Askofu Malekana: Matamko na nyaraka yanatengeneza taharuki katika jamii

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,862
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Kusini mwa Tanzania, Mark Malekana, amesema matamko na nyaraka zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa madhehebu mbalimbali nchini kwenda wa wahumini wao dhidi ya uogonjwa wa corona yanaongeza taharuki na kuongeza hofu kwa jamii.

Askofu Malekana amezungumza hayo leo Jumamosi, Febreuari 20, wakati akiongea na wahumini wa kanisa hilo katika Ibada maalumu iliyofanyika kwenye kanisa la Wasabato Sima mjini Bariadi katika Mkoa wa Simiyu.

b9a67f10-4dc5-4fff-8479-79c96c29242f.jpg
Kiongozi huyo amesema kuwa yeye kama Askofu wa kanisa hilo hawezi kutoa takwimu, wala ukubwa wa tatizo kwani kufanya hivyo ni kuingilia majukumu ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee ja Watoto na inaweza kuongeza hofu kubwa kwa waumini wake na jamii kwa ujumla.

Amesema kuwa hofu imekuwa kubwa kuliko tatizo lenyewe, ambapo ametakwa wahumini wa Kanisa hilo nchini kumrudia mungu na kuomba sana dhidi ya janga la ugonjwa huo ambao umeendelea kutesa ulimwengu.

“Kumekuwa tena siku za karibuni na hali fulani ya sintofahamu, msukusuko katika jamii, maelekezo na matamko ya watu mbalimbali, hata viongozi wa dini hapa na pale, wemetoa matamko, wameandika nyaraka na haya mambo yanaonekana kuchangia taharuki au kutengeneza taharuki fulani katika jamii.

“Sasa tufanye nini katika mazingira kama hayo, jambo la kwanza ni kumtanguliza mungu na kutambua kuwa yupo pamoja na nasi, twende kwake tukamlilie naye atatuokoa, lakini tuondoe hii hofu kwa kumuomba mungu lakini tuzingatie mashrati ya kiafya ambayo tunaelekezwa,” amesema Askofu Malekana.

AAidha, Askofu Malekana amewataka wahumini wake kujikabidhi kwa mungu kwani yeye ndiye kila kitu, ikiwa tayari wameingiwa na hofu mwenye kushinda tatizo hilo ni mungu pekee ikiwa watamuomba kila siku.

“Hofu ni zaidi ya tatizo lenyewe, hofu inaweza kuondoa maisha hivyo yapaswa wananchi waondoe hofu na kujipa moyo pamoja ujasiri na waendelee na shughuli za kila siku bila woga,” amesema Askofu Malekana.

Askofu huyo amewataka watanzania kuzingatia kanuni za afya na kuzifanya kuwa ni sehemu ya maisha ya kila siku pamoja na kufuata miongozo na maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya.


CHANZO: Mtanzania
 
Back
Top Bottom