Askofu Mwamakula: Mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan, mambo yafuatayo ni muhimu

1616163232030.jpeg
 
Kama alijijua kuwa Afya yake haiwezi mikiki ya ofisi hiyo kuu baada ya kaumaliza Ngewe yake ya miaka mitano angewaambia CCM kuwa imetosha

Sasa betrii kwenye Moyo na mikiki yote hiyo si kujitafutia kifo
 
Mshaurini mama kutumia sanitizer na kuvaa barakoa. ninaumia sana ninapomuona hajavaa barakoa na anasalimia watu. Au labda ni mimi tu nina shida ninii!!
 
Mpendwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan!

Kama nilivyoandika hapo awali, ninapenda kuchukua tena nafasi hii kutoa salaam zangu za pole kwako wewe binafsi kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. Hakika, hiki ni kipindi kigumu sana kwako wewe binafsi na kwa Tanzania kama Taifa na nchi.

Imenipasa katika kipindi hiki cha Maombolezo haya makubwa kushiriki katika kutoa maoni, maonyo na ushauri kuhusu mambo muhimu yaliyo na maslahi mapana kwa Taifa ambayo hayana budi kufanyika ili kuliweka Taifa pamoja. Ninaona ni muhimu haya kuyasema sasa wakati ambao pia nchi inajiandaa kupokea mabadiliko makubwa ya kiuongozi.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuanzia sasa wewe ndiye utakayekuwa Rais wa nchi kwa kipindi chote cha miaka minne na nusu iliyosalia. Ninaahidi kuendelea kukuombea wewe pamoja na Serikali yako katika jukumu hili zito.

Ni kwa sasabu hiyo, mimi Askofu Mwamakula, nisimamaye katika zamu yangu kama mtumishi wa Mungu katika zama hizi, ninao wajibu wa kukuangaliza mambo kadhaa lakini yaliyo ya muhimu ambayo itakupasa uyatafakari sana wakati huu unapoanza safari ya kuliongoza Taifa hili (Ezekieli 33:1-20)!

Ninapenda kukurejesha wewe pamoja na washauri wako katika tukio kama hili lililotukia miaka mingi iliyopita muda mfupi mara baada ya kifo cha Mfalme Sulemani ambapo mrithi wake alijikuta katika wakati mgumu kufuatia kukataa ushauri wa wazee na kufuata ushauri wa vijana wahuni. Tukio hilo limetunzwa vizuri kama kumbukumbu katika Biblia Takatifu katika Kitabu cha 1Wafalme 12:1-24 na Kitabu cha 2Mambo ya Nyakati 10:1-11:4.

Ni kwa sababu hiyo, mimi pamoja na wengine tunaona mambo yafuatayo ni ya muhimu sana kwa uongozi wako kuyarekebisha ili kuliunganisha Taifa lililogawanyika:

1. Tunashauri utawala mpya uondoe zuio la Vyama vya Siasa kufanya Siasa na hivyo mruhusu mikutano ya hadhara katika nchi nzima na mambo yote ya kisiasa yaliyoruhusiwa na Katiba ya Nchi.

2. Tunashauri utawala mpya uwaachie huru wafungwa wote wa kisiasa na kufuta kesi pamoja na kuwaachilia huru Mahabusu wote wanaoshikiliwa katika Mahabusu na Magereza zote nchini kwa tuhuma za kisiasa ambazo zimepewa majina ya uchochezi, uhujumu uchumi, utakatishaji fedha, madawa ya kulevya nk.

3. Tunashauri utawala mpya ujenge mazingira ya kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi ili Chaguzi ndogo zote (by-elections) zinazofuata pamoja na Uchaguzi Mkuu ujao visimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi.

4. Tunashauri utawala mpya usikilize maoni ya makundi mbalimbali nchini yanayodai Katiba Mpya na ujenge mazingira ya kuanza upya kwa mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya ili Uchaguzi Mkuu ujao ufanyike chini ya Katiba Mpya.

5. Tunashauri utawala mpya uachie Vyombo vya Habari kufanya kazi zao kwa Uhuru pasipo kuingiliwa na dola.

6. Tunashauri utawala mpya uanzishe mazungumzo na Vyama vya Upinzani nchini ili kufanya maridhiano kuhusu namna ya kufanya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao uliharibiwa mwaka 2019.

