Askofu Pengo na Balozi Ndobho wamjibu Nape

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo, amevitaka vyama vya siasa na serikali kwa ujumla kuacha mara moja kuwazuia watu wanaodaiwa kuwa mafisadi kwenda kupata huduma za kiroho.

Kauli ya Kardinari Pengo imekuja siku chache baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, kusema mafisadi walioenguliwa na chama hicho wanataka kuwatumia viongozi wa dini ili kujisafisha.


Pengo alitoa rai hiyo jana baada ya kuhitimisha ibada ya misa takatifu ya sikukuu ya Pasaka katika Kanisa la Mt Vinsent wa Paulo, wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani.


“Kanisa Katoliki halitamfukuza mtu yeyote yule anayedaiwa na serikali au chama kuwa ni fisadi eti asipate huduma zinazomstahili! Kanisa litampokea iwapo ni muumini mzuri na amekwenda kwa ajili ya kupata huduma za kiroho,” alisema.


Kumtenga mtu ni kosa. Mbona Yesu hakumkataa Maria Madgalena na Zakayo mtoza ushuru sasa iweje leo kanisa liwatenge watu wanaodaiwa kuwa ni mafisadi huku wakiwa ni waumini wa kanisa?


Aidha, alisema iwapo mtu hakubaliki katika chama si kweli kuwa na katika kanisa hakubaliki kwa kuwa chama na kanisa ni vitu viwili tofauti. Alisema vyama vinahitaji watu wasafi, lakini kanisa linahitaji wenye dhambi (watu wachafu) ili wapate kutubu na kumrudia Mungu ndio maana Yesu alikuja kwa ajili ya watu wagonjwa na si wazima.


Source: Tanzania Daima
 
Ni kweli Baba Kadinal, ila tu watubu wamrudie Mungu kwa ajili ya maisha ya baada ya kifo, lakini wasirudi kwenye vyama vyetu wakati huu bado wako hai, wapumzike siasa!
 
Hapo umenena baba Kadinal ila tu watubu kiukweli na sio kutakasa dhambi (kile walichotuibia warudishe kwanza kwa wananchi sio ndo wanatolea zaka(10%) au sadaka na hiyo ndo itakua maana halisi ya toba...!!!) :yawn:
 
*Asema kujivua gamba ni unafiki
*Amtuhumu kwa chuki na fitina
*Kahama nako mambo mazito
*K'njaro wahoji aliyemtuma Nape

Na Gazeti la Mtanzania




KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Paul Ndobho, ameiita hatua iliyochukuliwa na chama hicho ya kujivua gamba kuwa ni sawa na unafiki ambao kamwe Watanzania hawawezi kuukubali.

Balozi Ndobho alitoa msimamo huo alipozungumza na waandishi wa habari mjini Musoma, jana. Alisema si jambo jema kwa CCM kujifananisha na nyoka kwa vile kujitoa gamba kamwe hakuwezi kuondoa sumu ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wananchi. Tatizo si gamba,
bali sumu

"Pamoja kuwa mimi ni mwana CCM, lakini hawa jamaa zangu walichokifanya ni unafiki mkubwa na usanii wa hali ya juu, kwani tatizo la Watanzania lilikuwa gamba au sumu?" Alihoji Ndobho, ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Musoma Vijijini mwaka 1995-2000.


Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alikiri hadharani kuwa kwenye uchaguzi huo alimpigia kura Balozi Ndobho, licha ya ukweli kwamba alikuwa chama cha upinzani cha NCCR-Mageuzi.


Balozi huyo alisema kwamba suala la rushwa ndani ya CCM kamwe haliwezi kufananishwa na gamba la nyoka, kwa vile idadi kubwa ya viongozi wamekuwa wakipatikana kwa njia ya rushwa ambayo imekuwa kero kubwa kwa wananchi.

Wanyoosha vidole nao walipatikana kwa rushwa. Alisema inashangaza kuona chama kikubwa kama CCM kikiwanyoshea vidole baadhi ya watu kuwa ni vinara wa rushwa, wakati wakitambua wazi kuwa baadhi yao walipatikana kwa misingi hiyo hiyo.

