora kuliko mwenzake kwavile tu yeye ni Mchaga au Mhaya wakati hajalipa hata senti moja kama ujira wa yeye kuwa Mchaga au Mhaya!!!! Inakuwaje mtu anajiona bora kuliko mwenzake kwavile tu yeye ni mwanaume na mwenzake ni mwanamke wakati hajawekeza hata chembe ya struggle ili yeye awe mwanaume na badala yake amejikuta tu akiwa na hiyo jinsia!!

  Inawezekana kabisa mtu huyo akajiona yeye ni bora kwavile tu yeye ni Mchaga kutokana na mafanikio waliyonayo Wachaga!! Hata hivyo, unaweza kukuta Mchaga huyu anaejiona kazi yake ni Shoe Shiner!!! Unaweza kukuta mtu anajiona bora kuliko mwenzake kwavile tu yeye ni Mhaya na mwenzake ni Msukuma! Anajiona bora kwavile anaamini Wahaya ni watu waliopiga Book ile mbaya wakati mwenyewe kaishia Form TWO!!! Hivi utazichukuliaje akili za watu kama hawa?! Hivi utaithaminisha vipi akili ya mtu anayemdharau mwenzake kwavile tu mwenzake huyo ni Mgogo, Mmakonde au Mzaramo wakati anafahamu fika kwamba hajalipa japo punje ya mchanga ili yeye asiwe ni wa chimbuko la makabila hayo anayoyaoona si bora!!

  Rafiki yangu George alikuwa hafahamu kwamba yeye ni Mkristo kwavile tu ni mwenyeji wa Iringa, na bila shaka si ajabu angekuwa ni Abdulrahman endapo mungu angeamua chimbuko lake liwe Pangani!! Hafahamu kwamba si ajabu huyu Askofu Pengo tuliyenaye sasa angekuwa ndie Sheikh Yahya Hussein endapo Mungu angeamua huyu Polycarp awe ni mwenye chimbuko la Zanzibar! Si ajabu Wanyakyusa hivi sasa wangekuwa ndo akina Sunni, Shiha, Shafii (Madhehebu ya Kiislamu) endapo hali ya hewa ya Mbeya ingekuwa inalandana na ile ya Arabuni kiasi cha kuwafanya Wakoloni wa Kiarabu kuamishia makazi yao Mbeya badala ya ukanda wa pwani!! Si ajabu waislamu wa leo wangekuwa ndiwo wakristo endapo wazungu wangeamua kupiga kambi zao ukanda wa pwani badala ya bara!! Sasa ya nini mtu kujiona bora kutokana na dini au kabila lake?!

  Mentality hii ni mbaya kwavile inafifisha ustawi wa jamii, kuanzia at individual, national to regioanl level! Hata mimi siwezi kushirikiana na mtu anayejiona bora kuliko mwenzie. Leo hii wapo Watanzania wasiopenda ushirikiano wa Afrika Mashariki kutokana tu na tabia ya baadhi ya Wakenya ya wao kujiona bora kuliko wenzao wa TZ au UG, wakati ubora wanaojivunia wala hautokani na mafanikio yao binafsi!! Mkenya huyu atamdharau mwenzake Mtanzania sio kwavile yeye (Mkenya) ana kitu chake binafsi cha kujivunia kuliko huyu mwenzake, bali ni kwavile tu yeye ni Mkenya wakati Ukenya wake ni gift from Nature!!Waswahili wengi hawapendi kushirikiana na ndugu zetu Wa-Tz wenye asili ya asia, hususani bara hindi kwavile tu ndugu zetu hawa wana tabia kujiona bora kuliko wenzao weusi! Usishangae kukuta Mhindi akimdharau mweusi wakati yeye kazi yake ni kuuza duka la Mhind mwenzake pale Kitumbini!!

  Hii ni changamoto kwa wale wote wanaozani wao ni bora kuliko wenzao kwa tafsiri yoyote ile. Jamii yenye watu ambao baadhi wanajiona bora kuliko wenzao ni jamii inayotishia ustawi wake wenyewe!! Kusingekuwa na ubaguzi wa rangi SA endapo Makaburu wasingejiona wao ni bora kuliko weusi!
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  you are right.
  Mbora ni yule anaemuogapa Mungu na kuishi vizuri na wenzake.
   
 3. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mkuu unge-summarise hiyo hadithi inaboa kimtindo...!
   
 4. s

  smartJOE Member

  #4
  May 15, 2009
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ruth went to her mail box and there was only one letter.
  She picked it up and looked at it before opening, but then she looked at the envelope again.  There was no stamp, no postmark, only her name and address.

  She read the letter:

  Dear Ruth:

  I`m going to be in your neighborhood Saturday afternoon and I'd like to stop by for a visit.

  Love Always,


  Jesus

  Her hands were shaking as she placed the letter on the table. 'Why would the Lord want to visit me?
  I'm nobody special. I don't have anything to offer.'


  With that thought, Ruth remembered her empty kitchen cabinets.

  'Oh my goodness, I really don't have anything to offer.. I'll have to run down to the store and buy something for dinner.'  She reached for her purse and counted out its contents.. Five dollars and forty cents.


  Well, I can get some bread and cold cuts, at least.'


  She threw on her coat and hurried out the door.

  A loaf of French bread, a half-pound of sliced turkey, and a carton of milk...leaving Ruth with grand total twelve cents to last her unt il Monday..


  Nonetheless, she felt good as she headed home, her meager offerings tucked under her arm.


  'Hey lady, can you help us,lady?'


  Ruth had been so absorbed in her dinner plans, she hadn't even noticed two figures huddled in the alleyway.  A man and a woman, both of them dressed in little more than rags.


  'Look lady, I ain't got a job, you know, and my wife and I have been living out here on the street, and, well, now it's getting cold and we're getting kinda
  hungry and, well, if you could help us... Lady, we'd really appreciate it.'


  Ruth looked at them both.

  They were dirty, they smelled bad and frankly, she was certain that they could get some kind of work if they really wanted to.


  'Sir, I'd like to help you, but I'm a poor woman myself.. All I have is a few cold cuts and some bread, and I'm having an important guest for dinner tonight and I was planning on serving that to Him..'


  'Yeah, well, okay lady, I understand. Thanks anyway.'


  The man put his arm around the woman's

  shoulders, turned and headed back into the alley.  As she watched them leave, Ruth felt a familiar twinge in her heart.  'Sir, wait!'

  The couple stopped and turned as she ran down the alley after them.

  'Look, why don't you take this food. I'll figure out something else to serve my guest.'

  She handed the man her grocery bag..  'Thank you lady. Thank you very much!'  'Yes, thank you!' It was the man's wife, and Ruth could see now that she was shivering


  'You know, I've got another coat at home.  Here, why don't you take this one.'  Ruth unbuttoned her jacket and slipped it over the wom an's shoulders.  Then smiling, she turned and walked back to the street....without her coat and with nothing to serve her guest.  'Thank you lady!


  Thank you very much!'


  Ruth was chilled by the time she reached her front
  door, and worried too.  The Lord  was coming to visit and she didn't have anything to offer Him.  She fumbled through her purse for the door key. But as she did, she noticed another envelope in her mailbox.  'That's odd. The mailman doesn't usually come twice in one day.'


  Dear Ruth:


  It was so good to see you again.


  Thank you for the lovely meal.  And thank you, too, for the beautiful coat.  Love Always,
  Jesus
  The air was sti ll cold, but even without her coat, Ruth no longer noticed
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  May 15, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  JF imeingiliwa..lol
   
 6. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #6
  May 15, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Pengo vs Yahya and Nyerere vs Kenyatta .......Vinaunganishwaji na story hii wandugu?
   
 7. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #7
  May 15, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  wewe jamaa mvivu sana....na ndio maana RA atazidi kukuibieni.....

  mkuu hapo hatuna la kukusaidia....unataka utafuniwe umezewe?

  usianze kutuwekea vifungu vyako........
   
Loading...