BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,007
Siku chache zilizopita, nilisema jinsi ambavyo Maaskofu tulivyoandamwa na mamlaka kwa vitisho hadi baadhi ya Maaskofu wakaamua 'kuomba poo' lakini wengine tusonga mbele!
Sasa soma ushuhuda wa Mhashamu Baba Askofu Severine Niwemugizi wa Kanisa [Roman Katoliki] Jimbo la Rulenge - Ngara, unaoeleza jinsi ambavyo Maaskofu wa Kanisa Katoliki walivyotishwa na mamlaka mwaka 2016, hatua ambayo ilipelekea baadhi ya Maaskofu 'kuomba poo', lakini wengine wakasonga mbele
Sote tunamtumikia Mungu Aliye Hai! Utofauti wa Makanisa yetu hauondoi umoja wetu katika Roho Mtakatifu tunapoteseka kwa ajili ya haki ya wengine!
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki.
Ufuatao ni ushuhuda wa Mhashamu Baba Askofu Niwemugizi!
""Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu. Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri” (Mdo 4:29-31).
Ee Bwana, mwaka 2016 maaskofu Katoliki wa Tanzania tuliulizwa kupitia Rais wa Baraza wakati huo: “mmepata wapi mamlaka ya kuandika mliyoyaandika katika Ujumbe wa wenu wa Kwaresima?” Tukaambiwa katiba zetu (statutes) hazitupi mamlaka hayo, bila kujua mamlaka yetu hayatokani na Statutes zile tu. Likawa tisho kwetu. Baadhi yetu kwa tisho hilo wakajitenga na ujumbe huo. Lakini sisi tukaamua kusali tu.
Ni faraja kubwa Mungu ni msikivu sana kuliko binadamu. Anatudhihirishia daima kuwa sala ina nguvu sana. Mitume walitishwa pia na mamlaka za Baraza kuu la Wayahudi baada ya Petro kutoa hotuba ya kuwasuta kwa kumsulubisha Yesu lakini Mungu akamfufua katika wafu. Wakasema, “tuwatishe wasiseme tena na mtu awaye yote kwa jina hili” (Mdo 4:17). Mitume na jumuia ya waamini wakaamua kusali tu. Matokeo yake wakajawa na Roho Mtakatifu, na woga ukawaishia.
Katika mazingira mengine kunyamaza na kusali kunaweza kutosha kuleta suluhu kwa changamoto za wakati, bila kupambana kwa majibizano na wenye mamlaka. Kristo alileta wokovu bila kupambana na mamlaka. “Alionewa, lakini alinyenyekea, wala hakufunua kinywa chake; kama mwanakondoo apelekwaye machinjoni, ...” (Isa 53:7).
Tujalie neema yako Bwana itusaidie kuhimili matisho na kebehi au dharau zitujiazo kanisa kwa kutimiza wajibu wetu. Inapobidi tuwe “na busara kama nyoka, na kuwa wapole kama hua” kwa kunyamaza na kusali. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina."