Askofu Mhogolo amshambulia Dr Slaa na CHADEMA; asema anawahadaa Watanzania na Siasa za Utapeli

mimi kwa askofu ni sawa na kulinganisha mlima na kichuguu, lakini lazima tukubali kuwa ktk utawawala wa makanisa yetu tutapa viongozi ambao wako tayari kutumia joho la kuwaongoza konndooo wa bwana kwa manufaa ya kisiasa. Naamini askofu wetu amepotoka hapa, hebu washauri wake wa karibu wamsaidie arekebishe suala hili. kwani anglican tulishateswa na mzimu wa mashoga iweje leo tuanze kusumbuka na haya
 
Nivigumu kuamini mtu wa kada ya askofu kuwa na mtazamo kama wako, kwanza hilo la cheap popularity na utapeli kwa watanzania linaonyesha ni jinsi gani huyu askofu ni kipofu, na kwa mtazamo wa kibiblia kama kiongozi ni kipofu basi wanaoongozwa wanahatari ya kutumbukia wote shimoni. ZINDUKA ASKOFU - ULISHACHEMSHA ISHU YA USHOGA SASA ANGALIA USICHEMSHE SIASA ZA NCHI YETU
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Tuliingiliwa na majambazi, wakavunja mlango kwa 'fatuma' wakaiba gari and vitu vingi ndani wakakimbia. Wakati majambazi wakiwa kwenye deal ya kuuza hilo gari, wakakamatwa red handed. Gari, majambazi na manunuzi wakapelekwa polisi na kufunguliwa kesi. Baada ya kesi kutajwa miezi kadhaa, huku zikipigwa tarehe kisingizio uchunguzi unaendelea, mtuhumiwa wa kununua gari akaachiwa huru. Wakati gari liko polisi ikishikiliwa kwa ushahidi, vifaa mbalimbali vikaibiwa. Baada ya miaka 2 kesi ikinguruma, baba wa jambazi akaomba out of court settlement on condition they will pay for all items stolen and we agreed. So far they are yet to pay full amount agreed. Thinking back, it was a waste of time and resources dealing with police and the court on this case, leo hii mke wangu anashauri tungewapiga risasi wale majambazi. This is true story
Hii ndiyo hali halisi ambayo askofu wetu huyu mtetezi wa ushoga hajaielewa. Maana hajawahi kuibiwa wala kudhulumiwa. Kwake mahakama za Tz ni vyombo vinavyotoa haki kwa haki na hajui kwamba huko kuna bei ya kila haki.
mimi naungana na wanaoamini kwamba mkono mrefu wa vibakauchumi (Maana nasikia hawataki kuitwa mafisadi!) wa CCM umeshamfikia na tayari wameshajua bei yake. Si rahisi kwa mtu mwenye akili timamu kuzungumza pumba kama hizi. Nashauri aombewe ili mapepo yake yote yatoke.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Mufti wa Tanzania alipotoa maoni yanayokinzana na wana chadema, wana JF mlisema ana njaa na hajasoma, je huyu askofu naye ana njaa na hajasoma? mbona comments kama hizi hazitolewi? ubalakala utatumaliza

ana njaa kuwa mkamwana wa kikwete yaani mnamsikiliza mhogolo ni kichaa anaumwa unyafuzi wa kukosa pesa anafikiri kikwete ni father krismas mwaka huu kumbe aligawa ahadi na zawadi 2010
 
Mkuu wangu umeyasema yote na kama hawaelewi ni kwa sababu hawaelewi mahakama inaendeshwa vipi. Labda waulize hawa jamaa zetu utaratibu wa kusimamisha kesi za jinai mahakamani zina taratibu gani na kwa nini hizi zinasimamiwa na Prosecutor upande wa mashtaka ya umma hali huyu Prosecutor anatoka wa wizara ya sheria..

