Askofu Mwamakula: Polepole ametahadharisha tusipokuwa makini, Serikali inaweza 'kutekwa nyara' na kubaki kama 'mwanasesere'

Nimefurahi kuona Polepole akili zikimrudi

Pole pole hajawahi kuwa na akili tuh since then,tokea yupo kigoda Cha mwalim nyerere alipokawa anapiga domo kwa mgongo wa kina Mzee butiku had aliopoonwa na Magufuli na kufungwa mdomo hakuwahi kuwa na akili,

Hivi sasa kilichomrudia siyo akili,ni Njaa na mamlaka na audience....jitu la hovyo Sana
 
Na nyie mnaomlaumu sasa hivi nyamazeni bwana tuendelee kufaudu (kufaidi) vita ya kunguru......... hahahaha tamthilia inaendelea kuwa tamu sana hii............. Tutafutieni mwingine mropokaji ambaye akipokonywa tonge ataongeza safu ya Team Slowslow
 
Tena huyo Polepole mwambieni atulie tutamrarua hataamini Hawa ndio waliotumika kusema Lisu kajipiga risasi mwenyewe
Tundu lisu shida aliyo nayo ni kwamab dereva wake yuko hai sasa ni jinsi gani wataenenda sawa kwa upikaji data zao kuhusu shambulio lake kama wakilejea hapa tanzania.

Magufuli keshakufa lakini inakuwa vigumu kwa Tundu aludi vipi bila ya dereva wake?
Na kama tundu anaogopa kuuwawa je dereva amekimbia nini huku au nae anaogopa magufuli asiyekuwapo?

Shambulio la lisu analijua yeye na dereva wake na chama chake na ndio maana kashindwa kumleta dereva hapa tz.
Kama vipi amlete huyo dereva aje ahojie kisha arudi huko ili kila kitu kijulikane.
 
Tundu lisu shida aliyo nayo ni kwamab dereva wake yuko hai sasa ni jinsi gani wataenenda sawa kwa upikaji data zao kuhusu shambulio lake kama wakilejea hapa tanzania.

Magufuli keshakufa lakini inakuwa vigumu kwa Tundu aludi vipi bila ya dereva wake?
Na kama tundu anaogopa kuuwawa je dereva amekimbia nini huku au nae anaogopa magufuli asiyekuwapo?

Shambulio la lisu analijua yeye na dereva wake na chama chake na ndio maana kashindwa kumleta dereva hapa tz.
Kama vipi amlete huyo dereva aje ahojie kisha arudi huko ili kila kitu kijulikane.

kwa maana hiyo kama dereva wa lisu angekuwa amekufa uchunguzi usingefanyika? acha ushabiki maandazi wewe?
 
Humphrey Polepole ameanza kujenga taasisi huru ya fikra! Hahitaji kiwanja cha kujengea taasisi hiyo wala hahitaji Wajumbe wa Bodi wa kuendesha kwani kichwa chake ndio Bodi yenyewe. Ameanza kutoa mihadhara kuhusu mustakabali wa nchi. Anatahadharisha kuwa tusipokuwa makini, Serikali inaweza 'kutekwa nyara' na kubaki kama 'mwanasesere'! Kwamba 'kikundi cha wahuni' wanaweza kuiteka nyara ikawa inaendeshwa na hicho kikundi!

Hizo ndizo fikra huru zenyewe! Lakini Polepole anasahau kuwa hata yeye alipokuwa Mwenezi na Msemaji wa Chama kinachoongoza Serikali, kuna watu walikuwa wanasema kama yeye anavyosema sasa! Watu wale waliokuwa na fikra huru wakati akina Polepole wameshika hatamu walipigwa; waliteswa; walitekwa; walibambikiwa Kesi za uchochezi, uhujumu uchumi na utakatishaji Fedha. Sisi Askofu tuliokuwa tukiwapazia sauti na kuwatetea watu hao tuliandamwa na hata kukiona cha moto.

Mwelezeni Mheshimiwa Humphrey Polepole kuwa sisi Askofu tunamkaribisha katika ulimwengu ulio huru ambao hauna dola ya kukutetea badala yake dola ndio iliyo na uhuru wa kukufanya cho chote kile! Kwa ujumla, katika ulimwengu huu hatuna kinga ye yote dhidi ya dola haijalishi tuna hadhi gani katika jamii! Huku ukitoa tu mawazo yaliyo tofauti na ya watawala au hata watu walio karibu na watawala, basi wewe unalo.

Jamii yetu huku ni kama ya wale wezee walioambiwa wakati Polepole yupo katika hatamu kuwa 'watatwangwatwangwa' na yule aliyekuwa Mkuu wa Mkoa ule aliozaliwa Mukwavinyika! Huku katika ulimwengu huu ulio huru, unaweza kulazwa mahabusu hata kwa kutetea watu haijalishi kama wewe ni Askofu au Profesa! Huku, Jeshi la Polisi halifuatu hata kanuni na Sheria za kukamata watuhimiwa! Huku, Askofu anaweza kufuatwa hata alfajiri katika faragha akiwa chumbani. Mwambieni Polepole kuwa asiwe na wasiwasi kwani akianza kufinywa kwa kusema ukweli na kutetea haki za wengine, sisi Askofu tutakuwa tayari kumpazia sauti. Mwambieni aungane na Askofu kuhamasisha upatikanaji wa Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

Kuwa askofu si kwamba ndo una upeo mkubwa,ukimsikiliza na kumuamini polepole ni ujinga wa kiwango cha juu...

Askofu angejaribu kumfikiria polepole wa leo,wa Magufuli na yule wa katiba mpya atajua kuwa kumsikiliza polepole ni ujinga,angeacha tu wanasiasa wademke katika dimba lao,atadharaulika.
 
Hii kitu Inawezekana ikawa na ukweli. Polepole, Lissu na Ngurumo, wote wamekuja na similar statements.... Is it a coincidence.

South Africa story za STATE CAPTURE zilipoanza zilikuwa down played. Later ikaja kuwa wazi kuwa akina Gupta walikuwa ndiyo vinara..... Sasa Bongo kutokana na Polepole inaelekea ni kikundi ndani ya CCM.
Polepole anazungumzia kikundi gani? Sidhani nchi hii inaweza kuangukia mikono ya kikundi kibaya kuliko au hata kama kile kilichoishia March 2021. Kama kuna wakati nchi hii imepata kuongozwa na kikundi; tena kikundi cha watu wabaya sana ni baada ya uchaguzi 2015. Nchi ilikuwa mali ya mtu binafsi na kikundi kidogo chake kilichomsaidia kazi ya kuumiza, kuua na kurubuni wale wasiokubaliana nao. Polepole alikuwa meneja mradi wa ununuzi wanasiasa upinzani ambao hata hivyo ulishindwa kuua upinzani na kupelekea uchafuzi wa 2020. Shetani mkubwa huyu.
Polepole ni baadhi ya watu kwenye genge la Magufuli waliofanikisha siasa chafu kupata kutokea hapa nchini. Yeye anaamini chini ya utawala Magufuli serikali haikuwa kikundi, kwakuwa yeye alikuwa kwenye mlo.

Sasa hivi hayuko kwenye mlo, na yeye na wenzake waliokuwa kwenye genge la Magufuli wanaanza kutolewa kwenye mnyororo wa mlo, anaanza kupiga kelele.

Huyo Polepole inabidi avuliwe nyadhifa zote alizonazo, na akija huku mtaani ndio atavuna alichopanda. Na akiongea sana awekwe ndani ndio atajua ubaya hailipi.
 
Usimwamini mwanasiasa yoyote!

Ukishatolea kwenye nafasi yo yote ile ya kiuongozi akili ndiposa hurejea tena
Huyu keshasahau ya kwake alowatendea watanzania mpaka chama kutia fora kwa kuchagua wanaccm wote kwenye uchafuzi ulopita
Sijui anashauri nn wakati wake hakuyaona hayo ila leo yupo nje anayaona
Wacha tubatizwe wote
 
Hivi ni akina nani wale wanammwagia misifa kwenye comment za hizo video anazopost youtube?
Mbona humu idadi kubwa wanamponda?

Wale ni akina nani na humu ni akina nani?
 
1631623912544.png
Kuna majira huwa ana akili, kuna majira anakuwa kama kichaa kuna majira anakuwa kama ana busara na kuna majira anakuwa kama bendera
 
😂😂😂😂😂 sasa waambie MODS waliongeze liwe kama ubin wako lol!!!
Huo ni ubini wa huo Mkoa tajwa

Tazama

Mwanza - Rock City
Mbeya - Green City
Arusha - A Town
Iringa - Mukwavinyika
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Tumpuuze tuu huyo polepole sio msaada kwa taifa hili, Kama pindi akiwa kwenye system hakuweza kuona mabaya yaliyokuwa yakitendeka. Sahizi katupwa nje ndiyo anajifanya anaongea basi ni hasira tuu ya kuondolewa ndiyo inamsumbua. Angekaa kimya Kama alivyotulia bashiru, kupayuka kwake kipindi hiki anajiaibisha
 
Polepole jinga sana, pumbaf huyu, yeye akiwa Mwenezi katika Chama chetu, mbona alikuwa anapinga watu kusema wazi wazi na matukio ya ajabu ajabu ya serikali yalitendeka, watu kupotea, yeye Polepole alikuwa wapi? I wish ningekuwa Mh. Rais wangu, Mama Samia, natengua Ubunge wa Polepole haraka sana, na abaki tupu, huyu ana njaa mbaya sana huyu. Alafu haaminiki, ni mtu wa ku badilika badilika, wakati ule mchakato wa Katiba Mpya ya Warioba, Ndugu Polepole alikuwa mtetezi wa Katiba Mpya, baada ya kupata madaraka akabadilika kabisaaa, sasa hv anaona kaekwa kando, anaanza kelele, jinga sana huyu.
 
Kiongozi bora havumi kwa kiki ni matendo makuu pekee hudhirisha ubora wake
Kama kweli analihitaji kombe aje Pole pole
 
Kwa Polepole sio kwamba anaumia na wanachokutana nacho Watanzania bali ni njaa na tamaa ya kuwekwa mbali na mkate wa taifa
Nakubaliana na wewe maana Polepole wa Katiba mpya, na Polepole baada ya kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya na baadae katibu mwenezi, ni watu wawili tofauti. Na Polepole wa sasa ni tofauti na wale wawili wa mwanzo!
 
Back
Top Bottom