7. Tunashauri utawala mpya uangalie na kurekebisha mazingira ya wafanyabiashara na Taasisi mbalimbali nchini ikiwemo kuzifungua Akaunti zilizozuiliwa kwa sababu mbalimbali hasa ambazo mazingira ya kufungiwa kwazo yalikuwa na harufu za kisiasa.

8. Tunashauri utawala mpya uache kutumia Vyombo vya Dola hasa Jeshi la Polisi katika kuhujumu vyama vya Upinzani na makundi mbalimbali yanayotetea Haki nchini.

9. Ikiwa njia ya maridhiano, tunashauri utawala mpya ufungue milango ya mazungumzo na maridhiano kwa kutoa mwaaliko kwa wanasiasa, wanaharakati na Wafanyabiashara walio uhamishoni warudi nchini.

10. Tunashauri utawala mpya ufungue majadiliano na maridhiano na viongozi wa Vyama vya Upinzani kuhusu malalamiko yao kufuatia Uchaguzi Mkuu uliopita.

11. Tunashauri utawala mpya uwapandishe madaraja Watumishi wa umma wanaostahili pamoja na kuongeza mishahara kwa wafanyakazi wote.

Tunapenda kukuhakikishia kuwa sisi viongozi wa dini ambao tumejipambanua katika kutetea Haki na kusema kweli katika nchi hii tutatoa ushirikiano kwa utawala mpya kwa kila jema litakalofanywa kwa ajili ya kuweka upya na kuendeleza misingi ya Haki na Maridhiano katika nchi yetu.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfutate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania na Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani

View attachment 1729054
HAYA YOTE ULIYOANDIKA NI MAZURI ILA NGOJA WW UKIJA KUWA RAIS NDIO UTAYAFANYA ILA KWA SASA ENDELEA NA NJIA YA MSALABA ACHA KUPANGIA WATU KAZI ZA KUFANYA...
 
Aliji sacrifice kuwatumikia Watanzania maskini
View attachment 1729070
Alifanyaje ?! Kujisucrifice kwa kutoongeza mishahara ya watumishi na kuongeza makato ?

Kajisucrifice kwa kuiba kura ili atawale milele kama phar ao ?

Kajisucrifice kwa kupiga watu risasi kinyama mchana kweupe ?

Kajisucrifice kwa kupakazia watu kesi na kuwafunga kwa uonevu mf. Bendera

Kajisucrifice kwa kujijengea mahekalu na uwanja wa ndege kijijini kwake ?

Kajisucrifice kwa kudhulumu watu. Mf. Wakulima wa korosho.

Aise mkuu tafadhali sana mbona unatuonyesha damu afu unatuambia ni ya njano wakati sisi tunaona rangi nyekundu ?!!

Kajisucrifice kwa kutukana watu na kuwadhalilisha hadharani. Mf "bakini na mavi yenu nyumbani" "wakinamama mpanuliwe wapi"

Kajisucrifice kwa kuteka na kulazimisha makubaliano na wav. Mf. Mo

Kajisucrifice kwa kuua watu. Mf. Watu kuokotwa kwenye fukwe wakiwa kwenye viroba.

Kajisucrifice kwa kuahidi na kufurahia watu kuishi katika hali mbaya. Mf "mtaishi kama mashetani"

Kajisucrifice kwa kuwafukuza wadogo zetu chuo pale UDOM huku akiwaita "vilaza" mkuu umesahau au unajisahaulisha ?!

Kajisucrifice kwa kubomoa nyumba za watu kionevu bila fidia ?

mkuu tafadhali aise hivi are you serious ?! Huyo pharao alijisucrifice yeye au alisucrifice wananchi wake ?!
 
Kama alijijua kuwa Afya yake haiwezi mikiki ya ofisi hiyo kuu baada ya kaumaliza Ngwe yake ya miaka mitano angewaambia CCM kuwa imetosha
Sasa betrii kwenye Moyo na mikiki yote hiyo si kujitafutia kifo
Kumbe ndiyo maana alikua na hasira sana alikua akiona watu wanadunda alafu akiwaza yeye hana mda mrefu duniani alikua anakasirika sana yaani hasira za mgonjwa aliyekata tamaa. Ndo maana matukio yanayopelekea kuponya uhai wa watu alikua anapinga sana, tukianza na wale wanafunzi kule Arusha,tetemeko bukoba, njaa geita.
 
Kwa hii historia, Magufuli alirisk sana uhai wake kubeba jukumu la kuhudumia wananchi
Ni upendo
Huwezi kupoteza uhai wa mtu kisa eti unajenga madaraja.Ni kichaa na hayawani muuaji tu ndiyo anaweza fanya hivyo.Alichagua aache jina baya na kumbukumbu mbaya.

Hayo yote unaweza kuyafanya ktk amani na utulivu bila hata manung'uniko. Uongozi tu.

Aende na kila mtu atakufa. Na by the way siyo mm nimemuuwa.
 
Shi
Katiba inataka anaytakiwa kupewa jukumu la kuongoza katika nafasi hasa ya Urais anatakiwa awe na Afya njema!

CCM mlikosea mkaweka mtu mwenye historia ya ugonjwa toka muda mrefu.

Marehemu alishakiri kuwa yeye alikuwa anabipu akachukua fomu akasukumizwa huko moja kwa moja.

CCM mnastahili kulaumiwa katika jambo hili kwa sababu mlikuwa mnajua historia ya marehemu ila mlifanya kwa kukomoana, matokeo yake ndio haya.
Shida yote hii ni JK.
 
Askofu amesema yote, cha msingi ambacho mama anatakiwa kukiona mapema ni kuhusu viongozi almost wote waliofanya kazi na Hayati, wameonesha udhaifu mkubwa sana. Ni waongo wa wazi, wana dharau, wana viburi, ni wajeuri na wengi ni wasema hovyo, kwa ufupi hawana karama ya uongozi, labda wanafaa kuwa askari wanyamapori wakapambane na majangili, maana hakuna negotiation kati ya jangili na askari, au wakawe askari magereza napo nina wasiwasi kama hawatakandamiza haki za wafungwa.

Kingine ambacho binafsi nimekiona kuwa ni tatizo ni hili la vipngozi wanaopewa nafasi za kisiasa wanaotokana na TISS, hawa pia wameprove failure kubwa sana labda kwa sababu ya nature ya kazi yao, "kureport na kutekeleza order". Kiutendaji hiki kinawaathiri hawawezi kuwa wabunifu zaidi ya kusubiri "maelekezo kutoka juu" kama ambavyo walivyozoea wakiwa huko.

Si kwa ubaya, nachotaka kieleweke hapa ni kuwa kila kazi ina "culture" yake, na culture hiyo inaweza kumuathiri mhusika akitolewa katika majukumu yake ya awali na kupewa kofia ya kisiasa. Hawa wanafaa waendelee kupenyezwa tu kama ilivyo ada, ili kukusanya taarifa za sehemu husika na kuzipeleka zinakotakiwa, wakipewa VITI wanatuchelewesha kwakua wamezoea kuishi kwa kufungwa mikono.

Apumzike kwa amani mzee wetu JPM.
Hapa umenena vizuri TISS wanatakiwa wapenyezwe maeneo muhimu tu ili kutoa taarifa za kinachofanyika lakini kuwatumia kisiasa siyo jambo jema kwa taifa
 
Madame President ameanza kuonesha dalili nzuri za kulionganisha taifa na watu wake kuwa kitu kimoja, hata waliokua wakimpinga Marehemu Magufuli wameanza kuonesha dalili za kumuunga mkono Madame President. REF: Kigogo2014, Tundu Atipass Lissu, Askofu Mwamakula, Godbless Lema na wengine wapingaji katika mitandao kama JF/Twitter/Insta.

Nina amini, Madame President akitumia busara kama aliotumia Rais Hussein Mwinyi kuwaonganisha wazanzibari kuwa kitu kimoja licha ya itikadi zao za kichama na mengine, sambamba na kuto watetea viongozi na wasio na busara katika kazi zao (Viongozi wanao wachapa na kuwaonea raia kina Ole Sabaaya/Makonda/Cyprian Musiba, basi Madame atafaulu sana.