Mkuu Mkandara kuna watu humu JF wanaamini kwamba wewe kama Mkandara unaweza Kumfungulia mtu kesi ya Jinai. Wanashindwa kuelewa kwamba Kesi ya Jinai ni baina ya Mtuhumiwa na Jamhuri na Upande wa Jamhuri unakilishwa na Mwanasheria Mkuu ambaye ameshasema kwamba hakuna tatizo Dowans kulipwa Fidia
 
Askofu Godfrey Mdimi Mhogolo wa Dayosis of Central Tanganyika Mkoani Dodoma,amemjia juu Katibu Mkuu wa Chadema na chama chake kuwa wana wachezea Watanzania kwa kujijengea umaarufu rahisi(cheap popularity).

Askof Mhogolo katika mahubiri ya Ijumaa Kuu alisema kitendo cha Dr Slaa kutaja watuhumiwa wa Ufisadi mwaka 2007 huku akiwa na Ushahidi juu ya wanaotuhumiwa na Ufisadi huku akitembea na ushahidi kwenye briefcase ni Kujitafutia umaarufu na kuwapotezea muda Watanzania.

Kama umemkamata mwizi na una ushahidi kwa nini usiende mahakamani na Watuhumiwa washitakiwe!? Kitendo cha Dr Slaa kuongeza tena orodha ya Watuhumiwa huku aliowataja haja peleka ushahidi wake mahakamani kwa orodha ya mwaka 2007 ni kazi ya pwagu na pwaguzi.

Ana wahadaa Watanzania kutokana na uelewa wao mdogo hasa vijana wanao mshabikia! Alimalizia kwa kusema Chadema imekaa na mtizamo wa kutaka watu waiunge mkono kwa fujo na maandamano lakini Viongozi wake wako kwa kujitafutia Umaarufu wa kisiasa.

Akaonya Wanapofanya maandamano yao na uvunjifu wa amani kama ya jijini Arusha wakumbuke kuna amani ya Watanzania ambao si wafuasi wa vyama.

Askofu nenda nchi za wenzetu ukaangalie vyombo vya usalama vinafanyaje kazi, all i need to do is mention kwamba so and so anafanya crime, they move on to work on that...watatafuta ushahidi wenyewe na watawafikisha mahakamani wenyewe.

They have been trained to collect evidence with or without the reporter. Ni aibu kwa askofu kuexpose umbumbumbu kwenye masuala muhimu kama haya!!
 
Mkuu Mkandara kuna watu humu JF wanaamini kwamba wewe kama Mkandara unaweza Kumfungulia mtu kesi ya Jinai. Wanashindwa kuelewa kwamba Kesi ya Jinai ni baina ya Mtuhumiwa na Jamhuri na Upande wa Jamhuri unakilishwa na Mwanasheria Mkuu ambaye ameshasema kwamba hakuna tatizo Dowans kulipwa Fidia
Acheni kubabaisha watu!!...tumelalamikia ufisadi kwa muda mrefu sasa,fungueni mashtaka,sheria zinaruhusu mtu binafsi kufungua mashtaka.Kundi la wanasheria liangalie ushahidi uliopo na wafungue mashtaka kama hawawezi/hawataki basi wampe huo ushahidi mchungaji mtikila!....he is the only man with enough "ballz" to do so.
 
Askofu Godfrey Mdimi Mhogolo wa Dayosis of Central Tanganyika Mkoani Dodoma,amemjia juu Katibu Mkuu wa Chadema na chama chake kuwa wana wachezea Watanzania kwa kujijengea umaarufu rahisi(cheap popularity).

Askof Mhogolo katika mahubiri ya Ijumaa Kuu alisema kitendo cha Dr Slaa kutaja watuhumiwa wa Ufisadi mwaka 2007 huku akiwa na Ushahidi juu ya wanaotuhumiwa na Ufisadi huku akitembea na ushahidi kwenye briefcase ni Kujitafutia umaarufu na kuwapotezea muda Watanzania.

Kama umemkamata mwizi na una ushahidi kwa nini usiende mahakamani na Watuhumiwa washitakiwe!? Kitendo cha Dr Slaa kuongeza tena orodha ya Watuhumiwa huku aliowataja haja peleka ushahidi wake mahakamani kwa orodha ya mwaka 2007 ni kazi ya pwagu na pwaguzi.