"Kama CCM wanataka kujivua gamba ni vema viongozi wote wanaojua walichaguliwa kupitia fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) waanze wao kisha watafute wajumbe wa NEC ambao hata hapa tunawajua walipita kwa nguvu ya fedha, na si kwa kupendwa na wanachama waondoke, hivyo sisi tutaamini kweli hii ndio CCM ya Nyerere (Baba wa Taifa)," alisema.


Alisema idadi kubwa ya wajumbe wa NEC walipatikana kwa njia za kuhonga wajumbe, hivyo hawezi kujisafisha kwa kuwanyoshea vidole baadhi ya watu wakati wao pia walipatikana kwa njia za mkato na wengine kukwepa kodi za Serikali na fedha ambazo walitumia kununulia uongozi.


Kauli za Nape ni za chuki, fitna


Kuhusu kauli za Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, anazozitoa akidai kuwa ni uamuzi wa vikao, Balozi Ndobho alisema kauli hizo ni za chuki na fitina ambazo anazitumia kutaka kujipatia umaarufu. Alisema hatua hiyo inayotaka kuchukuliwa na CCM kwa kuwalenga baadhi ya watu inaweza kukimaliza chama hicho vibaya na kufanana na chama cha Kenya African National Union (KANU) cha nchini Kenya.


"Ushauri wangu, wasilenge watu katika kusafisha chama hata kama wewe ni mkubwa pisha ili watu waone umeonyesha njia, kwani hata Mwalimu Nyerere alituambia kuongoza ni kuonyesha njia," alisisitiza.


Alipongeza uamuzi wa NEC kubariki kuondoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, kuwa jambo hilo limeweza kurejesha heshima.


Alisema Makamba, licha ya kuwa mzigo, alikuwa pia akikivuruga chama kwa kupuuza kutatua kero zilizowasilishwa na wanachama kwake.


Kujivua gamba kuanzie Musoma Mjini


Alitoa wito kwa Sekretarieti mpya wakati ikiendelea na mpango wa kujivua gamba ianze na Wilaya ya Musoma Mjini kwa kuwatosa wote waliosababisha jimbo hilo lichukuliwe na Chadema. "Kama kweli wameanza kuondoa gamba waanze na Musoma Mjini, kwani sisi wanachama tuliwaambia viongozi huyo mnayempeleka kwa wananchi (mgombea ubunge) ni chaguo lenu tu, hakubaliki, bali kinachokubalika kwake ni fedha, wakabisha, sasa kwa vile wote wanajua walichokuwa wakivuna kwake tulianguka, sasa hapa napo unatafuta mchawi wakati unajua nani tatizo?" Alihoji.


Gamba nusura lisababishe ngumi Kahama


Mtafaruku miongoni mwa wana CCM umeibuka wilayani Kahama, baada ya kuwapo makundi mawili yanayokinzana juu ya uamuzi wa kuwataka viongozi wa chama hicho wilaya wajiuzulu.


Viongozi hao kuanzia ngazi ya matawi, kata na wilaya wanatakiwa wajiuzulu kama sehemu ya kuunga mkono uamuzi wa NEC Taifa wa kujivua gamba.


Uamuzi huo ulizua tafrani kubwa miongoni mwa viongozi wa matawi na kata wakati CCM Wilaya ilipoitisha kikao malumu cha Halmashauri Kuu ili kupongeza hatua iliyochukuliwa na NEC Taifa ya kujivua gamba.


Baadhi ya wana CCM walitaka viongozi wajiuzulu kutokana na kusababisha chama kifanye vibaya kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.


Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM Kata ya Bulungwa, John Kapaya, alihoji uongozi wa chama hicho wilaya akitaka useme ni kwa nini tathimini ya Uchaguzi Mkuu ilifanywa Machi, mwaka huu.


Alisema tayari Machi, mwaka huu mkoa ulikuwa umeshapeleka ripoti yake Makao Makuu.


"Dhambi waliyoifanya viongozi wa wilaya kuanzia kura ya maoni mpaka tathmini haipaswi kusamehewa, hivyo wanastahili wajijengee heshima kwa kujivua magamba, kwani tangu mchakato wa kura za maoni hawakuonyesha uadilifu," alisema Boniphace Paul, mkazi wa Kahama Nyakato.


Kundi la pili lilisisitiza kusameheana ndani ya chama kwa kuwa tayari kumeshaonekana kuporomoka kwa maadili.


Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Wilaya ya Kahama, Edward Msoma, alisema kila mwanachama ana dhambi ya uchaguzi kutokana na kutokuwa tayari kukipigania chama na vitendo vya rushwa.


Takukuru waliingia baada ya CCM kuharibika


Mmoja wa waasisi wa CCM Wilaya ya Kahama, Daud Masumbuko, alisema mmomonyoko wa maadili ulishajitokeza siku nyingi na kushamiri miongoni mwa makada ambao wamejitumbukiza katika rushwa.


"Kama ni kujivua gamba hakuna atakayebaki salama ndani ya chama, ndiyo maana Takukuru (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa) iliomba kukisimamia chama, hatua hiyo inadhihirisha tayari maadili yalishaporomoka kipindi kirefu, kwani hata waliopo bungeni hakuna msafi," alidai Masumbuko.


Ambaye hakutoa rushwa aape kwa kitabu cha dini


Mwanachama mwingine, Kundi Masanja, ambaye ni mkazi wa Kata ya Nyandekwa, alisema kama ni kuhukumu viongozi kutokana na matokeo mabovu yaliyopita itakuwa ni kuwaonea kwani kila mwanachama anastahili dhambi hiyo.


"Jamani tusihukumiane kwa rushwa, sote tumeshiriki haswa kwa hawa viongozi wa kuchaguliwa- madiwani na wabunge- tumeshiriki nao kikamilifu katika masuala ya rushwa, kama kuna anayedai hajatoa rushwa, basi asimame hadharani athibitishe ukweli wake kwa kushika kitabu cha dini," alisema Masanja.


Alisema si busara kushikana uchawi kwa upungufu uliokigharimu chama, bali kila mwanachama, hasa viongozi watubu dhambi ya uchaguzi waliyoifanya na kuweka kiapo katika nafsi zao kuwa wanarejea katika maadili.


Kilimanjaro wabashiri mpasuko mkubwa


CCM imetakiwa kuendesha mpango wa kukisafisha chama kwa kutumia busara zaidi kwa kuepuka malumbano yatakayoleta mpasuko.


Makada kadhaa mkoni Kilimanjaro wamesema malumbano yatasababisha uchochezi kwa kuwatumia baadhi ya wajumbe wa NEC kuwashawishi kutoa uamuzi usio sahihi kwa kuwahukumu wanachama na viongozi, hata wale wasiokuwa na hatia.


Kada wa CCM, Msafiri Kunda, alisema kuwa viongozi hao wanatakiwa kufanya kile kilichowaweka madarakani na si kutumiwa na watu wa nje kwa maslahi yao binafsi.


Alisema kauli ya Nape ya kuwapa wanachama miezi mitatu kujiuzulu si ya kukiendeleza chama, kwa kuwa ni jambo ambalo analifahamu kwa uhakika kuwa halikujadiliwa kwenye kikao cha NEC kilichomalizika mjini Dodoma hivi karibuni.


"Nape anatumiwa na watu wa nje ambao wanataka kujisafisha ili kugombea urais mwaka 2015 kwa maslahi yao binafsi, siyo vingine, tunamtaka aache kauli zake za uropokaji, kwani hilo silo tulilomtuma la kwenda kuwahukumu wanachama," alisema Kunda.


Alisema hali ilivyo sasa ni kwamba wanawapa wapinzani fursa kubwa ya kukiharibu chama kupitia wanachama.


Alisema Edward Lowassa na Rostam Aziz wamekisaidia chama, na akamsifu Lowassa kwa utendaji kazi mzuri.
 
Ili usamehewe dhambi rudisha kwanza chetu ndio mungu atakusamehe ila kama hujarudisha hata kanisa likuombee vipi utakwenda jikoni tu.
 
Sina hakika km kuna msafi hata mmoja...inawezekanaje wakati uko kwenye gari la taka? kuna haja ya kupiga deki kuanzia dereva hadi gari lenyewe! Kutoka hapo hata huyo Mungu rehema zake tutaziona zikitenda kazi,ila huu uteuzi wa wawakilishi wa ubadhirifu hofu yangu tutakamata paka ilihali panya wakisherehekea...pengine kujivua magamba ni kwa awamu,let us see!
 
