Askofu Kulola: Kuna mtandao wa kisiasa makanisani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu Kulola: Kuna mtandao wa kisiasa makanisani

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, Oct 22, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]* Asema unampigia debe mmoja wa wanasiasa nchini
  * Aonya walio chini yake kutojiingiza, Tume yasema ni hatari

  NA MWANDISHI WETU
  MKUU wa makanisa ya Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Askofu Mosses Kulola, ametoboa kuwa kuna mtandao wa kisiasa makanisani ambao unampigia debe mmoja wa wanasiasa nchini. Kutokana na hali hiyo, amepiga marufuku watumishi na waumini wa kanisa hilo kushiriki katika mipango ya uchochezi wa kidini unaofanywa na makanisa hapa nchini. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kutoka jijini Mwanza, Askofu Kulola, alisema: ìNapiga marufuku makanisa yote yaliyo chini yangu hapa nchini, kujiingiza katika mpango huo wa kishetani unaondaliwa kuleta uvunjifu wa amani."
  Alisema haoni sababu ya kuungwa na ëforumí ya makanisa kama chombo cha kuutetea Ukristo unaodaiwa uko mbioni kutokomezwa na Uislamu kwa kumkataa Rais Jakaya Kikwete na kuona Rais mkristo ndiye atakayenusuru ukristo hapa nchini. ìKanisa limejisahau, limeacha maombi sasa linataka kulazimisha kupata kiongozi wa nchi nje kabisa ya mpango wa Mungu,î alitahadharisha Askofu Kulola.
  Askofu huyo ambaye ni miongoni wa viongozi wa kidini wanaoheshimika hapa nchini, aliongeza kuwa anashangaa kuona jinsi viongozi wa makanisa wanavyokaa pamoja kuwapotosha waumini wao juu ya ukweli wa Mungu wakati awnaelewa wazi staili ya kanisa ya kuomba kitu chochote ni kwa njia ya maombi na siyo kutumia nguvu kama wanavyofanya sasa. Kulola aliendelea kusema kuwa baadhi ya viongozi wa makanisa wametanguliza maslahi binafsi badala ya kulitanguliza taifa na kuwa nenola Mungu linaeleza kuwa serikali au mamlaka yoyote inayotoka kwa Mungu hakuna budi kuitii na jukumu la watumishi wa Mungu ni kuiombea mamlaka hiyo.
  Askofu Kulola alisema katika Biblia hakuna kifungu chochote kinachoeleza nchi lazima iongozwe na mkristo, Mungu hana upendeleo, chuki wala wivu kama ilivyo kwa binadamu. Rais Kikwete hana baya katika nchi yetu, ameongoza kwa amani na utulivu. Hajamzuia mkristo yeyote kueneza na kuhubiri Injili amekuwa akiwapa ushirikiano na wakati mwingine mmekuwa mkumtumia kwa shughuli zenu, leo mnamkataa eti mnataka Rais mkristo,îalihoji kiongozi huyo. Aliwakumbusha viongozi hao wa makanisa kuwa Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ambaye ni muislamu aliwajengea kanisa Wakristo mkoani Kilimanjaro na ambalo hakuna kiongozi aliyelikataa kwa kuwa limejengwa na muislamu. Alitoa wito wa kudumisha amani ya Tanzania kwa kupinga kwa nguvu zote tamko lolote lenye misingi ya udini na kuwataka watanzania wa dini zote kudumisha mshikamano katika nchi pasipo kubaguana.
  Kwa misingi hiyo, alisema hawawezi kumkataa Rais Kikwete kwa uislamu wake na kumweka Rais mkristo kwa nguvu pasipo mpango wa Mungu. Ameagiza kuwepo kwa ibada za Jumapili katika makanisa yote ya EAGT kama kawaida na tofauti na ibada zilizopendekezwa na ëforumí ambazo zitafanyika Jumamosi badala ya Jumapili ya wiki ijayo ambayo itakuwa siku ya kupiga kura. Pia ameagiza makanisa yote ya EAGT kufunga na kuomba kwa ajili ya nchi na serikali. Katika hatua nyingine, Hamis Shimye, anaripoti kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kauli zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa dini kuwaelekeza wananchi kupiga kura kwa misingi ya udini ni hatari kwa taifa.
  Hali ambayo NEC imevitaka vyama vya siasa nchini kuhakikisha haviwatumii viongozi wa dini kuwapigia kampeni kwa ajili ya wagombea wao. Mkurugenzi wa uchaguzi, Rajabu Kiravu, aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kauli zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa dini. Alisema viongozi wa dini nao wanapaswa kuheshimu maadili ya uchaguzi nchini kama walivyofanya viongozi wa vyama vya siasa. ìViongozi wa vyama vya siasa walisaini fomu za maadili ya uchaguzi zenye mwelekeo wa kuacha kutumia udini kwenye kampeni zao,ííalisema
  Kiravu alisema kifungu cha 2.1(i) na 2.2(j) vinaeleza wazi kwa viongozi, wagombea au wafuasi wa vyama vya siasa kuhakikisha majengo wanayoyatumia kwa ajili ya kampeni sio ya ibada. Kutokana na hali hiyo, Kiravu alisema viongozi wa dini walipaswa kuliheshimu hili ambalo viongozi wa vyama vya siasa wanalitambua. Hivyo aliwataka viongozi wa dini kuacha kuwashinikiza au kuwaelekeza wananchi wawachague viongozi kwa misingi ya udini kwa kuwa inahatarisha amani ya nchi. Kwa upande wake, Baraza la Maadili ya Kiislamu Tanzania (BAMAKITA) limewashukia viongozi wa dini wanaogeuza madhabahu kuwa majukwaa ya kisiasa jambo ambalo linahatarisha umoja na mshikamano, anaripoti Khadija Mussa.
  Mwenyekiti wa BAMAKITA, Sheikh, Athumani Mkambaku, alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa kampeni za uchaguzi mkuu. ìTunawaona baadhi ya viongozi wa makanisa wamejiingiza kwenye kampeni ndani ya nyumba za ibada, kitendo chenu cha kumpigia debe makanisani mgombea wenu kinatufanya sisi Waislamu na wananchi tumuogope kuliko ukoma," alisema. Mkambaku aliwataka wananchi kuwa makini na viongozi wa aina hiyo na wajitokeze siku ya kupiga kura ili watumie haki yao kwa kuwachagua viongozi bora wasioendekeza udini na ukabila na ambao wataendeleza amani na mshikamano wa Watanzania. Alisema taifa linaweza kuingia kwenye mgogoro usio wa lazima kama wapiga kura hawatakuwa makini kuchagua viongozi. Mwenyekiti huyo aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na NEC.