Ana wahadaa Watanzania kutokana na uelewa wao mdogo hasa vijana wanao mshabikia! Alimalizia kwa kusema Chadema imekaa na mtizamo wa kutaka watu waiunge mkono kwa fujo na maandamano lakini Viongozi wake wako kwa kujitafutia Umaarufu wa kisiasa.

Akaonya Wanapofanya maandamano yao na uvunjifu wa amani kama ya jijini Arusha wakumbuke kuna amani ya Watanzania ambao si wafuasi wa vyama.

Askofu aliyeoa Muastralia na kushabikia mashoga sijui atatoa kauli gani ya maana toka mdomoni mwake kama siyo kushabikia ufisadi wa kila aina.
 
Acheni kubabaisha watu!!...tumelalamikia ufisadi kwa muda mrefu sasa,fungueni mashtaka,sheria zinaruhusu mtu binafsi kufungua mashtaka.Kundi la wanasheria liangalie ushahidi uliopo na wafungue mashtaka kama hawawezi/hawataki basi wampe huo ushahidi mchungaji mtikila!....he is the only man with enough "ballz" to do so.

Mahakama za kifisadi? Mbona waliotajwa hawalalamiki?
 
Sikila mtu aniitaye bwana ataingia ktk ufalme wangu.

Hawa watumishi wa Mungu tuwaombee angalau Mungu awafunge vinywa
Wasiongee mambo wasiyoyajua,mana niaibu kw kiongozi
wa kariba ya Askofu kupotosha watu.

Tuzidi kuwaombea.
 
Ya Mchungaji yanaweza kuwa ya ukweli au uongo lakini sisi washabiki wa Chadema tuko biased hadi inanisikitisha, yaani sisi ni kukandia na vijembe tu, Nahisi tukishika madaraka tutakua na serikali ya kidikteta!
 
Huyu jamaa ni swahiba wake mzee Malecela. so, huenda kamtuma akaseme vile.
Yaani wewe ndo umeugundua mchezo hasaa big up nakupa.. ni baada ya list of shame kupanuliwa. Mafisadi wana tabia ya kuteteana na kulindana, lakini moto unaoendelea hata mlindane vipi mwisho wenu umefika.Fisadi mjanja sasa hivi ni yule aliye kimya akilisikilizia mchezo utaishaje. Ushauri wa bure mafisadi na mnaotumwa: mbinu zenu zote tunazijua too late hakuna wajinga subirini tu...........
 
Wimbo ukirudiwa rudiwa sana unakosa radha, ndivyo ilivyo kwa orodha ya Dr.Slaa, naamini ata wewe umeshaanza kunotice hilo kufuatia orodha yake ya Tabora!!

Mtu akikuibia utaacha kukemea/kuongelea wizi huo kwa sababu ya kukosa ladha?!!!
 
Labda kuna hoja Hebu ngoja nifuatilie zaidi ukiwa msikivu utajua mengi sana nitamani kumhoji zaidi huyu Askofu !!!
 
Acheni kubabaisha watu!!...tumelalamikia ufisadi kwa muda mrefu sasa,fungueni mashtaka,sheria zinaruhusu mtu binafsi kufungua mashtaka.Kundi la wanasheria liangalie ushahidi uliopo na wafungue mashtaka kama hawawezi/hawataki basi wampe huo ushahidi mchungaji mtikila!....he is the only man with enough "ballz" to do so.

nawe "ume2miwa" useme ka yeye. Kamuhulize huyo "mtikila" kesi yake ya mgombea binafsi ambayo hukumu yake ilikuwa ya "kibabahishaji" ilikua vp mahakamani, na ndo'sehemu pekee alipokua anategemea kupata hiyo haki?
 
"nyie mnaongea ongea na kupiga kelele juu ya ufisadi ni kwamba hamjapata nafasi ya kula,ila mkipata nafasi ya kula hamtapiga tena kelele" maneno haya yalitamkwa na kardinal pengo,je kina SLAA na wenzie wanaopiga kelele ni kwa vile hawajapata nafasi ya kula?

