Askofu Pengo: Sikufahamu kuhusu waraka wa Kwaresma wa Baraza la Maaskofu Katoliki. Awaasa wasichanganye dini na siasa

Hapa kuna vitu viwili vilivyo wazi lakini mitanzania mingi haitaki kutumia hata akili kidogo tulizopewa na Mungu kufikiri.
Kuna Maaskofu na kuna waraka (ujumbe), je waliyoainisha kwenye huo waraka yapo au hayapo!? Uwepo wake au kutokuwepo hauwezi kutugusa kwa viwango sawa na ndio maana kila mmoja wetu anatakiwa kuutafakari kivyake na kutoa maoni. Bati mbaya kutoa maoni kwa sasa inatakiwa ukubaliane na upande mmoja na ukipinga, unalo!
 
Wakati wa utawala wa Mh Kikwete, huyu askofu aliiambia serikali ya Kikwete wasiwapangie makanisa kitu cha kuongea.
Na kwamba viongozi wa Dini wanatakiwa kuongea kila wanalo ona ni sawa kuliongea.
Wakati huo hakuwa anaongea siasa?? Leo kaingia rafiki yake anasema siasa zina mahali pake....
:):) kwa hiyo hana msimamo na hana maadili ya kidini
 
SIRI IMEFICHUKA!!!!!!
• Maaskofu waukana Ujumbe wa Pasaka.
• Maaskofu 4 wa TEC waliouandika wajulikana
Majina yao haya hapa, kwa taarifa za uhakika.
Nimeshtushwa sana na taarifa niliyoipata juu ya Ujumbe wa Kwaresima uliotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ulioelekezwa kwa waumini wakati huu wa toba ya Kwaresima iliyoanza Februari 14, 2018 hadi Pasaka siku ya kusherehekea ufufuko wa Bwana Yesu Kristo (Pasaka).

Mimi ni Mkatoliki wa Jimbo la Dodoma na Askofu wangu ni Mhashamu Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya.
Nikiri nilianza kupata mashaka tangu mapema ujumbe huu ulipotoka, nilijiuliza sana na hivyo nikaamua kufanya juhudi za kujua kama kweli Kanisa langu Katoliki limefikia hatua hii? Naujua utaratibu na utamaduni wa kanisa langu ndio maana nilipatwa na mashaka haya.

Kwa ambao hawajausoma ujumbe huu, ulikuwa na sura nne lakini iliyoleta tafrani ni sura ya tatu yenye ujumbe kuhusu “Dalili za nyakati zetu Tanzania” hususani katika kipengele cha siasa. Imeleta tafrani kwa sababu katika eneo hili ujumbe huu umeenda kwenye masuala ambayo siku zote yamesababisha kuwepo malumbano kuwa viongozi wa dini wanaingia mambo ya kisiasa ama wanachanganya dini na siasa.

Kwa ufupi kabisa ujumbe huu umetoa shutuma na bila shaka dhidi ya Serikali inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli kuwa shughuli za siasa kama vile uenezi, mikutano ya hadhara, maandamano, makongamano, mijadala na mikutano ya ndani zinazuiwa kwa kutumia vyombo vya dola.

Ujumbe unaendelea kushutumu kuwa vyombo vya habari vimefungiwa au kusimamishwa kwa muda, uhuru wa Mahakama na Bunge unaminywa na kwamba katika mazingira haya ni rahisi kwa jamii kufarakana na hata kujenga chuki kiasi cha kuhatarisha amani, usalama na hadhi ya uhai wa binadamu.

Ujumbe umeongeza shutuma nyingine kuwa chaguzi zinaharibiwa kwa vurugu na hivyo kuacha nyuma uchungu, hasira, tamaa ya kulipa kisasi na hata kususia chaguzi nyingine na kwamba hali hiyo ni hatari kwa mustakabali wa Taifa letu, ikiachwa izoeleke tusishangae huko mbele kujikuta katika mifarakano mikubwa zaidi itakayobomoa misingi ya amani na umoja wa kitaifa.
NIMEPATA TAARIFA ZA UHAKIKA KABISA kuwa ujumbe huu haukuandikwa na Maaskofu 35 wa Kanisa Katoliki kama ilivyotolewa na Baraza la Maaskofu (TEC).

Katika shauku yangu hii ya kutaka kujua kwa nini viongozi wangu wa Kanisa lenye heshima hapa nchini wamefikia hatua hii nimepata taarifa za uhakika kuwa Maaskofu walioshiriki kuandika ujumbe huu ni wanne (nitawataja huko mbele) na Maaskofu wengine walikataa kushiriki kikao kilichofanya kazi ya kuandika ujumbe huu.

Mniwie radhi sana nimepata mashaka makubwa sana niliposoma majina ya Maaskofu waliofanya kazi ya kuandika ujumbe huu na historia zao za mahubiri yenye uchochezi mkubwa na hata mara kadhaa wametuhumiwa kwa ukabila na uchochezi na ushahidi upo.
Maaskofu walioandika ujumbe huu ni Mhashamu Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya wa Jimbo Kuu la Dodoma, Mhashamu Askofu Mkuu Yuda Thaddaeus Ruwa’ichi wa Jimbo Kuu la Mwanza, Mhashamu Askofu Augustino Shao wa Jimbo la Zanzibar na Mhashamu Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo la Rulenge-Ngara.

Maaskofu wengine hawakushiriki kuandika ujumbe huu na kwa kuwa wanatambua dosari iliyokuwa inafanyika wakatoa udhuru mbalimbali na kwa hivyo hao Maaskofu wanne wakaifanya kazi hiyo wakishirikiana na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Padre Raymond Saba na wakamchukua Dk. Kasala kama mshauri wa uandishi wa ujumbe huo.

Kwa kuangalia safu hiyo utaona ujumbe huu umeandikwa pasi kuwepo Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Mhashamu Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa wala Mwadhama Polyacarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
Nimepata taarifa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea Mhashamu Damian Dallu aliondoka mkutanoni na kuomba udhuru baada ya kubaini mwelekeo wa ujumbe huu.

Hapo ni kujiuliza kwa nini? Na kama kuna yeyote hayaamini haya basi na awaulize viongozi hawa kama walishiriki kuandika ujumbe huo, naamini hata wao wamekwazika na kwa namna yeyote hawawezi kukubaliana na yaliyomo katika ujumbe huu hata kama watakuwa na changamoto ya kuukana hadharani kulingana na utamaduni na nidhamu ya Kanisa.

Ukiangalia Maaskofu watatu kati ya wanne walioandika ujumbe huu wanatoka Mikoa ya ama Arusha ama Kilimanjaro ambako wanasiasa wake ndio wamekuwa wakishikia bango hizo hoja walizoziandika na wao wamekuwa mara kadhaa wakipambana kutumia Ibada na shughuli za Kanisa kueneza siasa hizo.

Askofu Niwemugizi ambaye mpaka sasa ana mgogoro mkubwa na idara ya Uhamiaji kutokana na uraia wake kuwa na mashaka na yeye amekuwa akitaka kujificha kwenye kichaka cha kudai anafuatwafuatwa kwa sababu anawakosoa watawala, anafahamika kwa namna alivyojipambanua kuegemea siasa za upinzani na kuungana na wanaharakati wanaopambana na Serikali.

LAKINI kwa kungalia hizo hoja wanazozitoa kuikosoa Serikali na kutaka kujenga taharuki kwa Watanzania kuwa nchi inakwenda vibaya, mimi nimejiuliza mambo mengi sana.

Maaskofu hawa wanne wanadai shughuli za kiasiasa zimezuiliwa, hivi ni mwanasiasa gani amezuliwa kufanya siasa? Maaskofu hawa wanawasikiliza akina Freeman Mbowe, Godbless Lema, Zitto Kabwe, Tundu Lissu na genge lao linalojumuisha Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu kinachoongozwa na mwanachama wa CHADEMA Dk. Heleni Kijo-Bisimba ambao wanataka shughuli za siasa iwe ni kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya maandamano, fujo na uchochezi?

