Askofu Nyaisonga: Kukiri kwa Mkapa kwa aliyokosea ni ishara ya unyenyekevu

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,546
Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Mhashamu Askofu Gervas Nyaisonga, amesema kitendo Hayati Benjamin Mkapa kukiri mambo aliyowahi kukosea wakati wa uongozi wake akiwa Mkuu wa nchi katika kitabu chake cha ‘My life My Purpose’ ni ishara ya unyenyekevu na kumpenda Mungu.

edited.jpg

Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Mhashamu Askofu Gervas Nyaisonga.
Askofu Nyaisonga, ametoa kauli hiyo leo wakati wa ibada ya mazishi ya kuaga mwili wa Hayati Mkapa katika jijini cha Lupaso na kuwataka watu kuishi maisha ya haki, utu na uadilifu ili kusudio la Mungu katika uumbaji lipate kutimia, kwa kuwa tulipo ni wasafiri na kwamba inatupasa kuishi na kutenda kwa busara mema tusije tukalemewa na kubeza tunayaona, na tutumie vizuri muda wa sasa.

“Kama mnavyoona alifanya toba ya hadhara na kuandika kitabu chake cha ‘My Life My Purpose’ toba ni hujenga, uvumilivu, msamaha, kujikatalia, uwajibikaji na nyingine nyingi ambazo zimebaki kama kielelezo cha kufikia uzima wa milele,”alisisitiza.

Moja ya mambo aliyokiri kukosea katika kitabu chake hicho ni kuhusiana na suala la Jeshi la Polisi kuwavamia na kuwapiga wafuasi wa upinzani walipokuwa wakiandamana mwaka 2001 visiwani Zanzibar jambo lililosababisha mauaji jambo ambalo halikumfurahisha yeye wakati akiwa ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema dhambi ya kutofanya kitu ndiyo inatawala dunia kwa leo, hutashitakiwa na mtu lakini hutashtakiwa kwa kutofanya lolote, na kwamba siyo kuungama kwa maneno bali kutafsiri kwa vitendo na kwadhati tunayojifunza.

Askofu Nyaisonga, amesema Rais Mkapa kila alipokwenda kusoma ndani na nje ya nchi alijiunga na chama cha wanafunzi Wakotoliki, jambo ambalo ni fundisho kwa watu na kwamba hakuogopwa na watu ndani na nje ya kanisa, na hakuogopwa na watu wake .
 
Pumzika kwa amani baba tuta kumiss. Wachache sana huwa wanakili udhaifu wao. Unastahili utakatifu baba.

Watanzania bado tunapenda ushabiki kuliko uhalisia. Tunaishi maisha siyo yetu "fake life" wewe ulipenda tuishi maisha halisi pamoja na changamoto zetu ili tutatafakari na kutatua changamoto hizo. Maisha ya kujitegemea. Asante baba pumzika Baba tutakumis sana
 
Ni Unyenyekevu wa hali ya juu sana.
Hakika ilikuwa ni toba iliyo kuu kwani itadumu vizazi na vizazi.
Pumzika Mpendwa wetu Hayati Benjamin William Mkapa Rais wa awamu ya Tatu wa JMT ,Mwenyezi Mungu aiweke roho yako mahala pema peponi.
Amina.
 
Kwaio na hawa wa sasa na wao watakuja kuandika kitabu uko baadae na kukiri picha linakua limeisha au sio
 
Ni jambo jema kutubu na kusamehewa/pia kusamehe. Lakini kama toba hiyo haikuwaendea in person walio na majonzi ya kuuliwa ndugu zao /wapendwa wao mfano huko Zanzibar, basi sidhani kama toba hiyo inakubalika! ( labda sijui toba ni nini, niko tayari kuelimishwa), hasa pale unapoua wapinzani wako wa mawazo mbadala kwa sababu ya kubaki madarakani! ...

Baba Askofu, umetoa neno jema kuwa watu katika mitandao ya kijamii wajiepushe na "lawama" juu ya Mzee wetu Mkapa! Ni onyo jema sama, tumuenzi Mzee wetu Mkapa.

LAKINI, Baba Askofu, likewise nanyi viongozi wa dini nawaambia mjiepushe kukaa kimya wakati watu wanatendewa MAOVU na Watawala kinyume na mapenzi ya Mungu mnayoyahubiri. Mkikemea mabaya kwa watawala wetu, likitokea kama hili, mkikemea watu kujiepusha na kumsema marehemu mitandaoni, mtasikilizwa. Watu wanapopigwa risasi 38, mkakaa kimya! Watu wanapopotea.. Akina Ben, Azory, Mawazo mlikaa kimya bila kukemea, mtasikilizwa shingo upande.
 
Kwa mahubiri ya baba Askofu, ndiyo hivyo. Ua, tesa, poteza, funga, bambika kesi.... mwishoni andika kitabu utubu! Ridiculous!
 
Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Mhashamu Askofu Gervas Nyaisonga, amesema kitendo Hayati Benjamin Mkapa kukiri mambo aliyowahi kukosea wakati wa uongozi wake akiwa Mkuu wa nchi katika kitabu chake cha ‘My life My Purpose’ ni ishara ya unyenyekevu na kumpenda Mungu.

edited.jpg

Askofu Nyaisonga, ametoa kauli hiyo leo wakati wa ibada ya mazishi ya kuaga mwili wa Hayati Mkapa katika jijini cha Lupaso na kuwataka watu kuishi maisha ya haki, utu na uadilifu ili kusudio la Mungu katika uumbaji lipate kutimia, kwa kuwa tulipo ni wasafiri na kwamba inatupasa kuishi na kutenda kwa busara mema tusije tukalemewa na kubeza tunayaona, na tutumie vizuri muda wa sasa.

“Kama mnavyoona alifanya toba ya hadhara na kuandika kitabu chake cha ‘My Life My Purpose’ toba ni hujenga, uvumilivu, msamaha, kujikatalia, uwajibikaji na nyingine nyingi ambazo zimebaki kama kielelezo cha kufikia uzima wa milele,”alisisitiza.

Moja ya mambo aliyokiri kukosea katika kitabu chake hicho ni kuhusiana na suala la Jeshi la Polisi kuwavamia na kuwapiga wafuasi wa upinzani walipokuwa wakiandamana mwaka 2001 visiwani Zanzibar jambo lililosababisha mauaji jambo ambalo halikumfurahisha yeye wakati akiwa ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema dhambi ya kutofanya kitu ndiyo inatawala dunia kwa leo, hutashitakiwa na mtu lakini hutashtakiwa kwa kutofanya lolote, na kwamba siyo kuungama kwa maneno bali kutafsiri kwa vitendo na kwadhati tunayojifunza.

Askofu Nyaisonga, amesema Rais Mkapa kila alipokwenda kusoma ndani na nje ya nchi alijiunga na chama cha wanafunzi Wakotoliki, jambo ambalo ni fundisho kwa watu na kwamba hakuogopwa na watu ndani na nje ya kanisa, na hakuogopwa na watu wake .

(QUOTE)
ni kweli kabisa lakini leo watu tunaogopwa na tunatisha wengine kwa kuumiza tunataka kuonekana jinsi tulivyo wababe kwa kunyima haki wengine wenye maskio na asikie tunafunga jela bila makosa
 
Ni jambo jema kutubu na kusamehewa/pia kusamehe. Lakini kama toba hiyo haikuwaendea in person walio na majonzi ya kuuliwa ndugu zao /wapendwa wao mfano huko Zanzibar, basi sidhani kama toba hiyo inakubalika! ( labda sijui toba ni nini, niko tayari kuelimishwa), hasa pale unapoua wapinzani wako wa mawazo mbadala kwa sababu ya kubaki madarakani! ...

Baba Askofu, umetoa neno jema kuwa watu katika mitandao ya kijamii wajiepushe na "lawama" juu ya Mzee wetu Mkapa! Ni onyo jema sama, tumuenzi Mzee wetu Mkapa.