Kwa hiyo wewe umepata nafasi ya kula! Mimi nimesema kama mtu alidiriki kushabikia Ushoga hadharani tena ndani ya kanisa siyo ajabu kushabikia Ufisadi! Maana ndiyo tabia ya Mhogole alikuwa askofu wa Kwanza Tanzania kumuunga mokono Askofu Shoga Gene wa America, mpaka iliperekea vurugu katika Dayosisi yake kugawa watu ndani ya anglican hadi leo.

Je wewe unaweza kuthibitisha pasi na shaka kuwa watu wote wanapinga Ufisadi ni kwasababu hawajapata nafasi ya kula, je una evidence yoyote?

Jaribu kupanua akili yako kijana, kuna watu wamo humu wana uwezo mkubwa kuliko Babako, Mamako na hadi Ukoo wako wote.
 
Kama na wewe ni mmoja wa watu CCM inayotegemea katika kutoa Mawazo katika hiki kizazi kipya Basi CCM ina Kazi Kubwa sana. Naona Mmewashauri wazee wenu wagawe Bure Gazeti linalomchafua Dr. Slaa hivi hamuoni kama Mnazidi kukimaliza chama chenu. Ila Mimi nafurahia sana kufahamu aina ya Vichwa vilivyomo CCM maana inanipa Uhakika kwamba CCM Imekufa kwa Sababu haina Mawazo Mapya na hiana watu wa Kutoa Mawazo Mapya.

Sasa Mmeingia Mkenge Mnacheza Ngoma ya Dr Slaa ambayo kwa Miaka Mitatu mmekuwa Mnaona Aibu Kuivina, sasa Aibu imewatoka Mmeamua Kuicheza na tena Mnakata Viuno kwa Ustadi Mkubwa na Wajuvi wa Mambo wamekaa kando wakiangalia mwisho wa Mchezo

Mkuu inelekea unamuona Dr Slaa kuwa kamungu kako na una ukosefu wa kuona logic ya yaliyofanywa na CCM.
Jaribu kufikiri kidogo na usiingize katika unazi wa kisiasa maana wewe inelekea ni aina ya watu mnaoishia kuandamana bila kufikiri.
Siyo siri alichosema Dr Slaa kuhusu ufisadi kilisemwa na watanzania wengi tu na si peke yake.Hata ndani ya CCM upinzani ulikuwepo kupinga ufisadi.
Soma
Fikiri
Elewa na jaribu kurefresh kumbukumbu yako.
Tofauti kati ya uCoconut uliopost na ukweli wa mambo ni kuwa zaidi ya sera ya ufisadi chama chako hakina lolote la kuwaeleza waTanzania.
Dr Slaa amekuwa polisi mzuri wa kisiasa, sasa mpumzisheni au mpeni wimbo mpya wa kuimba majukwaani.
Sita comment la viuno maana that is beneath me and it explains the kind of character that is supposedly a CDM coconut.
Kazi kwako mkuu Libido er.... I mean Albedo
 
Acheni kubabaisha watu!!...tumelalamikia ufisadi kwa muda mrefu sasa,fungueni mashtaka,sheria zinaruhusu mtu binafsi kufungua mashtaka.Kundi la wanasheria liangalie ushahidi uliopo na wafungue mashtaka kama hawawezi/hawataki basi wampe huo ushahidi mchungaji mtikila!....he is the only man with enough "ballz" to do so.
Well said, only Mtikila is the man.
 
Mahakama gani inayoweza kutenda haki kwa Mafisadi wee vaa joo lako mwimbie Bwana wimbo mpya huku tuachie wenye shida na dhiki tupate matumaini toka Kwa mtetezi wa ukweli Dr Slaa.kesi ngapi umeona walala hoi wakishinda .
 
Huyo askofu anafaa kuja na njia mbadala ya kutatua matatizo ya watanzania, kukosoa hatua ambazo zinaendelea kuleta matokeo ambazo Dr slaa na CDM wanachukua si busara.
Hii inaonyesha jinsi askofu huyu alivyo na tamaa ya kupata umaarufu hapa nchini. Lakini anapaswa kukumbuka kwamba kazi ya kanisa hapaswi kuichanganya na siasa, vinginevyo aache kazi ya kuhubiri na aanze kufanya siasa, huo ni ushauri wa bure tunampa
 
Back
Top Bottom