Askofu Pengo ana tabia ya usaliti toka zamani tumpuuze

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,145
2,000
Mlio karibu na Mh. Kadinali Pengo marafiki zake na ndugu zake hivi mmeshindwa kabisa kumshauri huyu mzee walau abakie na tuheshima twake tudogo kabla hajafa?

Miaka kadhaa iliopita taifa lilipita ktk mchakato mgumu wa maamuzi ya kikatiba. Taifa lilitakiwa kuamua aidha Mahakama ya kadhi yaingizwe ktk Katiba ya Tanzania au yasiingizwe.

Taasisi nyingi zilitoa maoni yao kadiri walivyo kubaliana. Kanisa Katoliki kupitia baraza la maaskofu walitoa msimamo wao kupinga na Askofu Pengo alisaini msimamo huo wa baraza la Maaskofu katoliki kuwa hawakubali Mahaka ya kadhi iingizwe ktk Katiba ya Tanganyika.

Baada ya baraza la maaskofu kutangaza msimamo wao. Baadae Askofu Pengo akajitokeza hadharani na kudai kuwa yeye anaunga mkono Mahakama ya Kadhi iingizwe ktk katiba ya jamuhuri ya Tanganyika.

Hapo ndipo nilipo mfahamu kaka mkubwa GWAJIMA. Gwajima alisema hivi. Kuna Mtu anajiita Askofu Pengo" Zamani nilikuwa namheshimu mimi lakini sasa simuheshimu tena. Yaani Baraza la maaskofu Katoliki limekataa kuhusu mahakama ya kadhi, na yeye pia alisaini makubaliano hayo. Halafu baadae anakuja kuropoka kuwakana maaskofu wenzie.Sijui alikula Maharage ya wapi huyu? Sijui Kavimbiwa huyu? Gwajima akajiuliza Sijui kazeeka huyu? Ondoka Mzee, Kalale mzee , hufai mzee."

Wakati taifa lipo ktk wakati mgumu kuliko wakati wote sasa hivi, watu wanauwa hovyo, wanapotea, wanatekwa, hakuna uhakika wa uhai kwa wapinzani na kuporwa kwa demokrasi na uhuru wa Watanganyika, halafu hili zee linajitokeza tena na kumpongeza Magufuli.

Wakati ule nilijua GWAJIMA ni mropokaji lakini kwa sasa naamini maneno ya Dr. Gwajima huyu hayuko sawa tulipuuze. Linaendeshwa na watu kama akina Bashite?
 

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
8,700
2,000
Cardinal Pengo ni Mtumishi wa Mungu

huwa hana unafiki Ameongea kweli

Watanzania ni Jamii ya watu wasiopenda kusikia ukweli
 

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,356
2,000
Mimi nasubiri siku Askofu Ruwaichi aongee, halafu nione kama Wachaga watamtukana kama wanavyotukana na kudhihaki Viongozi wengine wa kiroho wasio Wachaga.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom