Mlendamboga
JF-Expert Member
- Sep 14, 2011
- 664
- 334
Taarifa kutoka KKKT Dayosisi ya kusini magharibi Magoye, zinadokeza kuwa aliyekuwa askofu wake Tito Job Mbwilo ameshindwa kutetea kiti chake baada ya kuangushwa kwenye uchaguzi uliofanyika 25 Octoba 2018
Aliyechaguliwa kwenye uchaguzi huo ni mchungaji Mlimitsi Nguvila ambaye kwa sasa anakuwa askofu mteule mpaka atakapoapishwa.
Aidha katika Uchaguzi huo, Msaidizi wa askofu amechaguliwa mchungaji Ngogo ambaye amemshinda Dr Naibu ambaye ni mkuu wa jimbo la Matamba
mara baada ya matokeo hayo Watu wanashangilia kwenye mitaa ya ti Matamba, Magoye baada ya moshi mweupe wa kura za siri kutegua kitendawili cha kiimani walichokuwa wakisubiri waumini wa KKKT na hasa wakazi wa bonde la Uwanji anbalo ndiko dayosisi hiyo ipo lililopo mati ya mkoa wa Njombe na Mbeya.
Askofu Mbwilo amedumu kwenye uongozi tangu miaka ya 90 mwanzoni baada ya kustaafu kwa askofu Levy Nsemwa, lakini aliendelea kukisaka kiti hicho licha ya kuonekana kuchokwa na waumini kutokana na kupoa kwa waumini kiimani na kushindwa kukua kwa huduma za kijamii zilizokuwa chini ya kanisa hasa afya na miradi mingine ya maendeleo