Askofu Malasusa: Wanandoa wamejawa hofu kwenye mahusiano, talaka zimeongezeka

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,402
Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Alex Malasusa amedai kuwa kwa sasa jamii imekosa hali ya upendo hali inayosababisha kuongezeka kwa matukio ya mahusiano mengi kuvunjika.

Askofu Malasusa amesema kauli hiyo Desemba 25, 2018 katika ibada ya Krismasi iliyofanyika katika Kanisa la Azania Front jijini Dar es Salaam ambapo amesema wana ndoa wengi wanahofu na mahusiano.

“Siku hizi talaka zimezidi jamii haina upendo wala hofu ya Mungu, hofu imejaa katika ulimwengu, wengi waliopo katika ndoa hawana hakika kama wataendelea,’’ amesema.

Aidha ameongeza kuwa “malaika anasema usiogope nitawaletea habari njema, tena katika aya yetu ya siku ya leo tunasema tumepewa mtoto mwanamume, yeye yupo tayari kubadilisha mitazamo yetu kutuondoa katika hofu na kuwa wajasiri katika maisha yetu.”
 
Ni maneno tu ambayo yataendelea kusemwa Ila hayatabadilisha chochote juu ya hii adhabu ambayo kizazi kimepewa kwa ajili ya ukaidi wake.....Kama binadamu hawakubali kuwa wanyenyekevu na kulila lile tunda kwa nidhamu Basi kupona wasahau..
 
Bora baba askofu umeliona hilo,kwa upande mwengine viongozi wa dini wanaidhinisha kutoa talaka badala ya kuunganisha bila kuangalia hathali za watoto.
 
Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Alex Malasusa amedai kuwa kwa sasa jamii imekosa hali ya upendo hali inayosababisha kuongezeka kwa matukio ya mahusiano mengi kuvunjika.

Askofu Malasusa amesema kauli hiyo Desemba 25, 2018 katika ibada ya Krismasi iliyofanyika katika Kanisa la Azania Front jijini Dar es Salaam ambapo amesema wana ndoa wengi wanahofu na mahusiano.

“Siku hizi talaka zimezidi jamii haina upendo wala hofu ya Mungu, hofu imejaa katika ulimwengu, wengi waliopo katika ndoa hawana hakika kama wataendelea,’’ amesema.

Aidha ameongeza kuwa “malaika anasema usiogope nitawaletea habari njema, tena katika aya yetu ya siku ya leo tunasema tumepewa mtoto mwanamume, yeye yupo tayari kubadilisha mitazamo yetu kutuondoa katika hofu na kuwa wajasiri katika maisha yetu.”
Talaka? Kwani wakristo huwa wanaachana?
 
Bora baba askofu umeliona hilo,kwa upande mwengine viongozi wa dini wanaidhinisha kutoa talaka badala ya kuunganisha bila kuangalia hathali za watoto.
Bora watengane kuliko waje kuchinjana ndani.
 
Kwa aina ya maisha na manzingira tuliyonao sasa talaka haziepukiki kwa nini uishi na mtu kwa mateso, mara nyingi kinachovunja ndoa ni usaliti wa mapenzi, kitu ambacho kwa sasa kuki- control ni kazi kwa sababu ya technologia kuwa kubwa na utafutaji wa maisha, jamaa yangu alimpeleka wïfe chuo wakati anamaliza akarudi na mimba .
 
Mathayo 19:9 "Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokua ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini."
Malasusa amesema talaka zimeongezeka kwa sababu ya upendo umeoungua na watu hawana hofu ya Mungu. Hajataja uasherati hapo. Muwage mnaelewa hoja siyo kukurupuka. Kwani mimi silijui hilo andiko 19:9 Mathayo?
 
Mbona una jazba sana mkuu, hivi unaelewa maana ya neno "Upendo"?

Hivi wanandoa mkiwa na upendo, uasherati utakuwepo?

Wakati mwingine uwe unajifunza kupunguza jazba kabla ya kuandika au kumjibu mtu.
 
Hao viongozi wa dini wenyewe hawana upendo wala hofu ya Mungu, wengine mpaka wanazini tena na wake za watu na ufisadi.
 
Malasusa amesema talaka zimeongezeka kwa sababu ya upendo umeoungua na watu hawana hofu ya Mungu. Hajataja uasherati hapo. Muwage mnaelewa hoja siyo kukurupuka. Kwani mimi silijui hilo andiko 19:9 Mathayo?

Watu hawana "hofu " wanafanya lolote uasherati likiwa mojawapo
 
Back
Top Bottom