Askofu Niwemugizi: Rais Magufuli aliagiza nirejeshewe Passport yangu na alisema 'Wewe ni Askofu wangu utanizika'

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,207
42,068
Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi amesema aliyekuwa Rais wa Tanzania marehemu, John Magufuli aliagiza arejeshewe hati yake ya kusafiria na alimtamkia mara mbili kuwa kiongozi huyo wa kiroho ndiye atakayemzika.

Akizungumza leo Alhamisi Machi 25, 2021 katika Kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato, Askofu Niwemugizi ambaye hakutaja muda maalum wa agizo la kurejeshewa hati hiyo, amesema Magufuli aliagiza idara ya uhamiaji kumrejeshea.

"Kwa kweli niwaambie mara mbili, Magufuli aliniambia, ‘wewe ni Askofu wangu utanizika. Mwaka ule 2015 akaniambia hivyo, mara ya pili akamwagiza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anirudishie passport akaniambia wewe ni Askofu wangu utanizika.”

Wasalaamaidi, soma: Askofu Niwemugizi wa Kanisa Katoliki aitwa Uhamiaji kuhojiwa juu ya uraia wake
 
Back
Top Bottom