Wakawaulize wanasiasa hao ni lini wamekatazwa kufanya shughuli za siasa kwenye majimbo yao? Au kwa wao wanafurahishwa na kauli za Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kuwa Watanzania wawe tayari kufa 100 hadi 200 kwa ajili ya yeye kwenda Ikulu? Hawataki hata kumuuliza Freeman Mbowe kwa nini kaatamia uenyekiti wa CHADEMA kwa zaidi ya miaka 20?

Maaskofu hawa wanne wanashutumu kuwa vyombo vya habari vimefungiwa na vingine vimefungiwa kwa muda na hivyo kupunguza uwigo wa wananchi kupata habari, maoni na uhuru wa kujieleza. Hivi Maaskofu hawajui kuwa uhuru huu una mipaka na ni kwa mujibu wa sheria? Maaskofu hawajui vyombo vya habari vilivyofungiwa ni kwa sababu vimevunja sheria? Nimejiuliza sana hivi hata ndani ya Kanisa Katoliki hakuna mipanga ya uhuru wa kujieleza?

Labda niwaulize Maaskofu kama mnahoji hilo, Je Kanisa Katoliki lenyewe limejihoji juu ya hatua lilizomchukua Padre Felician Nkwera? Kwa ambao hawajui Padre huyu alikuwa hodari wa mahubiri na alipendwa sana na waumini akawa tishio ndani ya vigogo wa Kanisa Katoliki, matokeo yake alipigwa fitina hadi Makao Makuu Roma Italia na mwishowe alitengwa na Kanisa.

Padre Privatus Kalugendo vivyo hivyo aliweka msimamo wake na akaamua kuoa ambayo ni haki ya mwanadamu yeyote, matokeo yake alitengwa na akafukuzwa kwa tamko la Papa, ambalo huwa halipingwi. Padre Titus Mageranga wa Iringa yalimkuta hayo hayo, na hata Askofu Jacob Koda wa Jimbo la Same Kilimanjaro naye yalimkuta hayo hayo.

Mifano ipo mingi, hivi kuna mtu anajiuliza Askofu Mkuu Norbet Wendelin Mtega yupo wapi? Askofu Mahiri kabisa aliyeliongoza Jimbo Kuu Katoliki la Mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba kule Songea, Ruvuma. Alipigwa fitna akaondolewa kimyakimya mpaka leo haijulikani yupo wapi na Kanisa Katoliki halijatoka kwa waumini kuwaambia alikosa nini na yupo wapi?

Na hili halipo Tanzania tu, huo ndio utamaduni wa Kanisa hili kwamba katika ngazi hizo za vigogo wakubwa, ukienda tofauti na matakwa yao bila kujali una haki au huna haki unafukuzwa, unafichwa Roma ama unawekwa popote duniani ama unapotezwa kabisa maana inakuwa hakuna mawasiliano na nyumbani wala ndugu zako. Wakatoliki wanaujua ukweli huu. Nausema kwa sababu walioanzisha kufukunyua mambo ya kuvuruga nchi ni vizuri wajue kuwa hata wao sio wasafi hivyo na sisi waumini tunajua mengi ila tunaheshimu tu.

Maaskofu hawa wanne wanasema vyombo vya habari vinafungiwa, nimewaza sana na nikakumbuka jinsi viongozi hawa hawa wa Kanisa Katoliki kule nchini Rwanda walipotumia kituo cha redio kueneza chuki miongoni mwa Wanyarwanda na kusababisha mauaji ya halaiki mwaka 1994, ambapo watu takribani Milioni 1 waliuawa kikatili kwa kuchinjwa, kuchomwa moto na kupondwapondwa kwa madai kuwa ni mende.

Kwa wasiojua mauaji ya halaiki ya Rwanda yaliibukia kwenye ukabila lakini fukuto lilianza zamani na miongoni mwa waliokuwa wanatengeneza fukuto hilo ni viongozi wa Kanisa Katoliki ambalo lina mizizi mikubwa nchini Rwanda.
Askofu Rwemugizi ambaye ana mgogoro na idara ya Uhamiaji kwa madai kuwa sio raia wa Tanzania bali nchi jirani anaujua ukweli huu na anajua vizuri madhara ya mchezo anaoufanya, naamini ama anashauku ya kuona tena mauaji yale ama anafanya kwa malengo mahususi.

Maaskofu hawa wanne wanasema Mahakama na Bunge vinaingiliwa, lakini hawajasema ni wapi mihimili hii imeingiliwa.
Kwa ujumbe unaotoka kwa jina la chombo kikubwa kama Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) nilitegemea kusoma mifano na uthibitisho wa kuingiliwa kwa mihimili hii.

Hii ni hatari kubwa sana kutoa tuhuma nzito kama hizo dhidi ya mihimili ya dola halafu ukaacha zinaelea hewani. Watoke tena Maaskofu hawa wanne waseme kwa uwazi na kwa uthibitisho kuwa mihimili hii imeingiliwa hapa na hapa na hapa.
Maaskofu hawa wanne wanasema chaguzi zinafanywa kwa vurugu na zinaacha chuki kiasi cha kuhatarisha amani, usalama na hadhi ya uhai wa binadamu. Japo kuwa kauli hii imeachwa inaelea lakini kwa namna yoyote Maaskofu wanatuhumu kuwa wanaoshindwa kwenye chaguzi nyingi hapa nchini ambao ni vyama vya upinzani ndio wanaobaki na hasira na chuki.

Hapa Maaskofu wanataka kutuambia kuwa ni Tanzania peke yake ambako wanaoshindwa kwenye uchaguzi ndio wananuna? Hivi kwenye chaguzi za ndani ya CHADEMA wanaokosa huwa hawanuni? Ina maana Maaskofu huwa hawaoni vurugu ambazo hutokea kwenye mataifa mbalimbali wakiwemo jirani zetu wa Kenya hata Taifa kubwa la Marekani ambao wamefanya uchaguzi karibuni? Mimi nilidhani jukumu la maaskofu lingekuwa kuponya kwa imani makovu ya uchaguzi hasa kwa wanaoshindwa na badala yake wanataka hapa Tanzania ndio paonekane pana tatizo kubwa na wanatuma ujumbe wa kuwachochea wananchi waikasirikie Serikali.

HITIMISHO.

Kwa sisi Wakatoliki hiki kilichofanywa na Maaskofu hawa wanne ni lazima kikemewe kwa nguvu zote. Naamini Kanisa linao Maaskofu wazuri, wacha Mungu na wanaotambua umuhimu wa Kanisa katika nchi, wanatambua umuhimu wao katika kuimarisha ustawi wa jamii badala ya kuivuruga.

Na hata katika mahubiri ya leo Jumapili ya Matawi (Machi 25, 2018) tumewasikia Maaskofu na Mapadre wazuri wakihubiri Injili juu ya Mateso ya Yesu na kusulubiwa kwake kwa ajili ya wanadamu. Wanafanya kazi ya Mungu ya kuwajenga waumini kwa imani, kutubu dhambi na kushika njia iliyonyooka, wametufundisha mambo muhimu katika maisha ya ukristo na kamwe viongozi hawa hawawi na mahubiri ya mihemko na siasa zinazoleta chuki na uchochezi.

Tunajenga Taifa la wachapakazi, nchi yetu ipo nyuma sana kimaendeleo, Maaskofu na Mapadre wetu wazuri wanahubiri matumaini, wanawaombea viongozi wa Serikali kuwa watumishi bora, wenye hofu ya Mungu, wanaviombea vyombo vya haki kutenda haki na wanawaombea Watanzania na dunia nzima kupigania amani, upendo, mshikamano na udugu badala ya kushabikia kauli na uchochezi wa kuleta vita, mapigano, malumbano na fitna.

Maaskofu na Mapadre Wakatoliki wazuri wanawahimiza Watanzania kufanya kazi mashambani na makazini ili kujipatia kipato halali kwa kuwa imeandikwa asiyefanya kazi na asile, wanawahimiza Watanzania kutovunja sheria na kuheshimu mamlaka zote badala ya kuchochea watu wakeshe kwenye maandano, malumbano na mapambano na Serikali.

