Askofu Niwemugizi ashuhudia jinsi baadhi ya maaskofu 'walivyoomba poo' baada ya kitisho kutoka kwa mamlaka

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
111,753
2,000
Siku chache zilizopita, nilisema jinsi ambavyo Maaskofu tulivyoandamwa na mamlaka kwa vitisho hadi baadhi ya Maaskofu wakaamua 'kuomba poo' lakini wengine tusonga mbele!

Sasa soma ushuhuda wa Mhashamu Baba Askofu Severine Niwemugizi wa Kanisa [Roman Katoliki] Jimbo la Rulenge - Ngara, unaoeleza jinsi ambavyo Maaskofu wa Kanisa Katoliki walivyotishwa na mamlaka mwaka 2016, hatua ambayo ilipelekea baadhi ya Maaskofu 'kuomba poo', lakini wengine wakasonga mbele

Sote tunamtumikia Mungu Aliye Hai! Utofauti wa Makanisa yetu hauondoi umoja wetu katika Roho Mtakatifu tunapoteseka kwa ajili ya haki ya wengine!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki.

Ufuatao ni ushuhuda wa Mhashamu Baba Askofu Niwemugizi!

""Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu. Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri” (Mdo 4:29-31).

Ee Bwana, mwaka 2016 maaskofu Katoliki wa Tanzania tuliulizwa kupitia Rais wa Baraza wakati huo: “mmepata wapi mamlaka ya kuandika mliyoyaandika katika Ujumbe wa wenu wa Kwaresima?” Tukaambiwa katiba zetu (statutes) hazitupi mamlaka hayo, bila kujua mamlaka yetu hayatokani na Statutes zile tu. Likawa tisho kwetu. Baadhi yetu kwa tisho hilo wakajitenga na ujumbe huo. Lakini sisi tukaamua kusali tu.

Ni faraja kubwa Mungu ni msikivu sana kuliko binadamu. Anatudhihirishia daima kuwa sala ina nguvu sana. Mitume walitishwa pia na mamlaka za Baraza kuu la Wayahudi baada ya Petro kutoa hotuba ya kuwasuta kwa kumsulubisha Yesu lakini Mungu akamfufua katika wafu. Wakasema, “tuwatishe wasiseme tena na mtu awaye yote kwa jina hili” (Mdo 4:17). Mitume na jumuia ya waamini wakaamua kusali tu. Matokeo yake wakajawa na Roho Mtakatifu, na woga ukawaishia.

Katika mazingira mengine kunyamaza na kusali kunaweza kutosha kuleta suluhu kwa changamoto za wakati, bila kupambana kwa majibizano na wenye mamlaka. Kristo alileta wokovu bila kupambana na mamlaka. “Alionewa, lakini alinyenyekea, wala hakufunua kinywa chake; kama mwanakondoo apelekwaye machinjoni, ...” (Isa 53:7).

Tujalie neema yako Bwana itusaidie kuhimili matisho na kebehi au dharau zitujiazo kanisa kwa kutimiza wajibu wetu. Inapobidi tuwe “na busara kama nyoka, na kuwa wapole kama hua” kwa kunyamaza na kusali. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina."
 
Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
14,240
2,000
Hakika kila mtu alitishwa. Ninaamini atakuwa aliungama dhambo zote na kuomba msamaha kwa wote kwa imani kuwa amesamehewa. Unapambanaje na viongozi wa dini? Huku kila wakati unataja jina la Yesu. Nimesahau hata Shetani analitaja jina la Yesu tena akitetemeka. 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Bu'yaka

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
1,435
2,000
Kosa ni udhaifu usio na mfano wa Mama Janet Magufuli aliyekubali mumewe azikwe na hasimu wake wa kisiasa, Askofu Mugenyizi.

Eti Askofu kadai "marehemu aliwahi kunambia utakuja kunizika." Maaskofu wenzake wakanunua stori, familia nayo imekaa tu na butwaa inapelekeshwa na maamuzi ya watu wasiojali chochote cha legacy ya marehemu.

Sasa Askofu Mugenyizi anaenda kuwa unhinged zaidi na zaidi.
 
Lombo

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
4,632

Mama Janeth n mtu Muungwana Sana,hakuathirika na matendo ya mume wake ...Kama wewe kapuku ulivoathirika!
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
42,675
2,000
Hakika kila mtu alitishwa. Ninaamini atakuwa aliungama dhambo zote na kuomba msamaha kwa wote kwa imani kuwa amesamehewa. Unapambanaje na viongozi wa dini? Huku kila wakati unataja jina la Yesu. Nimesahau hata Shetani analitaja jina la Yesu tena akitetemeka. 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Dikteta alikuwa mtu hatari sn
 
Janja weed

JF-Expert Member
Nov 20, 2020
561
1,000
Niwemugizi aliumizwa sana mpaka wakamchukulia poasport yake kwa madai sio Raia, cha ajabu Mungu anavyopinga dhuluma na uonevu akamchukua jiwe na kwa hasira zaidi Niwemugizi ndio aliomzika yaani Dunia inakwenda kasi sana ndugu zangu
 
ilu

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
1,117

Kuna mambo mengi sisi tuliobaki yafaa kujifunza katika maisha ya mwendazake hasa kipindi chake cha urais. Mungu ni mkali sana. Kuna madiktekta wengi Afrika ila wamepata maisha marefu labda inawezekana wao hawalutaji sana jin la Mungu. Mwendazake alikuwa haishi kulitaja jina la Mungu ila matendo yalikuwa yanakataa utukufu wa Mungu.
 
Nazgur

JF-Expert Member
Apr 19, 2020
2,847
2,000
Kwa hiyo na wewe ni askofu?
Labda utakua askofu wa mashoga, kwa tabia zako za humu na yale matusi kisha ukawa askofu? Acha utani basi.

Na kama utakua askof basibuatakua ni
1 mwamakula
2 mpemba
3 bagonza
4
Pole sana kwa maumizvu yenu na faraja zenu kwa sasa, ila utawala ni ule ule
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom