Askofu Mokiwa aibua sifa za Rais ajaye

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
588
1,698

Mokiwa-01June2015.jpg
Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk. Valentino Mokiwa.
Wakati mchakato wa watangaza nia ya kuwania urais ukiendelea nchini, Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk. Valentino Mokiwa, ametaja sifa anazopaswa kuwa nazo rais ajaye.

Dk. Mokiwa ambaye aliwahi kuwa mkuu wa kanisa hilo, alitaja sifa hizo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya miaka 50 ya dayosisi hiyo yanayotarajia kufanyika Julai 5, mwaka huu pamoja na mafanikio mbalimbali yaliyopatikana ikiwamo elimu, afya na huduma za jamii.

Askofu Mokiwa alisema kiongozi anayetaka kuiongoza nchi anapaswa kufahamu changamoto kubwa ambazo zinalikabili taifa na namna ya kupambana nazo.

"Wote waliotangaza nia na wengine wanaotarajia kutangaza wana sifa hizo, nawapongeza na kuwatakia heri, hata mimi ningeweza kutangaza nia kama urais usingekuwa ni majukumu makubwa, lakini kiongozi anayetaka kuliongoza Taifa hili anapaswa kuweka vipaumbele muhimu kuwa suala la kwanza kwa Watanzania kuliko sura yake," alisema Askofu Mokiwa.

UMASKINI
Alitaja changamoto ya kwanza ambayo Rais ajaye anapaswa aifanye kuwa kipaumbele chake ni tatizo la umaskini uliokithiri.

Alisema umasikini umesababisha kuenea kwa magonjwa makubwa kama virusi vya ukumwi na kuua watu wengi, watu kuchomwa moto pamoja na kugombanisha majirani.

"Umaskini unaumiza watu, unaniumiza mimi, unasababisha maradhi, hatutaki rais atakayekuja na kipaumbele chake na kuacha kipambele hiki ambacho kinawaumiza watu wengi," alisema.

RASILIMALI
Changomoto nyingine aliitaja kuwa ni rasilimali za taifa kama gesi na madini ambayo rais ajaye anapaswa kuitatua na kuifanya kipaumbele chake.

Askofu Mokiwa alisema rais ajaye anapaswa kutumia rasilimali za nchi kushusha ukali wa maisha na siyo kugawa rasilimali za taifa kwa nchi nyingine au watu wachache.

KUBORESHA MAISHA YA WATUMISHI
"Changamoto ya kukimbiwa na wataalamu wetu kutokana na kutolipwa vizuri kukimbilia mataifa mengine kutoa huduma, lakini kumbe tunaweza kuboresha maisha yao na kusababisha kubaki nchini na wengine kuja," alisema.

Alifafanua kuwa rais ajaye anatakiwa kutambua changamoto hiyo ambayo kama ikimalizika uwezekano wa wataalamu kutoka mataifa mengine kuja nchini upo.

"Natamani siku moja nione shule za kata zinafundishwa na walimu kutoka mataifa mbalimbali, kama tunavyoshuhudia wataalamu wetu wakiwa katika mataifa mengine," alisema Askofu Mokiwa.

Aliseman rais ajaye anapaswa afahamu na kuona kuwa bajeti ya serikali inaboresha masuala ya elimu kwa kulipa vyema watumishi.

SAYANSI, TEKNOLOJIA

Alisema Rais ajaye anapaswa kufahamu kuwa ukuaji wa sayansi na teknolojia ambayo Watanzania ni wanufaikaji, inahitaji kuwa na wataalumu na wabunifu wa mambo mbalimbali kutoka nchini.

Askofu Mokiwa alieleza kuwa rais anapaswa kufahamu kuwa kupata wazalishaji na wabunifu ni kuongeza idadi kubwa ya wageni kuja nchini kuchukua ujuzi badala ya kutegemea wabunifu kutoka nje.

ULINZI WA TAIFA NA MIPAKA
Askofu Mokiwa alibainisha kuwa rais ajaye anatakiwa kulinda mipaka ya taifa ili kuboresha usalama wa nchi na Watanzania.

"Mtanzania anapaswa kuwa huru, tofauti na sasa unahofia kusafiri kutokana na kushamiri kwa wimbi la majambazi wanaoingia nchini kwa njia ya makontena, hivyo rais ajaye atambue kulinda na kuimarisha mipaka ya nchi," alisema.

