Askofu Malasusa Naye Atoa Elimu ya Uraia: Chagueni mtu makini si chama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu Malasusa Naye Atoa Elimu ya Uraia: Chagueni mtu makini si chama

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by The Dreamer, Oct 17, 2010.

 1. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 2. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nafikiri kile kipindi cha kuchagua chama kimepitwa na wakati maana hatujaona matunda yake, wakati huu tuangalie ni nani anaweza kutuvusha na si chama gani.
   
 3. A

  August JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  ngoja bi s akafanye kampeni za shuka kwa shuka hapo kumtoa askofu mapepo ya uchaguzi
   
 4. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Na ndivyo itakavyokuwa!

  Lakini sisim ... waalizma hoja ya mgombania binafsi katika ngazi ya Urais...!
   
 5. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Tarehe 22 ni zamu ya masheikh kutoa muongozo wao wa nani kuchaguliwa oktoba 31.Safari hii kuchanganya dini na siasa ruhsa kama ilivyokuwa wakati wa kupigania uhuru.
   
 6. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Hapa maaskofu hawajataja nani achaguliwe. Wametaja sifa. Kama JK anazo usiwe na shaka. Bila shaka safari hii lazima ile kwenu
   
 7. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2010
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,289
  Likes Received: 598
  Trophy Points: 280
  "Waliponiletea kadi ya mwaliko, niliwauliza nani mwingine atakayehudhuria hafla hii?"
  Alikuwa anahofia kukutana na nani huko?
   
 8. k

  kisoti Member

  #8
  Oct 17, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 81
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
   
 9. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ukiachilia mbali Askofu Malasusa ambae hajawahi kushika uongozi katika CCM unaweza ukadharau mamneno yake japo yana ujumbe mfupi sana....lakini kwa Rais mstaafu ambae alishakua mwenyekiti wa CCM lakini hakusema tuichague CCM nadhani kwa mtu mwenye uwezo wa kufikiri utakua umeshajua kuna jambo linaendelea. Tatizo ni kwa nini hawatuweki wazi. Kwa nini wasitamke chagua flani???? atleast kwenye ngazi ya Urais. Ingekua vyema kama wangesema chagua Kikwete koz ni mwenzao katika CCM ila hawajamtaja....wanachosema ni chagua mtu na si chama...........


  Hawa watu wanatuambia tumchague Slaa dhidi ya Kikwete sema hawana uthubutu wa kulitamka hili....wanaijua System kuliko sisi tunavyoijua...na wameshaona kuwa something is wrong within the system na the only man to wipe off our tears ni SLAA.....Am sure one day one them will dare to say this b4 31st....
   
 10. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  SIKU 16 kabla ya kufanyika wananchi kupiga kura, askofu mkuu wa Kanisa la Anglikana, Dk Valentino Mokiwa amedai kuwa hivi karibuni alipelekewa rushwa ya Sh11 milioni na mtu asiyemfahamu ili asizungumze masuala ya uchaguzi.

  Dk Mokiwa alisema hayo kwenye tamasha la kuombea uchaguzi mkuu lililoandaliwa na Usharika wa Yombo wa Kanisa la Kiinjili la Kulutheri Tanzania (KKKT) Dar es Salaam jana.

  Alisema tukio hilo lilitokea siku moja baada ya watu wawili mmoja akiwa anamjua kwenda nyumbani kwake kwa lengo la kumsalimia ambapo alizungumza nao kisha wakaondoka.

  "Siku moja baadaye, mlinzi alinipigia simu akaniambia yule mgeni wa jana ameleta ….nikamwambia kwa nini ulichukua? sina ahadi na mtu yeyote kuniletea mzigo," alisema Dk Mokiwa.

  Alifafanua kuwa taarifa hizo zilimlazimu aende nyumbani kwake ili kujua nini kimeletwa... na alipofungua alikuta fedha taslimu Sh11 milioni ambazo zilimtia wasiwasi.

  "Nikampigia yule ninayemfahamu nikamwambia njoo uchukue fedha za jamaa yake, akaniambia 'usiwe na wasiwasi', nikamwambia haiwezekani njoo akaja akachukua zile fedha," alisema.

  Aliongeza kuwa alikumbuka maneno ya mtu yule wakati walipokwenda nyumbani kwake kuwa nyinyi (viongozi wa dini) mkizungumza nchi inatikisika, akaona ile ilikuwa ni rushwa ili anyamaze kuzungumzia masuala ya uchaguzi mkuu ujao.

  Alisema aliamua kukataa fedha hizo kwa sababu alikuwa na wasiwasi asije baadaye akaambiwa na yeye alipewa fedha za rushwa na kumalizia nyumba yake kwani ile kwake ilikuwa ni rushwa ili anyamaze.

  Akizungumzia hoja yake iliyopingwa na taasisi za serikali zinazohusiana na rushwa na uchaguzi kwa madai kuwa anahamasisha watu kupokea rushwa, Dk Mokiwa alisema:

  "Mimi sikuhamasisha rushwa ila nilikuwa nawapinga viongozi wabaya wanaotoa rushwa kwa wapiga kura. Sheria ya Gharama za Uchaguzi si mbaya, lakini wasimamizi wa sheria hiyo ndio wabaya," alisema Dk Mokiwa.

  Alidai kuwa atafanya awezalo kuhakikisha kuwa viongozi wala rushwa hawaiongozi nchi hii kwa sababu mwaka huu rushwa imeenea na wakati huu wa kampeni rushwa ndio inaliwa sana na viongozi wasiokubalika ndio watoa rushwa.

  "Tunamuomba Mungu leo, tupate viongozi ambao hawajawahi kutuongoza nchi hii; viongozi watakaotuletea amani bila ya kuwepo polisi shirikishi kwa kuwa hapa tulipofika ni matokeo ya kuwapa ushirikiano viongozi wabovu," alisema.

  Akizungumzia kauli ya vyombo vya usalama juu ya amani kulekea kwenye uchaguzi, Dk Mokiwa alisema ili kulinda amani iliyopo hakuna budi vyombo hivyo vikatenda kazi yake bila ya upendeleo katika kusimamia uchaguzi.

  "Nani alisema hakuna amani, tatizo ni vyombo hivi vinataka kuwalinda watu waendelee kuongoza wakati wananchi wamewachoka. Wanatakaiwa wawe fair katika usimamizi," alisema.
   
 11. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #11
  Oct 17, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,999
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  gari inapita hiyo, CCM wanasoma namba za gari
   
 12. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2010
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  """Tumedanganywa vya kutosha miaka mingi, na kuchagua chama. "Tunahitaji kutulia na kumuomba Mungu ili atuelekeze njia ya kupata na kuchagua kiongozi bora na atakuwa nasi katika Uchaguzi Mkuu". Kauli ya Dk Malasusa inakuja siku chache baada ya viongozi wa makanisa Katoliki, KKKT na Pentekoste mkoani Kilimanjaro, kutoa waraka unaowataka waumini wao kuchagua mgombea anyafaa kuwaletea maendeleo badala ya chama cha siasa""" CHANZO: Malasusa: Chagueni mtu makini si chama

  SIPATI PICHA HALI INGEKUWAJE KATIKA JAMIIFORUMS IWAPO MANENO HAYA YANGESEMWA NA MMOJAWPO WA MASHEIKHE. LAKINI LEO YAMESEMWA NA ASKOFU MAMBO NI SHWARI. KWELI KUNYA ANYE KUKU AKINYA BATA KAHARISHA.

   
 13. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2010
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  kumuelewa alhaji hassan mwinyi ni lazima ukijue kiswahili ipasavyo. Yee ni mswahili hasa, anaongea lugha ya kiswahili. Aliposema chagueni viongozi bora alimaanisha viongozi kutoka ccm kwani ccm ndio ina viongozi bora. Sema wee hukumwelewa, rudia tena hotuba yake na kisha umsikilize kwa makini.
   
 14. S

  Sir Leem JF-Expert Member

  #14
  Oct 17, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Waatambiwa Masheikh hawana elimu ,wana elimu za Madrasa!wadini!Akitamka Akofu anatoa elimu ya Uraia
   
 15. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,053
  Likes Received: 3,961
  Trophy Points: 280
  kwani uwongo anayeshabikia ccm/kikwetu hana upevu wa mambo hebu jiulize kwanini Tanzania isiwe kama Mauritius in Moo ibrahim's index? wakati Mauritius wana sukari tu sisi tuna kila kituuu! Au kwanini leo hii uwajue mafisadi ila Kikwete asiwajue? Ni dhahiri tumekosa uongozi bora na ni watu wa Madrasa bila elimu dunia tu ndo wanaweza pinga! ninajuta kumpigia Kikwetu 2005, kila ranks Tanzania imeshuka at World stage! tumechoka na sikio lisiloskia dawa!
   
 16. B

  Bull JF-Expert Member

  #16
  Oct 17, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mpuuzi mwingine anafundusha watu wachague sura sio sera!!! Allahu akbar

  Kamatukiangalia umakini basi mchungaji mwenzake Slaaa hafai kabisa hana umakini kwa sababu zifuatazo:

  1- Decision zake mbovumbovu kwa kuacha kazi ya Mungu kukikmbilia siasa
  2- Kakimbizwa ukatibu wa chama cha kikatoliki
  3- Kaowa mke wa mtu bila kufanya uchunguzi wa makini
  4- Chama chake kina asili ya udini, ukabila na udicteta anshindwa kuukemea
  5- Kavuncha amri za ukatoliki, kwa kuowa na kuacha na kuowa tena mke wa mtu
  6- Alikuwa mkereketwa wa CCM, alipo nyimwa ubunge akahamia chama cha mtandao wa kanisa
  7- nk..........

  Mchungaji Slaa hana umakini kabisa katika uamuzi wake, kwa hiyo huyu mchungaji angeweka wazi bila kujikanyaga na pili angewafundisha kondoo wake wachague sera si sura. Ohfyuuuu   
 17. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  These comments comes from a great thinker????????????????????
   
 18. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #18
  Oct 17, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hata mkimtaja Jakaya kwa jina msikitini hatachaguliwa maana waislamu wengi wameenda shule na wanachukia ufisadi sasa. Pole. Wambie watoe tamko sie tunasubiri:dance:
   
 19. Y

  YgJunior Member

  #19
  Oct 17, 2010
  Joined: Jan 12, 2008
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  mungu akusamehe kwa upuuzi wako siku ya mwisho usichomwe na moto wa milele
  maana hujui ulitendalo
   
 20. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #20
  Oct 17, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Slaa hana chake na Ukristo Tanzania ndio unajizika wenyewe kwa kujionesha kuwa hauna mafunzo madhubuti.
  Itakuwaje wahamasishane kumchagua mtu ambaye amevunja mafunzo ya kanisa.
   
Loading...