Askofu Niwemugizi, asitisha Misa na Ibada zote Jimbo la Rulenge, awataka waumini Wasali Majumbani pia Wajikinge na Corona

Roving Journalist

JF-Expert Member
Apr 18, 2017
597
1,000
Kanisa Katoliki Jimboni Rulenge-Ngara, wamesitisha kabisa Ibada/misa. Watu wasali nyumbani! Pia amewataka waumini wajikinge na COVID-19 na kuchukua tahadhari


Kanisa Katoliki Jimbo la Rulenge-Ngara limesema limesitisha Ibada za Misa, maadhimisho mengine yanayokusanya Waumini wengi Kanisani na sala za Jumuiya kwa muda wa mwezi mmoja kuanzia Aprili 19, 2020

Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo hilo amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kutafakari alama za nyakati na kujifunza kutoka kwa watu wa Ulaya, Marekani na nchi za jirani na hatua ambazo Baba Mtakatifu alizichukua kwa kutoa maelekezo kwa Maaskofu Wakatoliki Duniani na namna ya kuadhimisha Ibada

Amesema pamoja na kumshukuru Rais Magufuli kutotoa amri ya kufunga Makanisa na Misikiti, akihimiza kufanya ibada kumuomba Mungu atunusuru na janga hili, kama Mchungaji wa Jimbo la Rulenge-Ngara ameamua kuchukua uamuzi huo

Aidha, Askofu Niwemugizi amesema pale itakapowezekana wataomba redio Kwizera irushe adhimisho la Misa fupi na Waamini wafuatilie redioni. Baada ya mwezi kuisha Kanisa litaangalia hali ilivyo ili kama iliongeze muda

Pia, amewataka mapadre kuadhimisha misa peke yao kwa niaba ya waumini kuwaombea na kuiombea dunia ili Mungu atunusuru na #COVID19 hili na kuagiza sala za Jumuiya kufanyika ndani ya familia kwa familia moja moja
IMG-20200418-WA0047.jpg
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
39,574
2,000
Safi sana,huu ndio utumishi wa Mungu tunaouhitaji.

Better late than never.

Waumini katika maeneo mengine, mjiongeza,msisubiri taarifa kama hii kwani si kila kiongozi wa dini atafanya hivi katika maeneo yenu.

Viongozi wa madhehebu mbalimbali(RC,KKKT.n.k) wanaokutana kutoa matamko ya pamoja(waraka) kama ya kukemea maovu,kukemea wanasiasa,n.k,walipaswa kuwa wamekutana na kuja na tamko kama hili; hivyo, tunatumai tangazo hili litatumika kama mfano kwa viongozi wengine wa dini waliobaki.

Baba Askofu,katika hili,umevaa viatu vilivyowapwaya wengi wakiwemo viongozi wa dini na wasio viongozi wa dini.

Hongera sana Baba Askofu!
 

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
2,243
2,000
Askofu wa Jimbo katoliki la Rulenge- Ngara amewataka waumini wake kutumia redio kufuatilia Ibada na sala kwa muda huu wa mlipuko wa #COVID19

Aidha mapadri wa Jimbo hilo wataendelea kuongoza misa peke yao ili kuliombea taifa wakati waumini watabaki nyumbani ili kuepusha misongamano

Agizo hilo litaanza kutekelezwa Aprili 19. Pia amewataka wenyeviti wa walei kuangalia namna ya kuwalisha mapdri kwa kipindi hiki ili wasife njaa

1587219815878.png
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom