Askofu Mwamakula: Ni nani wa kuionya TBC kuacha upendeleo?

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,409
NI NANI WA KUIONYA TBC KUACHA UPENDELEO?!​

TBC inaongozwa na AYUBU RYOBA,huyu ni mhafidhina aliyegeuka kuwa mwimba kwaya.
ameharibu sana TBC na kimekuwa chombo cha chama badala ya UMMA.
Kumbuka amekuwa akimdanganya mkuu kwamba TBC hakuna matatizo na pia amekuwa akifanya ujanja ujanja ili JPM asifanye ziara pale TBC, na pia hasikilizi ushauri wa kitaalam hasa kwa watu wa procurement ,na wengineo.
SAFARI CHANNEL imepata vyombo vya kisasa kabisa kwa maagizo cha JPM lakini hii TBC ! hakuna kitu kabisa.

Watu wanalipa kodi! Kodi zao zinatumika kulipa gharama za uendeshaji wa TBC ikiwemo kuwalipa mishahara waandishi wa habari, wapiga picha na watangazaji wake! Sehemu ya hao walipa kodi wanasikika wakilalamika kuwa TBC wanapendelea CCM! Wanahoji kwa nini TBC inatangaza mubashara mikutano ya CCM lakini haiwezi kutangaza mubashara mikutano ya vyama vikuu vya Upinzani kikiwemo CHADEMA na ACT Wazalendo!

Ni wajibu wa Askofu kuwatuliza watu hawa wasikasirike na waendelee kuwa watulivu, lakini pia ni wajibu wa Askofu kuwakemea wenye mamlaka ya kuendesha, kusimamia na kuiagiza TBC kuwa vitendo hivyo vya upendeleo visipokoma vitaichafua nchi! Kwa sababu hiyo basi, tunawaonya Uongozi wa TBC na wale wote wenye mamlaka ya kuisimamia na kuiagiza TBC watambue kuwa hasira dhidi ya TBC huku uraiani kutoka sehemu ya Watanzania wasio wana CCM inazidi kujaa katika kikombe cha ghadhabu! Ni wajibu ya wenye mamlaka kulirekebisha hili mapema iwezekanavyo!

Mimi nimetimiza wajibu wangu kama Askofu (Ezekieli 33:1-20)

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki

From Askofu Mwamakula
 
Mnapo laumu mtuwekee na ushahidi Kama wanalipia lakin idara ya masoko inakataa au
 
Mnapo laumu mtuwekee na ushahidi Kama wanalipia lakin idara ya masoko inakataa au
Yani habari inalipiwa? Upo Tanzania?
Msiba wa Mkapa vyombo vililipia kurusha?
Majambazi wakikamatwa huwa wanalipia kuonyesha?
Mafuriko ya DAR JANGWANI vyombo vinapewa fedha vionyeshe?
MATAGA mna utapia mlo nyie
 
Wana Chadema hawana muda wa kuangalia TBC1 na kila mara wanasema hivyoo. Sasa, ya nini kurusha habari zinazowahusu?
 
Huyu askofu Mwamakula pamoja na yule Shoo bila kumsahau Bagonza wanajielewa sana hawa viongozi. Kwao nyeupe ni nyeupe na nyeusi ni nyeusi. Kuna wengine wanafiki wanangojea rais ajaye akiwa muislam ndio waanze kufungua mabakuli yao kumkosoa kosoa. Wanakwenda kuaibika mwaka huu.
 
Rioba alikua mkosoaji mzuri sana alipokua mwalimu lakini Sasa hawezi kuongea ana chakula mdomoni
 
Back
Top Bottom