Muhimu, awakumbuke vijana wasio na ajira, wastaafu, wapinzani, waajiriwa wanao stahiki nyongeza ya mishahara na madaraja, wafanya biashara na waliofungwa kisiasa na visasi. Atafaulu katika utawala wake.
Nchi inaongozwa na wenye nchi ambao ni miongoni mwa wananchi ila hauwafahamu na inawezekana hujawahi kuwaona; wapo na wana nguvu kuzidi Rais na Katiba, je Wananchi nguvu yao iko wapi?

1. Marekani ni taifa lenye nguvu, Rais wake ana nguvu za ukomo, senata na magavana wa nguvu kwenye jimbo lakini maamuzi ya nani awe Rais na nchi iende mwelekeo upi iko kwenye mikono ya wachache;
2. Uingereza ni taifa la kistaarabu lakini liko chini ya utawala wa malkia/mfalme ambaye hachaguliwi na wananchi ila ni daraja fulani tu lililojitengeneza na kujihalilishia umiliki wa nafasi hiyo. Kiongozi wa kisiasa ijapokuwa anachaguliwa na wananchi lakini ni sharti awe ni mkristo tena dhehebu la Anglikana
3. Tanzania ni zao la nchi mbili huru zilizoungana na kuunda jina moja lenye kuitambulisha kimataifa. Viongozi wanachaguliwa na wananchi lakini kuna nguvu fulani iliyonyuma ya ngome kubwa ndio huchezesha kama karata ni nani awe kiongozi wapi na wakati gani. Mtu akilazimisha kwa kufuata amekidhi sifa zilizoanishwa kwenye katiba kwamba anatosha na wananchi wanaonekana kumuunga mkono juhudi hizo zinaweza kuishia kusikojulikana.

Wapambe wanapoteza viongozi bora wanajaa kiburi ambapo hatima yake wanazalisha chuki badala ya upendo na amani kisha wanasimamia haki na uhuru wa kila mmoja kwa mjibu wa sheria zilizopo.
1. Kusoma sana hakuzalishi kiongozi bora kama maarifa, hekima na busara havitatumika vyema
2. Kuwa mzungumzaji sana na mbishi sio sifa ya kuwa kiongozi bora kama wanaokusikiliza hauwaheshimu na kuwathamini
3. Kusafiri sana duniani na kufahamiana na watu wa aina nyingi tofauti sio kigezo cha mtu kuwa ni kiongozi bora ambaye atawawezesha anaotaka kuwaongoza wafanikiwe kama hataepuka majivuno, dharau, ugomvi, kiburi, chuki, mifarakano na visasi;

Kinachotakiwa kufanyika Tanzania sio katiba mpya au tume huru ya uchaguzi wa kisiasa isipokuwa ni DIRA na SERA BORA za kipekee za Taifa [The National Unique Vision, Direction and better Policies]
 
Mpendwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan!

Kama nilivyoandika hapo awali, ninapenda kuchukua tena nafasi hii kutoa salaam zangu za pole kwako wewe binafsi kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. Hakika, hiki ni kipindi kigumu sana kwako wewe binafsi na kwa Tanzania kama Taifa na nchi.

Imenipasa katika kipindi hiki cha Maombolezo haya makubwa kushiriki katika kutoa maoni, maonyo na ushauri kuhusu mambo muhimu yaliyo na maslahi mapana kwa Taifa ambayo hayana budi kufanyika ili kuliweka Taifa pamoja. Ninaona ni muhimu haya kuyasema sasa wakati ambao pia nchi inajiandaa kupokea mabadiliko makubwa ya kiuongozi.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuanzia sasa wewe ndiye utakayekuwa Rais wa nchi kwa kipindi chote cha miaka minne na nusu iliyosalia. Ninaahidi kuendelea kukuombea wewe pamoja na Serikali yako katika jukumu hili zito.

Ni kwa sasabu hiyo, mimi Askofu Mwamakula, nisimamaye katika zamu yangu kama mtumishi wa Mungu katika zama hizi, ninao wajibu wa kukuangaliza mambo kadhaa lakini yaliyo ya muhimu ambayo itakupasa uyatafakari sana wakati huu unapoanza safari ya kuliongoza Taifa hili (Ezekieli 33:1-20)!

Ninapenda kukurejesha wewe pamoja na washauri wako katika tukio kama hili lililotukia miaka mingi iliyopita muda mfupi mara baada ya kifo cha Mfalme Sulemani ambapo mrithi wake alijikuta katika wakati mgumu kufuatia kukataa ushauri wa wazee na kufuata ushauri wa vijana wahuni. Tukio hilo limetunzwa vizuri kama kumbukumbu katika Biblia Takatifu katika Kitabu cha 1Wafalme 12:1-24 na Kitabu cha 2Mambo ya Nyakati 10:1-11:4.

Ni kwa sababu hiyo, mimi pamoja na wengine tunaona mambo yafuatayo ni ya muhimu sana kwa uongozi wako kuyarekebisha ili kuliunganisha Taifa lililogawanyika:

1. Tunashauri utawala mpya uondoe zuio la Vyama vya Siasa kufanya Siasa na hivyo mruhusu mikutano ya hadhara katika nchi nzima na mambo yote ya kisiasa yaliyoruhusiwa na Katiba ya Nchi.

2. Tunashauri utawala mpya uwaachie huru wafungwa wote wa kisiasa na kufuta kesi pamoja na kuwaachilia huru Mahabusu wote wanaoshikiliwa katika Mahabusu na Magereza zote nchini kwa tuhuma za kisiasa ambazo zimepewa majina ya uchochezi, uhujumu uchumi, utakatishaji fedha, madawa ya kulevya nk.

3. Tunashauri utawala mpya ujenge mazingira ya kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi ili Chaguzi ndogo zote (by-elections) zinazofuata pamoja na Uchaguzi Mkuu ujao visimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi.

4. Tunashauri utawala mpya usikilize maoni ya makundi mbalimbali nchini yanayodai Katiba Mpya na ujenge mazingira ya kuanza upya kwa mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya ili Uchaguzi Mkuu ujao ufanyike chini ya Katiba Mpya.

5. Tunashauri utawala mpya uachie Vyombo vya Habari kufanya kazi zao kwa Uhuru pasipo kuingiliwa na dola.

6. Tunashauri utawala mpya uanzishe mazungumzo na Vyama vya Upinzani nchini ili kufanya maridhiano kuhusu namna ya kufanya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao uliharibiwa mwaka 2019.

7. Tunashauri utawala mpya uangalie na kurekebisha mazingira ya wafanyabiashara na Taasisi mbalimbali nchini ikiwemo kuzifungua Akaunti zilizozuiliwa kwa sababu mbalimbali hasa ambazo mazingira ya kufungiwa kwazo yalikuwa na harufu za kisiasa.

8. Tunashauri utawala mpya uache kutumia Vyombo vya Dola hasa Jeshi la Polisi katika kuhujumu vyama vya Upinzani na makundi mbalimbali yanayotetea Haki nchini.

9. Ikiwa njia ya maridhiano, tunashauri utawala mpya ufungue milango ya mazungumzo na maridhiano kwa kutoa mwaaliko kwa wanasiasa, wanaharakati na Wafanyabiashara walio uhamishoni warudi nchini.

10. Tunashauri utawala mpya ufungue majadiliano na maridhiano na viongozi wa Vyama vya Upinzani kuhusu malalamiko yao kufuatia Uchaguzi Mkuu uliopita.

11. Tunashauri utawala mpya uwapandishe madaraja Watumishi wa umma wanaostahili pamoja na kuongeza mishahara kwa wafanyakazi wote.

Tunapenda kukuhakikishia kuwa sisi viongozi wa dini ambao tumejipambanua katika kutetea Haki na kusema kweli katika nchi hii tutatoa ushirikiano kwa utawala mpya kwa kila jema litakalofanywa kwa ajili ya kuweka upya na kuendeleza misingi ya Haki na Maridhiano katika nchi yetu.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfutate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania na Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani

View attachment 1729054
Ameen
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
"Alipoingia yerusalemu walimwita mbarikiwa...alipofika Golgotha wakasema asulubiwe"
Sauti ya Bahati Bukuku
 
Back
Top Bottom