Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini na ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ameitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), ‘kudhibiti wahuni wanaotaka kuvuruga amani visiwani humo'.Kauli hiyo ya Pengo ni ya kwanza tangu kuibuka kwa vurugu visiwani Zanzibar mapema mwezi huu, na kusababisha uharibifu wa mali, huku makanisa yakilengwa zaidi na kikundi kinachojiita cha Jumuiya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam (JUMIKI).
Pengo alitoa kauli hiyo wakati wa ibada maalumu iliyofanyika katika Kanisa la Msalabani Bagamoyo, mkoani Pwani, ikiwa ni maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Shirika la Roho Mtakatifu, utakaofanyika kwa siku 30 kuanzia jana.
Kardinali Pengo alisema, ‘wahuni hawawezi kuizidi Serikali makini'."Makanisa yetu yamecomwa moto na watu wahuni. Kama Serikali ipo na haiwezi kuchukua hatua dhidi ya wahuni, usalama uko wapi?" alihoji Kardinali Pengo.
"Wahuni wanaweza kutuunguzia makanisa saba kwa mpigo, lakini mbele ya hapo kuna makanisa kadhaa ambayo yalikwishaunguzwa na kubomolewa na hao wahuni," alisema.Pengo aliendelea kuhoji, "Kama sasa wahuni wameishinda nguvu Serikali ya watu kwa hiyo tutawaliwe na wahuni na wafanye lile wanalolitaka, tunajiuliza tunakwenda wapi?
Mara baada ya vurugu za Zanzibar, jopo la maaskofu kutoka madhehebu mbalimbali, walifanya mazungumzo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), huku wakiituhumu kushindwa kudhibiti vitendo vya uchomaji moto makanisa na kuihadharisha kuchukua hatua za haraka.
Jana, Pengo alilitaka shirika hilo kumsaidia Askofu Augustine Shayo wa Jimbo Katoliki Zanzibar, kuunganisha nguvu zao katika harakati za kuimarisha amani.
Pengo alisema mbali ya vurugu hizo, hivi sasa utumwa bado unandelea kukithiri nchini, hususan kwa viongozi wa Serikali kuwakandamiza wananchi wa hali ya chini.
Alisema wapo baadhi ya viongozi wanaotaka utumwa uendelee kuwapo kutokana na matendo yao dhidi ya wananchi.
"Tanzania ni huru sawa, lakini mimi sitaki kusadiki kuwa ni huru kwa kila mmoja na kila Mtanzania, wapo watu ambao wangependa wao waneemeke hata kwa madhara ya wengi bila huruma hadi siku ya leo," alisema na kuongeza:
"Tangu Shule ya St. Marian inaanzishwa, kuna baadhi ya viongozi wamekuwa wakitaka watoto wao wakasome pale na watoto wa maskini wasipate nafasi."
Alitoboa siri kuwa ‘kuna barua za maombi zisizo za msingi ambazo amekuwa akipelekewa Askofu Shayo na kuzikataa, na wakati mwingine amekuwa akitishiwa maisha, kwani wapo wanaotaka kuwasomesha watoto katika shule nzuri ili waendele kujineemesha. Sasa huu sio utumwa?'
Kardinali Pengo alililitaka Shirika la Roho Mtakatifu kutumia mkutano huo kuendelea kuhimiza amani hapa nchini na kutupia jicho Zanzibar, ambako amani inavurugika kwa matendo ya watu aliowaita wahuni.
Source:Mwananchi Jumatatu