MAFILILI
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 2,377
- 1,194
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Arusha, Thomas Leizer, amesema vurugu za kisiasa mkoani hapa, hazina faida na zinagharimu maisha ya wananchi. Kiongozi huyo amepongeza muafaka uliofikiwa kati ya madiwani wa CCM na CHADEMA kwa nafasi ya meya na kumtaka mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kuridhika badala ya kuendekeza vurugu. Amesema wananchi wamekuwa wakiishi kwa kuhofia usalama wao, kutokana na vurugu na kwamba, huu ni wakati wa madiwani kufanya kazi.
Kiongozi huyo wa kanisa alitoa tamko hilo jana, wakati wa uchangiaji ujenzi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Likamba, wilayani Arumeru. Alitangaza kumtambua Meya wa jiji hilo, Gaudence Lyimo (CCM).Alisema Lyimo amechaguliwa kihalali, hivyo jambo muhimu kwa madiwani ni kufanya kazi ili kuharakisha maendeleo ya wananchi.
Tamko la Askofu Leizer ni pigo kwa uongozi wa CHADEMA na Lema, ambao wamegoma kuutambua muafaka huo, huku wakiwatuhumu madiwani wao kuwa wamerubuniwa. Uongozi wa juu wa CHADEMA uliunda kamati chini ya Mabere Marando, ambayo iliwahoji madiwani wa chama hicho, huku Lema akitamba yupo tayari kufanya kazi bila kuwashirikisha madiwani hao.
"Madiwani walifanya jambo la busara, kwani vurugu zilizokuwa zikiendelea hazikuwa na faida, zaidi ya kugharimu maisha ya wananchi. Lema aridhike na nafasi aliyopata," alisema. Askofu Leizer alisema ameshangazwa na hatua ya Lema kuendeleza vurugu, huku akishindwa kukaa na madiwani wa chama chake kuandaa bajeti na kuwasilisha kwa jiji.
Kwa mujibu wa Leizer, vurugu za kisiasa zinazoendelea mkoani hapa zimefika pabaya, kiasi cha kumgombanisha mbunge na madiwani, jambo alilosema ni la hatari kwa kuwa linachelewesha maendeleo. Alimtaka Lema kuridhika na nafasi ya ubunge aliyonayo, na ya naibu meya na uenyekiti wa kamati ambazo madiwani wa CHADEMA wamezipata ili wazitumie kuwatumikia wananchi.
Source: Gazeti la Uhuru, Julai 18, 2011
NGOMA INOGILE A TOWN!