Askofu Pengo: Sikufahamu kuhusu waraka wa Kwaresma wa Baraza la Maaskofu Katoliki. Awaasa wasichanganye dini na siasa

Hivi najiuliza huyu Pengo hakushirikishwa ktk huo waraka?na km hakushirikishwa ni kwanini wakati nae ni miongoni mwao?na katika maaskofu wote wakatoliki anayepinga huu waraka ni pengo pekee au !mwenzenu hata sielewi !mwenye ile clip ya Gwajima tafadhali aiweke hapa tujikumbushe alimwambia nini huyu mzee!
 
Sina tatizo na msimamo wake, maana ndio maana waliosema tusichanganye dini na siasa, maana hakuna uwezekano dhehebu lolote lile Tanzania kuwa na watu wa upande mmoja. wenye maoni sawa, ndio maana dini zikaambiwa zijikite na mambo ya imani.

Shida yangu: Maaskofu mlioandika kama kweli mumeandika, mtaingizaji jina la mtu asiyekuwa amehusika na waraka huo...

Hiyo tu si inaonyesha waraka ulikuwa na nia ovu?
 
Heko Kadinali PENGO. Wakati mwingine viongozi wa dini ni vema kufuata mafundisho ya KRISTO., alipoulizwa kodi alimwagiza mmoja wa mitume wake (BIBLE SAYS) akavue samaki, ampasue, alipe kodi wanayodaiwa. Hakuna 'DOBLE STANDARD' katika kulipa kodi, kila mtu afanye kazi, na alipe KODI. Inauma, lakini huo ndio ukweli. Msema kweli..... VIVA DR.JPM
 
Nimesikiliza kauli ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo. Nimesikitika. Na nimegundua mambo mawili:

1. Hajui tena wajibu wake kwa jamii anayoongoza.

2. Amefanya siasa kwa mgongo wa dini. Kwa wanaojua kwamba yeye ni mwanachama wa CCM na rafiki binafsi wa JPM, kauli yake ni sawa na utetezi wa mambo maovu yanayofanywa na serikali anayoipenda. Kwake, bora serikali kuliko kanisa!

Hii ni mara vya pili katika miaka mitatu, anatetea serikali, anapuuza msimamo wa kanisa.

Mwaka 2014 alipingana na kanisa kuhusu katiba inayopendekezwa; akasimama na CCM na serikali.

Kwa kauli na msimamo wake, Kardinali Pengo anafanya siasa chafu dhidi ya kanisa na jamii. Yeye anadhani kuchanganya dini na siasa maana yake ni kukosoa serikali. Haoni kwamba yeye anayeunga mkono serikali anachanganya dini na siasa.

Sasa naona hekima ya kanisa kuweka umri wa maaskofu kustaafu. Kardinali Pengo, ambaye anafikisha umri huo mwakani (2019), angeshauriwa apumzike mapema kuliko kuendelea kukwaza waamini.

Kiukweli, katika hili la kupingana na maaskofu wake, sioni aibu kusema: “he is not my bishop."

Huna lolote. Unatangaza Demokrasia Afu mtu akisema ukweli wake. Unakurupuka kama umebanwa na uharo. PENGO ANA AKILI KUBWA SANA. Watu wajinga kama nyie ambao mnakuwa mnapenda kusikia maskio yenu yanavyotaka. „HAMTASIKIA lakini HAMTAELEWA. MTATAZAMA LAKINI HAMTAONA“

Sauti ya kinabii ambayo VIONGOZI wa dini wanapaswa kuwa nayo Sio ya uchochezi. Kuna Lugha ya kinabii tena huruma „kama upanga wenye makali kuwili „. Ukiona ujumbe unanyooshea kidole kwa specifics ambazo Kama maaskofu hawawezi kujua. Ni Hatari sana.

Pengo anajua anachoongea ,kwa mbumbumbu ambaye unasoma kwa miwani ya SIO TU CHADEMA bali Chadema asiyejitambua. Hutaweza kuelewa. Wewe tafuta ukimbizi huku Ulaya ule bure.
 
Naona Pengo yuko sahihi katika hoja ya jina lake kuonekana kwenye waraka ambao hajashirikishwa na ikionekana ameshirimishwa hilo ni kosa ukiachilia mbali maudhui.
Lakini huwa nawaza siku moja dini tofauti zikitoa nyaraka zenye maudhui yanayokinzana haiwezi kuleta shida?

Tuwaachie wenye dini maana watu wa dini huwa wanajua kila kitu.
Sio muda maaskofu na mapadre wa RC watagombea nafasi za kisiasa nao wale mema ya nchi.
 
Kesho yangu isingekucha vema bila kutoa ya moyoni, japo najua hakuna wasomaji usiku but potelea mbali.

Nimekuwa nikitafakari sana kauli ya Pengo ambaye inasemekana amesema kwamba "Maaskofu wenzake wanajaribu kuchanganya dini na siasa kwenye waraka wao walioutoa"

Punde tena nilimuona mwana JF Paskali Mayalla akishabikia jambo hilo hilo kwamba dini isichanganywe na siasa. Japo nilimjibu ya kwamba Dini (mfano Ukatoliki) ilitumika mwanzoni kabisa kuwaleta watu pamoja na kuwarahisishia watawala wa Roma kwenye nyakati ambazo upagani ulikuwa umeshamiri. Kwa maana hiyo, wakati huo dini na siasa vilienda pamoja. Hata Ukatoliki wenyewe ulitokana na chimbuko la wanasiasa wa Roma waliokaa chini kupiga kura na kuuanzisha ukatoliki.

Kutoka nyakati hizo vitu hivi viwili havikuwahi kuachana wala kupishana. Wanasiasa wa mwanzo kwenye tawala kama Roma wanaelewa kwamba dini ndo ipo karibu na jamii na ili uwe na amani ya kudumu ndani ya jamii ni sharti wanasiasa (siasa) wapokee maono kutoka kwenye dini. Na hapa sio mambo ya kiroho wala kuombewa, hapa tunaongelea logic ya chombo kipi kipo karibu na jamii.

Kwa kauli ya Pengo kwamba eti, maaskofu wakiongelea masuala yanayohusu jamii na yanayosababishwa na wanasiasa kama mauaji, utekaji, dhulma za polisi, masuala ya katiba na mambo mengine ya kisiasa yanayoathiri jamii basi eti anadai kufanya hivo ni kuchanganya siasa na dini.

Binafsi imenishtua sana mtu kama Pengo kusema hivo, nimeutafakari sana uumini wangu wa dini ya ukristo-ukatoliki.

Kwa tafsiri nyingine Pengo na shule yake ya ufikiri, akina Paskal Mayalla, wao wanaiambia jamii kwamba masuala ya mauaji, utekaji, dhulma za Polisi, masuala ya katiba, na dhulma nyingine za kisiasa dhidi ya jamii yenye dini sio kipaumbele kwa kanisa.

They dont give a damn, jamii itekwe, jamii idhulumiwe, inyanyaswe halafu wewe Pengo unasema Maaskofu wasiyaangalie hayo wa concentrate na mambo yanayowahusu ya dini hayo ya siasa wayaache. Does it make sense? Yaani kwa mazingira ya kadhia katika jamii halafu wewe unasema jamii hii hii ya waumini waende wakakutane na maaskofu wakayajadili ya dini mwisho waseme Amen. Huku umepigwa kirungu cha mguu na polisi, huku mama unaambiwa mwanao hajulikani alipo, baba unaambiwa mwanao amepigwa risasi na polisi halafu wewe eti usahau hayo yote uende kanisani, msikitini, useme sheikh padri niombee na hizi mashida nyingi za dunia. This is weird country!!!! Endapo jamii itafanya hivo itakuwa ni jamii ya vichaa

Haya ni moja wapo ya mambo yanayochanganya sana akili anakuambia wewe usichanganye siasa na dini, na mimi namuambia hakuna haja ya kuendelea kwenda kanisani. Huo mda ntautumia kumuomba Mungu wa haki mwenyewe na kupambana mwenyewe na hao waovu kwenye kofia ya siasa.
 
Kesho yangu isingekucha vema bila kutoa ya moyoni, japo najua hakuna wasomaji usiku but potelea mbali.

Nimekuwa nikitafakari sana kauli ya Pengo ambaye inasemekana amesema kwamba "Maaskofu wenzake wanajaribu kuchanganya dini na siasa kwenye waraka wao walioutoa"...
Sasa unamwambia nani? Kama wewe hutaki kwenda kanisani kwa sababu ya kauli ya Pengo hiyo ni juu yako.
 
Kapoteza credibility huyu ya kuendelea kuwa kiongozi wa dini. Waumini wako wanatekwa, wanateswa, wanauwawa, katiba inadharauliwa, Bunge na mahakama vinadharauliwa, sheria za nchi zinapindishwa badala ya kusimama upande mmoja na waumini wake kaamua kusimama upande mmoja na dhalimu muuaji!!!!

Atengwe huyu hafai kuongoza tena.
 
Back
Top Bottom