Askofu Mkuu J. Lebulu Wa Arusha - Polisi arusha walitumia nguvu kubwa kuua inzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu Mkuu J. Lebulu Wa Arusha - Polisi arusha walitumia nguvu kubwa kuua inzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jan 8, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Maaskofu licha ya kulaani nguvu kubwa iliyotumika na polisi arusha, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Arusha Joseph Lebulu amesema Polisi walitumia nguvu kubwa kuua inzi, ni usemi wa kifasafa kwa wanaojaribu kuutafakari vizuri.

  Source: Habari leo newspaper
   
 2. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kauli ya Maaskofu kudai hawamtambui meya wa Arusha ni kauli ya kichochezi na kanisa kuacha kazi yake ya kuchunga kondoo na badala yake kuingilia kazi za siasa!!
  Imekuaje leo Maaskofu wanakurupuka na kutoa tamko la kisiasa na hali kazi yao ni kuhubiri makanisani? nani kawatuma?

  Huko nyuma wakati wa utawala wa Benjamin Mkapa walipouliwa watanzania 27 Zanzibar na mauaji ya mwembechai, Maaskofu walikuwa likizo? mbona hawakutoa kauli kama hizi? mbona walimtambua Rais Karume wakati CUF na jumuia za kimataifa walipodai kuwa hakushinda urais kihalali?

  Kuingilia kazi za manispaa na kutoa tamko la kutomtambua meya ni kuvuka mpaka kwa maaskofu kwani dhamira haiwatumi kabisa kuleta madai haya kwani hawana historia nzuri ya kupigania haki!

  Mimi siungi mkono kuchaguliwa meya wa CCM Arusha kama kanuni hazikufuatwa lakini nachokipinga ni hiki cha Maaskofu kujitokeza ghafla na kutoa tamko la kitatanishi wakati haki hiyo waliipoteza huko nyuma! hivyo chondechonde Maaskofu kaeni kimya na kazi hii ya kutetea haki za watanzania zitafanywa na wapigania haki wa kweli!

  Matamshi yenu wakati wote huwa yanatuchanganya wananchi kama tamko la kudai JK ni chaguo la mungu wakati huo huo mnataka achaguliwe Rais mchamungu! tuwaeleweje?
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Polisi badala ya kulinda raia wanabakia kufanya kazi za siasa! Shame on Polisi CCM
   
 4. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hulijui Kanisa; Nyamazaaaa
   
 5. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Matumizi ya nguvu kubwa dhidi ya wananchi wasio na silaha ndiyo hulka za marais wanaotawala nchi kiimla. Wanafanya hivyo ili kuwatisha wananchi wasiendelee kuwatibulia mipango yao ya kujinufaisha wao binafsi na familia na marafiki zao. Watawala wanaoishi kiimla, hufanya hivyo baada ya kubaini kuwa wananchi hawamtaki.
   
 6. A

  Adili JF-Expert Member

  #6
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 2,003
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Kadogoo,
  Safari hii umetumia the wrong of your relief valves.
   
 7. czar

  czar JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 340
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ivo Arusha si ina waislamu pia mbona hawajatoa tamkoo? Au wanajipanga au ndo ...., yule JK ni mwenzetu? Nauliza tu maana mh!.
   
 8. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu kwani Maaskofu huko makanisani wanaongoza na kuhubiria miti? Wanawahubiria watu wale wale ambao serikali ya JK imeamua kuanza kuwaua!!!! Nakushangaa kuwashangaa maaskofu kukemea kitendo hiki!!!

  Tiba
   
 9. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #9
  Jan 8, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Maaskofu wanachunga kondoo sasa kondoo wakiteseka unanyamaza kimya au unanena kidogo...

  Wametoa tamko lao ngoja tusikie masheikh nao kama watazungumza....
   
 10. Sambah

  Sambah Member

  #10
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mwenye akili hawezi kushangaa watetea haki wanapo zvngumza . watu wanapoteza uhai ambao ni haki yao kimsingi unataka wakae kimya utakuwa na matatizo. kiujumla ulitakiwa uwena maono ya mbali kujua kuwa viongozi wa dini zote ni mojawapo ya waleta amani kivipi wapi ulishasikia wakiwataka wav kumwaga damu . hawa wanawatetea kutokana na udhalimu unaofanywa wewe unasema wakae kimya . nakuambia wewe unaeona wamekosea ujue ni wajibu wao kusema maana hao wanaotuongoza wanafundishwa na viongo wa dini lakini hawaelewi nd6 maana wanaona sawa tu kumwaga damu za wasio na hatia . fikiria kido zaidi.
   
 11. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #11
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Kadogoo, Kondoo wa Askofu sio wa kufugwa bali ni hao wanaosulubiwa na Polisi wa Chama cha Mapinduzi. Askofu au kasisi ye yote ni lazima awe na upendo na huruma wakati kondoo wake anapopotea ama kuteswa.
   
 12. baha

  baha Member

  #12
  Jan 8, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  sina uhakika kama na wewe umesoma! wasomi wanatabia ya kuchambua na kuainisha mambo na kuongea akili zao! Shame on you maana inaonekana dini imekukamata na kudhihirisha kuwa ni "virus of the mind" kwako na siyo waamini wenyewe! Kati yako na maaskofu sijui nani anajua kazi ya kanisa...! Ila jaribu kujifunza zaidi utabadilika na kuwa msaada kwa wengine.
   
 13. mchonga

  mchonga JF-Expert Member

  #13
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,250
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Acha unafiki wewe ulikuwa wapi kutotamka hayo, mpaka mauwaji yatokee ndiyo ulete point zisizo na maana. EL aliwaambia kuwa kaeni muwaachie CDM waongoze Jiji la Kimataifa. kwa kuwa mna maslahi yenu na vigogo wamegawiana viwanja. Mnaona ni bora watu wafe kuliko kuumbuka CDM wakichukua Umeya
   
Loading...