#COVID19 Askofu Niwemugizi, asitisha Misa na Ibada zote Jimbo la Rulenge, awataka waumini Wasali Majumbani pia Wajikinge na Corona

Ndio maana ninyi mkaifunga makkah?

Hivi ktk uislamu hamnaga kabisa mambo ya uponyaji eeh?
Ni kweli , hata hakuna haja ya kunawa mikono na kuvaa barkoa kwani ikiwa wao na wewe ni Mkristo wa kweli ni lazima uyakumbuke maneno ya Yesu aliposema

Bwana akasema: “Kama mngekua na imani kiasi cha chembe ya haridali mngeuambia mkuyu huu, ng'oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii.” (Luka17:7).

Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia mkiwa na imani , msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, ngo'ka ukatupwe baharini, litatendeka. na yoyote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea.
(Mathayo 21:21-22)

SASA TUNAKUOMBA WEWE KAMA UNAYO KWELI IMANI BASI ANZA KUIAMBIA KORONA ONDOKA ULIMWENGUNI ,

ILI TUPATE NAFUU , VYENGINEVYO NA WEWE UTAKUWA NI MMOJA WA MATAPELI TU NA WALA HUNA IMANI YOYOTE NA YESU NnA WALA WEWE SI MKRISTO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kanisa Katoliki Jimboni Rulenge-Ngara, wamesitisha kabisa Ibada/misa. Watu wasali nyumbani! Pia amewataka waumini wajikinge na COVID-19 na kuchukua tahadhari


Kanisa Katoliki Jimbo la Rulenge-Ngara limesema limesitisha Ibada za Misa, maadhimisho mengine yanayokusanya Waumini wengi Kanisani na sala za Jumuiya kwa muda wa mwezi mmoja kuanzia Aprili 19, 2020

Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo hilo amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kutafakari alama za nyakati na kujifunza kutoka kwa watu wa Ulaya, Marekani na nchi za jirani na hatua ambazo Baba Mtakatifu alizichukua kwa kutoa maelekezo kwa Maaskofu Wakatoliki Duniani na namna ya kuadhimisha Ibada

Amesema pamoja na kumshukuru Rais Magufuli kutotoa amri ya kufunga Makanisa na Misikiti, akihimiza kufanya ibada kumuomba Mungu atunusuru na janga hili, kama Mchungaji wa Jimbo la Rulenge-Ngara ameamua kuchukua uamuzi huo

Aidha, Askofu Niwemugizi amesema pale itakapowezekana wataomba redio Kwizera irushe adhimisho la Misa fupi na Waamini wafuatilie redioni. Baada ya mwezi kuisha Kanisa litaangalia hali ilivyo ili kama iliongeze muda

Pia, amewataka mapadre kuadhimisha misa peke yao kwa niaba ya waumini kuwaombea na kuiombea dunia ili Mungu atunusuru na #COVID19 hili na kuagiza sala za Jumuiya kufanyika ndani ya familia kwa familia moja moja
View attachment 1422602
Nilitegemea kardinari atoe tamko hili, baada ya kuchelewa sana bado ana nafasi ya kutoa kuliko kuangalia tu!
 
Huyo hamuogopi Mungu anaogopa Corona angekuwa anaogopa Mungu asingezuia ibada kufanyika kanisani.Hana lolote
Rwanda watu waliuawa ndani ya makanisa.

Kanisa ni imani yako, siyo jengo. Jengo linaweza kuchomwa moto, linaweza kuwa na virusi vya Corona. Watu wanaweza kuambukizwa Corona ndani ya jengo la kuabudia.

Kanisa la kweli ni imani yako ambayo haiishi ndani ya jengo la kuabudia, isipokuwa lipo nafsini mwako.
 
Linapokuja swala la maaskofu wasioyumba huyu ni mmoja wao misimamo yake ilipelekea mpaka akahojiwa uraia wake

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Wajua kuna sated standards za kila kitu:mfano mdogo tu ni ufugaji wa kuku wa kisasa,kama hufuati taratibu za ufugaji wa kisasa(especially kitu kinaitwa Biosecurity)utapata hasara kubwa sana kwa kuwa kuku watakufa dk sifuri.
-Kufunga shughuli zozote kwa mantiki ya Biosecurity iyo ni Godly intelligence,then ukiomba God God intervention utafanikiwa..!
-Kwa hivo Askofu ametengeneza mazingira mazuri sana ya kusikilizwa na Mungu baada ya kuchukua hatua.
-look,hata Ibrahim alipoagizwa akamtoe mwanae wa pekee sadaka hakuhoji,alichukua kwanza hatua ndipo intervention ya Mungu ikafuata..
-Hatua sahihi kwanza, then kifuatacho ni agenda nyingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante.

Kwa maana hiyo ina maana Kadinali ana cheo zaidi ya Askofu, hivyo sitashangaa huo uamuzi wa Askofu ukiondolewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Haiko hivyo unavyojua wewe. Askofu ni Mkuu wa jimbo husika. Yeye ana mamlaka yote juu ya Jimbo lake ilimradi havunji sheria za kanisa

Unafahamu kwamba kuna nchi hazina na hazijawahi kuwa na kardinali? Kwa hizo nchi ni nani sasa anakuwa kiongozi wa maaskofu?

Maaskofu wana chombo chao kinachowasimamia, Baraza la maaskofu! Katika hicho chombo mkuu wao ni Rais wa Baralaza la maaskofu. Huyo ndo anaweza kutoa maelekezo na yakafuatwa! Hata kardinali kama ni askofu (kumbuka kardinali sio lazima awe askofu) atalazimka kuyafuata.

Hata hivyo maelekezo hayo lazima yawe yameungwa mkono na angalau robo tatu ya maaskofu wote sio Rais wa TEC aamke asubuhi tu na kusema fanyeni hivi au vile. Hapo atakuwa anatoa maoni yake binafsi kama Mimi na wewe tunavyochangia hapa. Kauli na maelekezo ambayo lazima yafuatwe yanatoka kwa Papa tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa maana nyingine unatuambia hakuna maana ya kuwa na
viongozi
Serikali

Kama kila mmoja atafanya maamuzi kivyake vipi wale wasioweza kujisimamia mf wazee, watoto wasio na walezi mtaani, wagonjwa, wafungwa nk
Waachwe wafe?

Ni lipi jukumu namba 1 la serikali kwa maoni yako?
Kwanini wanapokusanya kodi hawasemi wanaotaka watoe na wasiotaka waache hatufungwi, kwanini kwenye majanga muwatelekeze wananchi?

Kwenye kukusanya kodi wananchi hawana akili wanalazimishwa na wengine kufungwa kwa kuhujumu uchumi Ila kwenye majanga wananchi wana akili waatelekezwa wapambane wenyewe

Hii ndio sababu inayotufanya tuchague viongozi?
Kusali hulazimishwi ukijisikia kusali nenda hujisikii usiende acha kutupia lawama zisizo na msingi watu .

Unaogopa kuwa utapata corona ukienfa kanisani kuwa Mungu atakupa corona kanisani kwake usiende

Tamko la nini wakati kusali ni hiari yako Wewe Fanya maamuzi kuwa utaenda au huendi.Hufungwi pingu kwenda kanisani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Askofu huyo akili hana alipo Mungu shetani hakajagi awe corona au Nani.Hana Mungu huyu Askofu na hajui uwezo Wa Mungu

Na hajui kanisani kuwa Mungu akiwepo hakuna corona

Askofu mpagani huyo

Wasabato mna shida sana sijui vichwa vyenu vimejaa nini sasa kosa la askofu nini na wakati ata ukatoliki haukuhusu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Huyo hamuogopi Mungu anaogopa Corona angekuwa anaogopa Mungu asingezuia ibada kufanyika kanisani.Hana lolote

Vipi na Yusufu alipo mficha Yesu Misri alikuwa hana imani kuwa Mungu anaweza kumuokoa mtoto Yesu

Ukinijibu hili swali ntahamia dhehebu lako


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom