Askofu Mokiwa: Migogoro Anglikana ni ya kupandikizwa

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Mokiwa.jpg

Askofu Mkuu Kanisa la Anglican Dayosisi ya Dar es Salaam, Valentino Mokiwa​

Askofu Mkuu Kanisa la Anglican Dayosisi ya Dar es Salaam, Valentino Mokiwa, amesema migogoro mingi inayotokea katika kanisa hilo ni ya kutengenezwa jambo linalowavunja mioyo waumini.

“Kanisa ndilo kimbilio la waumini wenye shida mbalimbali, sasa kukiwa na migogoro waumini watamkimbilia nani?” alisema

Dk Mokiwa alizungumza hayo jana na waandishi wa habari wakati akitoa ufafanuzi wa mgogoro ulioibuka hivi karibuni ambapo Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglican nchini, Jacob Chimeledya alimtaka Dk Mokiwa ajiuzulu.

Askofu Chimeledya alimtaka Askofu Mokiwa ajiuzulu kwa kile alichodai kuwa anatumia madaraka yake vibaya na ubadhirifu wa fedha.

Hata hivyo, katika kikao chake na wanahabari leo asubuhi, Askofu Mokiwa alikanusha na kudai kuwa migogoro hiyo inapandikizwa na maadui zake.

CHANZO: Mwananchi
 
Mokiwa kakosea sana tena sana kusema eti hawezi kujiuzulu!

Kwa vile zilishakuja tuhuma tena kutoka kwa viongozi wenzake ambao nao ni wa kiroho angekaa pembeni tu ili waliomtuhumu kama ni uongo basi ingejulikana baadae. Hapa tutoe mfano wa mke wa Kaisari kwamba tuhuma pekee!

Kuna story moja kuhusu uongozi wa dini ambapo alitokea mtu mmoja tena kwenye 'inner cycle' akidai yeye ndio kiongozi halali huku akimtuhumu aliyekuwepo kuwa sio. Baada ya huyu aliyetuhumiwa kuona hivyo wala hakuanza kubishana au kutoa maelezo bali alichukua maamuzi tofauti. Aliamua kuondoka machoni pa waumini na kwenda kuishi mbali kabisa (remote areas) na wale watu wa kule matokeo yake wakashtukia uwezo wake mkubwa wa kiroho na kuanza kumfuata. Sasa huyu aliyejidai ndiye kiongozi huku nyuma kila kitu kikamharibikia na kukwama na baada ya miaka kama miwili ikabidi waumini waweke mkakati wa kumfuatilia yule wa kwanza na kumshawishi arejee ili kuwanusuru.
Na hapo ndipo ilijulikana ni nani kiongozi wa kweli na muongo.

Nimetoa hadithi hii muhimu kama kipimo kizuri kwenye maongozi ya Imani, haya ya kukataa kujiuzuru, na kusemana kwenye media hayahakisi sifa za kiroho. Pia askofu mzima kuongelea eti katiba ya Kanisa ni aibu kubwa maana katiba kubwa kabisa ya Wakristo ni Biblia na Biblia inafundisha sifa za kiroho ambazo ni unyenyekevu kwa yeyote hata aliyekuudhi, kujishusha nk.

Mokiwa akipitia hapa naomba ani PM nimpe ushauri zaidi kumuondolea aibu.
 
Bishop Mokiwa amekuwa kwenye mgogoro mkubwa na waumini na viongozi wa Kanisa la Anglican Tanzania kwa muda mrefu.

Mgogoro huu ni wa muda mrefu sana ila umekuwa wa kimya kimya na hii ni kwasababu wengi walikuwa wana msitiri kwasababu ya kumlindia heshima yake kwenye jamii.

Issue kubwa hapa ni ya UBADHIRIFU na MATUMIZI MABAYA ya mali za Kanisa.

Mtu mmoja ambae ni muumini alipata kuniambia Mokiwa ni kama "kupe ".

Ana mali nyingi na utajiri mkubwa hivyo kwamba hauwezi kuamini ni Askofu.

Mambo ya Mokiwa ni makubwa sana.
 
Hapa naona sehemu zote mbili kuna shida kwani swala la Kiongozi mkubwa wa kiroho tena ngazi ya juu inatakiwa kwanza kufanya mazungumzo na mhusika mwenyewe akubali kwa moyo wa dhati ndipo itengenezwe lugha ya kuwa tangazia waumini na kwa kuheshimu wadhifa wake haipendezi kutaja sababu za kijihuzulu kwake bali inatosha tu kusema anastaafu majukumu ya kikanisa.
 
Mkuu ataaaibikaaaa vibayaa janaanilikuwaa Bahamas wamachokwendaa kufanyaaa hadifamiliaa itashtukaa
 
DK JACOB

AMETOA AIKUKADHAA AAIPOJIUZULU AMETANGAZA KUWEKAA HADHARANI DOCS ZOTE ZINAZOMHUSU KTK UBADHIRIFU NAAMEOMBWA ASILALAMIKIWE NAMTU N KTK KULINDA KANISA LA BWANA

NAJIULIZA ANASUBIRI NINIAIAVIMWAGE
 
Hapa naona sehemu zote mbili kuna shida kwani swala la Kiongozi mkubwa wa kiroho tena ngazi ya juu inatakiwa kwanza kufanya mazungumzo na mhusika mwenyewe akubali kwa moyo wa dhati ndipo itengenezwe lugha ya kuwa tangazia waumini na kwa kuheshimu wadhifa wake haipendezi kutaja sababu za kijihuzulu kwake bali inatosha tu kusema anastaafu majukumu ya kikanisa.
Kutotaja sababu sio kiroho, kutaja sababu ndio kiroho. Katika Biblia mambo yalikuwa yanawekwa peupe tu!
 
Bishop Mokiwa amekuwa kwenye mgogoro mkubwa na waumini na viongozi wa Kanisa la Anglican Tanzania kwa muda mrefu.

Mgogoro huu ni wa muda mrefu sana ila umekuwa wa kimya kimya na hii ni kwasababu wengi walikuwa wana msitiri kwasababu ya kumlindia heshima yake kwenye jamii.

Issue kubwa hapa ni ya UBADHIRIFU na MATUMIZI MABAYA ya mali za Kanisa.

Mtu mmoja ambae ni muumini alipata kuniambia Mokiwa ni kama "kupe ".

Ana mali nyingi na utajiri mkubwa hivyo kwamba hauwezi kuamini ni Askofu.

Mambo ya Mokiwa ni makubwa sana.
Binafsi sioni sababu ya Mokiwa kung'ang'ania uaskofu kutokana na mambo yake yalivyo, angetii mamlaka kama katiba ya kanisa hilo inavyoelekeza. Kimsingi, ameamua kuliingiza kanisa katika mgogoro ambao sio wa lazima. Na hiki ni kipimo kwake kama kweli anampenda Yesu ama la! Nimefuatilia hoja zake sijashawishika nazo maana anawalaumu wanasheria wakati tuhuma zake ziko wazi!
 
Back
Top Bottom