Naamini mtazamo huu sio wa kwangu pekee yangu, naamini wapo Wakatoliki wengi ambao wamechukizwa na sehemu ya ujumbe huu wa Kwaresima ulioandikwa na Maaskofu hawa wanne, nawaomba tusiyumbishwe na hilo, tuendelee kuipenda nchi yetu na kuungana na Serikali hasa wakati huu ambapo kiongozi wa nchi Mhe. Rais Magufuli anafanya mambo makubwa ya kimageuzi katika uchumi, ustawi wa jamii, kutetea wanyonge na kudhibiti wizi wa mali za umma.

Natambua kuwa Baraza la Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) nao wamefanya makosa haya haya yaliyofanywa na TEC, natambua vinara wa kutoa Ujumbe wa Pasaka wa KKKT ni watu wa mlengo gani, natambua kwa nini wamekasirishwa hivyo lakini hili wacha niwaachie waumini wa KKKT wenyewe, mimi nipo na hawa wa kwangu Kanisa Katoliki.

Kwa Maaskofu wote na viongozi wengine wa dini, naomba niseme Tanzania ninayoijua mimi ina watu ambao wapo makini sana hasa linapokuja suala la nchi yao, sisi Watanzania tunapenda amani, tunapenda upendo, sisi ni ndugu sana, hatujazoea vurugu, hatupendi ukabila na ukanda, tunawapenda majirani kama Yesu alivyosema na ndio maana hao wanasiasa walioasisi haya mnayoyasema leo wameshindwa kwenye uwanja wa siasa na sasa wanataka kuwatumia nyie kwenye makanisa.

Ninachokiona kwa kuwa mmesahau kuwa Makanisani kwenu kuna waumini wenye milengo tofauti ya siasa tunakokwenda mtayavuruga Makanisa, kwa Kanisa Katoliki itakuwa ni mtihani mkubwa kwa sababu hakuna utaratibu wa Askofu kupigiwa kura ili aendelee ama asiendelee kama ilivyo kwa Makanisa mengine, kwa hiyo kitakachotokea ni kuendelea kukimbiwa na waumini kama ambavyo mmewapoteza waumini wengi kwenda kwenye makanisa ya Kilokole.

Kwa makanisa yenye uchaguzi wa Maaskofu ninachokiona ni kuendeleza mitafaruku ambayo mpaka leo inazitafuna baadhi ya Dayosisi zenu. Tena huku mlikoingia ndio kubaya zaidi maana sasa vyama vya siasa vitaanza kushindana kuweka Maaskofu wao. Inawezekana msilione hili lakini mkae mkijua kuwa litakapofika hapo hamtaweza kulidhibiti.

CHADEMA walipoanzisha kumchukua Mwana CCM Lazaro Nyalandu walidhani CCM watakaa kimya, walichokipata na wanachoendelea kukipata wote mnaona. Sasa na nyinyi mmeamua kuingia kwenye siasa za kushabikia hoja za CHADEMA na kutumwa na CHADEMA kuichokonoa Serikali ya CCM, mjiangalie siku CCM nao wakiingia huko Makanisani kwenu mjue shughuli itakuwa pevu.

Nawaombeni msituharibie Kanisa. Acheni Makanisa yafanye kazi yake ya kuhubiri Injili, siasa waachieni wanasiasa, harakati waachieni wanaharakati na vita waachieni wanajeshi.

Julius Kindonga
Mkazi wa Dodoma Machi 25, 2018
Asante kwa taarifa.Lakini kaa mbali na watumishi wa Mungu.
 
Kandonga usitumike, umeandika kama wewe unaona taratibu za kabisa katoliki, kila Askofu ana mamlaka katika jimbo lake, na unajua fika kwamba kila kipindi cha kwarezima baraza la maaskofu lazima watoe ujumbe na lazima usomwe kwa waumini. Mimi nipo katika Jimbo ambalo Askofu wake si mmoja wa wale 4 uliowatuhumu kuandika ujumbe huu. Maana yangu nikuwa Kata wasingekuwa wanauunga mkono basi usingesomwa majimbo yote. Wewe kinachokuchanganya ni kuwa uende kuna timu iliyopewa kazi ya kuandika yaliyoongelewa kwenye baraza. Uelewe kuwa siyo rahisi maaskofu wote wakashika kalamu kuandika.
Pia katika maelezo yako umeonyesha kuwa wewe ni shabaki wa CCM na serikali yake na ulivyo na chuki na CDM
 