LAKINI, Baba Askofu, likewise nanyi viongozi wa dini nawaambia mjiepushe kukaa kimya wakati watu wanatendewa MAOVU na Watawala kinyume na mapenzi ya Mungu mnayoyahubiri. Mkikemea mabaya kwa watawala wetu, likitokea kama hili, mkikemea watu kujiepusha na kumsema marehemu mitandaoni, mtasikilizwa. Watu wanapopigwa risasi 38, mkakaa kimya! Watu wanapopotea.. Akina Ben, Azory, Mawazo mlikaa kimya bila kukemea, mtasikilizwa shingo upande.
kabisa waseme ukweli wakemee na kuonya
 
Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Mhashamu Askofu Gervas Nyaisonga, amesema kitendo Hayati Benjamin Mkapa kukiri mambo aliyowahi kukosea wakati wa uongozi wake akiwa Mkuu wa nchi katika kitabu chake cha ‘My life My Purpose’ ni ishara ya unyenyekevu na kumpenda Mungu.

edited.jpg

Askofu Nyaisonga, ametoa kauli hiyo leo wakati wa ibada ya mazishi ya kuaga mwili wa Hayati Mkapa katika jijini cha Lupaso na kuwataka watu kuishi maisha ya haki, utu na uadilifu ili kusudio la Mungu katika uumbaji lipate kutimia, kwa kuwa tulipo ni wasafiri na kwamba inatupasa kuishi na kutenda kwa busara mema tusije tukalemewa na kubeza tunayaona, na tutumie vizuri muda wa sasa.

“Kama mnavyoona alifanya toba ya hadhara na kuandika kitabu chake cha ‘My Life My Purpose’ toba ni hujenga, uvumilivu, msamaha, kujikatalia, uwajibikaji na nyingine nyingi ambazo zimebaki kama kielelezo cha kufikia uzima wa milele,”alisisitiza.

Moja ya mambo aliyokiri kukosea katika kitabu chake hicho ni kuhusiana na suala la Jeshi la Polisi kuwavamia na kuwapiga wafuasi wa upinzani walipokuwa wakiandamana mwaka 2001 visiwani Zanzibar jambo lililosababisha mauaji jambo ambalo halikumfurahisha yeye wakati akiwa ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema dhambi ya kutofanya kitu ndiyo inatawala dunia kwa leo, hutashitakiwa na mtu lakini hutashtakiwa kwa kutofanya lolote, na kwamba siyo kuungama kwa maneno bali kutafsiri kwa vitendo na kwadhati tunayojifunza.

Askofu Nyaisonga, amesema Rais Mkapa kila alipokwenda kusoma ndani na nje ya nchi alijiunga na chama cha wanafunzi Wakotoliki, jambo ambalo ni fundisho kwa watu na kwamba hakuogopwa na watu ndani na nje ya kanisa, na hakuogopwa na watu wake .
ONYENI WAAMBIENI WATU WAACHE KUUMIZA WENGINE KUUWA KUPIGA KUJIMWAMBAFY
 
Watu wakizeeka kumbe huwa wanakuwa wanyenyekevu. Mkapa niliyemfahamu wakati akiwa Rais hakuwa mnyenyekevu. Nakumbuka alikuwa akigombana mara nyingi na waandishi wa habari. Kuna siku alikuwa BBC Hard Talk akampandishia mtangazaji aliyekuwa anamhoji (Sebastian). Sebastian akamuuliza, "President Mkapa, why are you angry?"
 
Sebastián alimuuliza Mzee Mkapa.. Mr President you sound angry. Akajibu yes I am. Ilikuwa kufuata mauaji ya Zanzibar ambayo yalitokeaje akiwa London. Actually, Mhusika mkuu inawezekana kabisa alikuwa ni Makamu wake maana yeye hakuwepo nchini. Alichukuwa responsibility kwa kuwa alikuwa ni mkuu wa nchi.
 
Tutachinjwa sana kwa sababu tu myawala mwishooooooooni atandika kitabu kukili aliuoyenda akiwa na madaraka na watu watibuka wakisema ametubu

Huku watu alivunjwa miguu alimiminiwa risasi watu walifukiwa bira ndg kijua wamefukiwa wapi kutesa na kutukana kupoteza na kila Aina ya mateso , poa lakini nyie mnaoibuka na kutetea hayo nyie ndio chanzo Cha mateso haya kemeeni kwanza ili msijekuja kutetea viyabu wakati roho zimeumizwa.
 
Back
Top Bottom