MIGOGORO YA KISASA

Kuhusu migogoro ya kisiasa, Askofu Mokiwa alisema ni chanzo cha uvunjifu wa amani kutokana na tamaa za madaraka miongoni mwa wanasiasa ndani ya vyama ambayo inatokana na nguvu ya fedha walizonazo.

"Kwa sasa tuko kwenye kipindi ambacho vyama vya siasa vitaanza kutumia vijana kupambana badala ya kutumia ajenda ya ajira kwa vijana," alisema.

UBORA WA MATIBABU
Askofu Mokiwa alisema anasikitishwa na kitendo cha mawaziri na viongozi wakubwa wa nchi kwenda kupata matibabu nje ya nchi kwa magonjwa ambayo yanaweza kutibika nchini.

Alisema ni vyema rais ajaye akatambua kuwa Watanzania wanahitaji usawa katika matibabu.
Alisema changamoto kwake iwe ni kuleta madaktari kutoka mataifa mengine ili watoe matibabu nchini kwa usawa.

"Kiongozi ajaye aondokane na suala hilo la kukosekana kwa madaktari wenye sifa kwani viongozi wakubwa kutibiwa nje ya nchi ni kuwatukana madakari wetu," alisema.

HAKI ZA WATANZANIA
Askofu Mokiwa alisema masuala ya elimu, afya, maji na mahitaji muhimu ni mambo ambayo ni haki ya Watanzania hivyo hayapaswi kuwa vipaumbele vya wagombea.

"Wagombea waje na vitu ambavyo ni vya maana na siyo mambo ambayo ni haki ya Watanzania, kuyafanya kuwa hoja ya kutaka kuwa rais wa nchi," alisema.

KATIBA MPYA
Askofu Mokiwa alisema suala la Katiba mpya kiongozi ajaye anapaswa kuangalia hasa vipengele ambayo vimeingizwa visivyo na maslahi kwa Watanzania na nchi ili viondolewe kwa ajili ya usalama wa Taifa.

"Nitapenda kila anayetaka kuchukua fomu awe na mzingo wa Watanzania kichwani kwake na furaha ya Watanzania ndio iwe furaha yake na siyo vinginevyo," alisema Askofu Mokiwa.

Alisema pia anatamani kukaa na wagombea wote ili kuwapa maswali magumu ambayo yataleta mstakabali wa Taifa.

UANDIKISHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA

Akizungumzia uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura, alisema mashine za kuandikisha ziongezwe pamoja na siku za kuandikisha zisiwe na kikomo.

Alisema ni vyema Watanzania wakaendelea kujiandisha kutokana na watu kuongezeka pamoja na kufikia sifa za kujiandikisha kila mara.

"Tukiweka kikomo cha kuandikisha Watanzania kwenye daftari la wapiga kura ni kuwanyima haki yao ya msingi ya kupiga kura. Kila mwezi, siku watu wanatimiza vigezo hivyo daftari liachwe ili kila mara watu wajiandikishe," alisema.

MIAKA 50 YA DAYOSISI
Askofu Mokiwa alisema Dayosisi hiyo inatimiza miaka 50 ya tangu kuanzishwa kwake Julai 10, mwaka 1965.

Alisema kanisa hilo linajivunia mafaniko makubwa ya huduma za jamii, kama elimu, afya, maji na mahitaji muhimu kwa majirani wanaowazunguka, yatima na wasio na uwezo.

"Kwa kuazimisha miaka hii 50 tutafanya sherehe Julai 5, tukiwa na malengo yale yale ya kuboresha, kudumisha na kujali jamii inayotuzunguka katika kutoa huduma muhimu kwa kutumia wahisani wengi na makanisa ya Anglikana ndani na nje ya nchi," alisema Askofu Mokiwa.

CHANZO: NIPASHE
 
Ogeza la Ushoga
 
Huyu naye ni mnafki kama wanafki wengine tu nakumbuka kuna harambee alialikwa lowassa akasema anaomba Lowassa aje kuwa Rais wa nchi ili azirudishe shule za Agrican zilizochukuliwa na Serikali.

MWAKA HATUSIKILIZI VIONGOZI WA DINI TUMEGUNDUA WOTE MNAONGOZWA NA NJAA TU
 
Anawaza kwa kutumia tumbo,Tanzania kwasasa tuna matatizo makuu mawili ufisadi na rushwa ndo yazungumziwe kwanza hayo
 
Back
Top Bottom