Tanzania ya sasa inatia huruma kinga ni bora kuliko tiba huwezi kutafuta mchawi wakat mchawi upo nae ndani kwako ccm ni chama kilichojifia muda tu kukaa madarakani ni nguvu ya dora mtahangaika na kila mtu shida chama kimechokwa hata aje nani ccm bado ni chama cha hovyo huwez kumpiga mtu risasi zaidi ya 38 ukategemea Mungu atakuwa upande wako ccm inapitia viasharia vya vurugu za nchi zijazo kabla ya matukio makubwa kutokea huwa alama kama hizi za maonyo hutolewa werevu tunajua nini kinafuata.
Kumbe wewe unamjua aliyefanya kitendo hicho?
Na kama unauhakika, mtaje/mripoti kwa njia unayoona inafaa (kwa vithibitisho) ili vyombo husika vifanye kazi yake. Haijalishi anatoka chama gani, au dini au kabila gani!
 
Kandonga usitumike, umeandika kama wewe unaona taratibu za kabisa katoliki, kila Askofu ana mamlaka katika jimbo lake, na unajua fika kwamba kila kipindi cha kwarezima baraza la maaskofu lazima watoe ujumbe na lazima usomwe kwa waumini. Mimi nipo katika Jimbo ambalo Askofu wake si mmoja wa wale 4 uliowatuhumu kuandika ujumbe huu. Maana yangu nikuwa Kata wasingekuwa wanauunga mkono basi usingesomwa majimbo yote. Wewe kinachokuchanganya ni kuwa uende kuna timu iliyopewa kazi ya kuandika yaliyoongelewa kwenye baraza. Uelewe kuwa siyo rahisi maaskofu wote wakashika kalamu kuandika.
Pia katika maelezo yako umeonyesha kuwa wewe ni shabaki wa CCM na serikali yake na ulivyo na chuki na CDM
Mbona Pengo aliukana?
 
Nimejaribu kutenga muda kusoma thread hii...kumbe mwandishi anakerwa anapoona au kusikia mtu au taasisi fulani inaikosoa serikali.
Hapa kuna shida kidogo, watu tunasahau maslahi ya nchi kwa kuitetea serikali hata kwa mabaya yanayoendelea kutoa!!

Naona kundi la watu wakijifunika blanketi usoni mchana kweupe na kujifanya hawaoni mateso, vurugu, risasi, kutekwa, kuuawa, kuokotwa miili ufukweni, hali mbay ya uchumi, mfumuko wa bei n.k....wao hayo japo yanawagusa, lakin kwa mapenz yao kwa serikali (na sio nchi) wanaona kama ngoma za jadi zinazoburudisha

Mungu Shusha Nabii Mwingine Atuokoe
 
Hivi mnamjibu ili iweje? yeye mwenyewe haelewi kama huyo alieandika asivyojielewa
 
Namwomba Mungu Mkuu atusaidie watanzania, atufumbue macho yetu ya rohoni ili tuweze kujua, kusema na kutenda yaliyo mema daima. Amina
 
Hakuna sahihi kwenye ule waraka kuna majina.

Mamlaka ya kuwasemea hao maaskofu anayatoa wapi? Wale maaskofu hakuna mjinga kati yao sio rahisi kuingizwa kwenye kitu wasichokitaka. Ukumbuke kuwa askofu anamamlaka kamili kwenye jimbo lake na haingiliwi na yoyote. Maaskofu namapdre huwajibishwa pale wanapopinga na misingi ya kanisa haujawahi kutokea mzozo wa kimamlaka katika kanisa katoliki Tanzania.
 
Mangonjwa mtambuka wewe ni mgonjwa kweli kweli kajpime dini siyo stagnant dini ni divesity tunasonga mbele. Tembea dunia uone dini inavoevolv. Stupid runny. watu tunatembea 5 continents we can lean who to cop with the changing world wewe kaaa na ukilaza wako.
 
Back
Top Bottom