Askofu Munga: Hivi Ndugai toka moyoni mwako ulikuwa hujui Lissu aliko? Moyo wako hauna huruma na upendo?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,867
Ameandika baba Askofu Dr.Steven Munga (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,

__________________

Ndugu Spika, hivi ni kweli ya moyoni mwako kuwa ulikuwa hujui Mhe.Lissu aliko? Kama moyo hauna huruma na upendo, hata sheria nzuri zitatafsiriwa vibaya. BWANA uturehemu"

SHARE Zaidi uwezavyo ujumbe ufike
 
Hawa maaskofu wa KKKT baadhi yao mmmhhhh....
 
Yeye katumia zaidi ya Bl 27 fedha za walipakodi wa Nchi hii, Lissu kamzuia kutumia hata kumi kwa kigezo cha blah..blah..blah..utaratibu sijui..!!

Hata kumnyang'anya ubunge ni mwendelezo wa kuhakikisha anakosa hata fedha za kujikim huko hospital... Roho hizi hata Shetani hana..!! Kama kweli Karma ipo na ina-works basi naisubiri kwa hamu kwa huyu mzee.

BACK TANGANYIKA
 
..acha hilo la kudai hajui alipo.

..lile la kukataa kumpeleka TL Nairobi, huku hana fahamu, risasi ziko maeneo mbalimbali ya mwili, anavuja damu, na yuko ktk hatari ya kukata roho, ilikuwa jambo ktk historia ya Maspika wote wa Tz.
Mkuu JokaKuu, nadhani Ndugai kama aliona hali hiyo ya Lissu ambayo nilishuhudia hata Mbowe akiisema hadi machozi yanalenga akikumbuka na bado Ndugai kakosa moyo wa huruma anaweza kuwa Spika katili zaidi duniani kwa wakati huu tulio nao.
 
..CHUKI imeanzishwa na CCM.

..wao hawathamini kabisa utu, uhai, au maisha, ndugu zao walioko upande wa vyama mbadala.

..maamuzi aliyoyafanya Spika Ndugai ya kukataa kumpeleka TL Nairobi kwangu mimi ni mabaya kuliko uamuzi wa kumfuta ubunge.
 
Ndugai kwa nafasi yake kama Spika, naona hajiamini, hivyo anafanya kila awezavyo kuitetea nafasi yake hiyo katika bunge lijalo kwa kujaribu kumfurahisha Mkulu. Si kwamba hatambui TL alipo, bali pengine anaijua chuki ya JPM dhidi ya TL, hivyo ameamua ku "side" naye kimkakati. Uwepo wa Dr. Tulia chini yake unamkumbusha jinamizi la enzi za Spika Sita na Naibu wake Makinda.
 
46 Reactions
Reply
Back
Top Bottom