Askofu Mkuu KKKT auchambua utawala wa Rais Magufuli

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Frederick Shoo, amesema kasi ya Rais John Magufuli, ya kutumbua majipu inaridhisha na amemtaka akaze kamba kwani watanzania wako nyuma yake.

Aidha, Askofu Shoo amewasihi viongozi wenzake wa dini na madhehebu tofauti kuungana kumuombea Rais Magufuli ili kumnusuru na jambo baya kwasababu kazi anayofanya ni ngumu na inahitaji maombi.

Aliyasema hayo jana wakati akifanya mahojiano maalumu na gazeti hili kuhusu siku 80 za Rais Magufuli Ikulu.

Kwa tathmini ya Askofu Shoo, Magufuli ameonyesha uongozi mzuri na ushupavu, na ni kiongozi anayepaswa kuigwa na marais wengine duniani. Alisema anafurahishwa na kasi ya utendaji kazi ya Rais kwasababu ndani ya muda mfupi ameonyesha umahiri kwa kuokoa mabilioni ya fedha zilizokuwa zikitafunwa na "wezi".

Askofu Shoo alisema kazi ya Rais Magufuli inatia moyo kwa taifa na kanisa kwa ujumla, hivyo alimuasa aendelee na kasi hiyo kuibua ufisadi ambao ulikuwa ukisababisha kupotea kwa mabilioni.

Alisema wakati wa uongozi wa Hayati Mwalimu Julias Nyerere, uchumi ulikuwa imara na nchi ilikuwa ikijiendesha kwa rasilimali zilizoko, lakini baada ya kupita utawala wake mambo yamekuwa tofauti.

Alisema haijawahi kutokea katika historia ya nchi kwa kiongozi mkakamavu kama Magufuli kujitoa kwa maslahi ya taifa kwa kufichua wezi na kuwafukuza kazi kwani kwenye serikali zilizopita hawakuguswa.

“Labda niseme tu inawezekana Mungu amemwonyesha njia mtumishi wake Magufuli, kwa makusudi ili afichue mambo ambayo yakiboreshwa na kusimamiwa yataweza kuibadilisha nchi na kuwa miongoni mwa nchi za kuigwa kupitia ukuaji wa uchumi,” alisema Askofu Shoo.

Alisema anatarajia kutoa tamko lake mwanzoni mwa wiki ijayo kuhusu utendaji kazi wa Magufuli katika hatua za mwanzo za utawala wake, na kuwasihi viongozi wa dini mbalimbali kuungana katika maombi ili kumnusuru na jambo baya dhidi yake.

Alipoingia tu madarakani, Magufuli alisababisha mtikisiko mkubwa ndani ya Mamlaka ya Bandari (TPA) na kwenye Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya kubaini mianya ya ukwepaji wa kodi hivyo kulazimika kuchukua hatua kali ikiwemo kuwasimamisha kazi vigogo kadhaa wa mamlaka hizo mbili.


Chanzo:
Gazeti la Nipashe
 
Hawa the so called maaskofu should shut their mouth. Hatujasahau ya Chaguo la Mungu ya Kilaini. Tell them to shut their mouth
 
...

The facts are plain to see.

Especially when the bishop lies plainly!!

Wakati upi wa Nyerere uchumi ulikua imara? Tulidanganywa na hakukua na uhuru wa watu kusema yanayokera.

In fact, uchumi ulikua unaanguka tu mpaka alipoona hawezi tena kuvimba nao akawa muungwana kung'atuka.
 
Hawa the so called maaskofu should shut their mouth. Hatujasahau ya Chaguo la Mungu ya Kilaini. Tell them to shut their mouth
Kwa nini usianze wewe!

You have to show the way!

Wewe unataka maaskofu wafunge midomo wakati wewe hutaki kufunga mdomo wako! Hizi ni fikra za kidikteta!
 
Siasa ndo maisha tunayoyaishi kaka kila unapolala maisha yako yote yanaongozwa na siasa.Sasa nitashangaa wewe unapostaajabu kwanini hawa wanafalsa wanajiingiza kwenye masuala ya siasa,kwani wao wanaishi ktk sayari ipi?Navyojua mimi siasa safi na makini na kiongozi madhubuti ndiyo chanzo cha uchumi imara ktk nchi yoyote ile duniani kote.
 
Siasa ndo maisha tunayoyaishi kaka kila unapolala maisha yako yote yanaongozwa na siasa.Sasa nitashangaa wewe unapostaajabu kwanini hawa wanafalsa wanajiingiza kwenye masuala ya siasa,kwani wao wanaishi ktk sayari ipi?Navyojua mimi siasa safi na makini na kiongozi madhubuti ndiyo chanzo cha uchumi imara ktk nchi yoyote ile duniani kote.

Mnafiki mkumbushe tuzo LA lowasa uliyemjibu alipongeza sana
 
Back
Top Bottom