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo, amevitaka vyama vya siasa na serikali kwa ujumla kuacha mara moja kuwazuia watu wanaodaiwa kuwa mafisadi kwenda kupata huduma za kiroho.

Kauli ya Kardinari Pengo imekuja siku chache baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, kusema mafisadi walioenguliwa na chama hicho wanataka kuwatumia viongozi wa dini ili kujisafisha.


Pengo alitoa rai hiyo jana baada ya kuhitimisha ibada ya misa takatifu ya sikukuu ya Pasaka katika Kanisa la Mt Vinsent wa Paulo, wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani.


"Kanisa Katoliki halitamfukuza mtu yeyote yule anayedaiwa na serikali au chama kuwa ni fisadi eti asipate huduma zinazomstahili! Kanisa litampokea iwapo ni muumini mzuri na amekwenda kwa ajili ya kupata huduma za kiroho," alisema.


Kumtenga mtu ni kosa. Mbona Yesu hakumkataa Maria Madgalena na Zakayo mtoza ushuru sasa iweje leo kanisa liwatenge watu wanaodaiwa kuwa ni mafisadi huku wakiwa ni waumini wa kanisa?


Aidha, alisema iwapo mtu hakubaliki katika chama si kweli kuwa na katika kanisa hakubaliki kwa kuwa chama na kanisa ni vitu viwili tofauti. Alisema vyama vinahitaji watu wasafi, lakini kanisa linahitaji wenye dhambi (watu wachafu) ili wapate kutubu na kumrudia Mungu ndio maana Yesu alikuja kwa ajili ya watu wagonjwa na si wazima.


Source: Tanzania Daima

Kila siku kwenye magazeti lazima usome "Kiongozi fulani ametaka/amewataka hili", "Wananchi wametakiwa hiki"; imekuwa kero kubwa kwa kweli huu msemo wa "amewataka", "wametakiwa", "Government has urged this and that". Hii ni Rhetorical Style ya muda mrefu sana (tokea enzi za Ujamaa) kwenye Vyombo vya Habari ambayo Watawala na Waandishi wa Habari wamekuwa wakitumia kwa makusudi mbele ya Umma ya Wafuatiliaji Habari magazetini, Redioni, kwenye Runinga, nk. ili kuwafanya Wananchi wawe passive, subservient, obedient, and otherwise totally under control siku zote. Katika nchi zote nilizoishi sijawahi kusoma style hii ya Uandishi wa Habari inayoonyesha kujikomba kwa Waandishi Habari kwa Watawala.
 
Unabii uliwahisema CCM itavunjikia mikononi mwa J. Kikwete. Niliupuza nilipousikia toka kunukuriwa kwa mchungaji mmoja wa TAG (Tz Assemblies of God). Sasa naona kama ni kweli unabii huo unaweza kutimia.
 
Quinine kazi yako unaiweza sina shaka una taaluma inayohusiana na mambo ya Marketing!
HA unaweza kufafanua, hii habari nimekopi toka gazetini wala sijaongeza kitu labda komenti yangu ni kwamba naungana na askofu kuwa kanisa ni tofauti na chama cha siasa lenyewe linapokea watu wote wahalifu na wema kwa hiyo Nape asiwachonganishe akina RACHEL na kanisa, lakini nashukuru kwa kwa kunipa kredit.
 
Hii mistari katika biblia ina maana gani?
1.Mwenye vingi ataongezewa
2.Akupigae kofi upande wa kushoto mgeuzie na wakulia

Je pengo ataweza kuwarekebisha kweli? au atawatia sumu zaidi ya kutuibia?
 
Ngoma aichezayo nape imechezwa sana na wengi bt wamepotezwa, wamesahaulika! Ngoma aichezayo Nnape haijui!
 
HA unaweza kufafanua, hii habari nimekopi toka gazetini wala sijaongeza kitu labda komenti yangu ni kwamba naungana na askofu kuwa kanisa ni tofauti na chama cha siasa lenyewe linapokea watu wote wahalifu na wema kwa hiyo Nape asiwachonganishe akina RACHEL na kanisa, lakini nashukuru kwa kwa kunipa kredit.

Mkuu hiyo ya RACHEL na Kanisa imetulia.
 
Back
Top Bottom