Askofu Mwamakula: Mamlaka zinazominya haki na Demokrasia

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,009
Mamlaka zote duniani zinazofinya haki, uhuru wa kujieleza, uhuru wa kujumuika, demokrasia, nk hufanya mambo yanayofana kama vile: kutumia Majeshi na Idara za Usalama kuwadhibiti, kuwatisha na hata kuwatesa wapinzani, wakosoaji na watetezi wa haki; kutumia Idara za Usalama na pesa katika kudhoofisha upinzani kwa kuugawa na hata kuwanunua baadhi ya viongozi wenye ushawishi na ikishindikana, basi kuwaua baadhi kwa njia mbalimbali; kutumia Vyombo vya Habari katika kujisafisha mbele ya umma kwa kupamba Sera za Serikali, na kuwasifia viongozi, nk;

Pia, hulitumia Bunge katika kutunga sheria za kukandamiza upinzani na kuwalinda watawala; hutumia Mahakama kuwahukumu wapinzani, wakosoaji na wanaharakati kupitia kesi za 'uchochezi', 'uhaini', nk; huondoa uhuru wa taasisi muhimu kama vile Tume za Uchaguzi, Mahakama, Bunge, Vyombo vya Habari, nk na kuviweka chini ya udhibiti wa Serikali; hudhibiti taasisi za dini kwa kuhakikisha kuwa viongozi wa taasisi hizo wanakuwa ni wale wanaounga mkono watawala; hufanya chaguzi bandia ili kuudanganya ulimwengu kuwa kuna demokrasia; huunda vyama bandia vya upinzani ili kuudanganya ulimwengu ambapo viongozi wa vyama hivyo huwa sehemu ya mfumo; hutumia nguvu kubwa katika kuvidhibiti vyama vya upinzani vinavyoonyesha upinzani wa dhati kwa kuhakikisha kuwa havipati fursa ya kutumia vyombo vya habari, kueneza sera, kufanya mikutano na maandamano, nk.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
 
Yote yaliyoandikwa ndiyo yanayotokea Tanzania awamu hii ya tano.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Waumini wa Kanisa la Moravian wanamfahamu huyo Jamaa, kiukweli alitimuliwa Moravian kwasababu ya kugombanisha/ kufarakanisha waumini. Msishangae aliungana na Wafarakanishaji na Wasaliti wenzake.
Huyo Tulimzika kisiasa pamoja na Tototundu na shekhe mrundi wake tarehe 28/10/2020
 
...hudhibiti taasisi za dini kwa kuhakikisha kuwa viongozi wa taasisi hizo wanakuwa ni wale wanaounga mkono watawala; hufanya chaguzi bandia ili kuudanganya ulimwengu kuwa kuna demokrasia;
Kipindi hiki sijasikia zile nyimbo za:
"....huyu ni chaguo la Mungu"
Au wanahofia kuonekana waongo na kupoteza waumini?
 
Waumini wa Kanisa la Moravian wanamfahamu huyo Jamaa, kiukweli alitimuliwa Moravian kwasababu ya kugombanisha/ kufarakanisha waumini. Msishangae aliungana na Wafarakanishaji na Wasaliti wenzake.
Kwa andiko hilo Askofu amemfarakanisha nani kama siyo kuelezea kile anachokiamini?

Mwanakondoo ameshinda. Tumfuate
 
Inamaana bila feni ndio parapanda italia?
Parapanda ikilia watoto wetu watajazwa uwanja wa Taifa, maana wananchi watakao kwenda ni wachache sana. Ningekua na pesa ningepeleka wanangu International Schoo of Tanganyika. Hizi shule za kata hizi ndiyo wanafunzi wanajazwa uwanja wa taifa.
 
Askofu Bangoza na askofu Mwamakula Nawakubali sana hawa watu, wanafanya kazi nzuri sana ya kufundisha, kukemea, kuonya, nakuelekeza. Kwenye timu ya kusifu hawapo wanausema ukweli na ukweli ndio utakao liponya taifa hili. Kiongozi wa kiroho WA ukweli lazima awe na uwezo wa kukemea matendo maovu bila kujali nani ametenda.

Hata mfalme Daudi alivyochukua mke wa mtu alionya na kuadhibiwa herode vivyo hivyo, Viongozi wengi wa dini wanaogopa kukemea serikali mana wataanza kuojiwa kuusu mapato na matumizi ya madhehebu yao.

Kama vile watoto wa Nuhu walivyochukua shuka wakafunika uchi wa baba yao, hebu na sisi tuchukue shuka turudi kinyumenyume tufunike uchi wa viongozi wetu wa kidini.
 
Back
Top Bottom