  Chanzo: Gazeti la Uhuru

  UPDATE
   
 2. m

  mosesk Member

  #2
  Oct 22, 2010
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mjukuu wake Mbasha si yuko kwenye kampeni za JK , hilo linafahamika. wale wale!
   
 3. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2010
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ana mgawo wake hapo, mjukuu ambaye ni mwimbaji wa injili mbona anaimba siasa na amenyamaza? toa boliti jichoni mzee ndipo utaona kibanzi kwa mwenzio....
  mbona hao watu mnaowatuhumu leo walisema JK ni chaguo la Mungu mkachekelea bila kukemea kuwa wametumia jina la Mungu bure? leo wamesema msichague mafisadi mnalilia kama watoto....mnataka kutuaminisha kuwa CHICHI m ni mafisadi na tuendelee kuwapa kura?
  katika hili MTUMISHI nakupinga kwa ujasiri kabisa, i wish ningekuona kwa macho ni kuambie kweli hii.....injili ya siku hizi sio kama ya zamani ambapo mliweza hata kufundisha mapotofu bila kupingwa na waumini leo tunakupinga ukienda kinyume na kweli ya Mungu....unapinga siasa kanisani unamalizia kwa kupiga kampeni....
  i guess umeishiwa mzee wangu hasa ktk hili uko nje kabisa ya point,unapinga watu kutowachagua mafisadi? wewe unatakatuongozwe na mafisadi?
   
 4. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ndugu;

  Hilo ume-quote toka Gazeti gani? Kwanza nani analisoma gazeti hili UHURU! Jamani...!, tunaweza kuishi mwaka 2010 lakini tunajenga mawazo kwa kutumia zana za 1960! Ndio hii kusoma Magazeti haya ya 'Kibanga kampiga Mkoloni', yanakurejesha kule kule - kana kwamba mawazo yako ndio bado yanaendeshwa enzi za Wakoloni (CCM) na unasubiria kupewa freedom!(kama ilivyokuwa 1961). Jitambue...piga hatua!

  Huyo Babu Kulola, anatakiwa awe anaingia na madhehebu mengine ya dini pia apate picha halisi! Na atofautishe elimu ya Uraia na uchochezi. Wachochezi wakuu wanajulikana, wala hawako makanisani...ndio wa kwanza kujikanyaga na kunyoosha vidole kwa yulee!...Achana na UHURU ili uwe kenye same wavelength na discussions za humu ndani...
   
 5. p

  politiki JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2010
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Jamani hizi habari zimetoka kwenye gazeti la uhuru ambalo ni gazeti la ccm. Ile pesa alioikataa askofu mochiwa inaelekea kulola ameichukua. Mtandao umeugundua wiki moja kabla ya kupiga na umeugundua wewe pekee yako nchi nzima wana ccm wote wakristo wanaosali makanisa mbalimbali awajauona isipokuwa wewe pekee yako.
  Angalia connection yake wakati jk analalamikia udini akiwashutumu cuf kwa uislamu upande wa pili wanashutumu chadema ukristo wao wako katikati. Ccm wameishiwa hoja kwahiyo wameanza kutapatapa kwani
  walikuwa wapi siku zote mpaka wasubiri wiki moja kabla ya uchaguzi kuanza kulalamikia udini.
   
 6. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  habari ndio hiyo! askofu kanena.. mnaanza kupinga
   
 7. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Kuna la ajabu? Si chanzo mnakiona?
   
 8. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,582
  Likes Received: 1,949
  Trophy Points: 280
  Sikubaliani na udini hata hivyo Kulola si mkweli na inawezekana anazungumza kimaslahi zaidi. Anasisitiza kuwa silaha ya wakristo ni maombi,lakini kwenye mgogoro wake na Askofu Imanuel Lazaro kuhusiana na kanisa lake vurugu ndio zilikuwa silaha yake na wafuasi wake na walipigana sana na kufungiana milango nk na hata ikabidi serikali iingile kusuluhisha...Kwanini hakuomba tu ili mgogoro wake wa kugombea uaskofu vs Lazaro uishe?Aache unafiki hata yeye hatumii maombi all the time,yani anataka kusema watu waombe tu lakini kura wasipige?Haya ya kutumia dini kumanipulate wananchi kwa maslahi binafsi ndo staili ya watu kama Kulolo....Shame on him mtumishi maslahi.
   
 9. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Duh, jamani nimeona Askofu Kulola sikusoma source ya habari! Too sad kuona Uhuru. Yaani ameshasahau mara hii mjukuu wake yuko kwa JK akituimbuiza nyimbo kibao kama wasanii wengine.

  Anyway, ngoja tuone miujiza mwaka huu naona vijimambo ni vingi.
   
 10. M

  Mashi Member

  #10
  Oct 22, 2010
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Do not "JUDGE" you will be "JUDGED"
   
 11. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #11
  Oct 22, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Askofu Kulola hana usafi wa kulikemea hilo ukizingatia kuwa mwaka 2005 alikuwa mstari wa mbele kupiga debe kuwa Kikwete ni chaguo la Mungu, na mwaka jana tu amekiri hadharani kuwa yeye ni CCM damu.
   
 12. Wakwetu03

  Wakwetu03 Senior Member

  #12
  Oct 22, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hivi huyu kulola alikuwa wapi 2005? Au ndo kusema hakuona ile slogani yao ya eti 'Chaguo la Mungu'.Naingiwa na mashaka na huyu mzee inawezekana kaishapa ile 40mil.Awaache wenye uchungu na nchi yao wawatetee wanyonge.Mzee tulia ili Heshima yako isishuke.Jina la Bwana lihimidiwe
   
 13. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #13
  Oct 22, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Askofu waombee washindwe!
   
 14. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #14
  Oct 22, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Source Please.
   
 15. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #15
  Oct 22, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Madrasa al sul
   
 16. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #16
  Oct 22, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,766
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Akamatwe akatoe maelezo ni akina nani wenye kampeni za chinichini!
   
 17. T

  Tata JF-Expert Member

  #17
  Oct 22, 2010
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,735
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Source in Gazeti la CCM la Uhuru
   
 18. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #18
  Oct 22, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Oktoba 31.
   
 19. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #19
  Oct 22, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,785
  Trophy Points: 280
  Gazeti linalomilikiwa na CCM la Uhuru la leo limemnukuu Askofu Mkuu Moses Kolola katika mazingira yanaonyesha ya kuwa anakerwa na Makanisa ya Kikristu kumpigia debe mgombea mmoja ambaye hata hivyo hakutajwa ambaye alidai siyo chaguo la Mungu.

  Pamoja na ukweli kuwa gazeti la Uhuru kama ilivyo kwa Habari Leo ni magwiji wa kuongeza chumvi habari zao lakini swali la muhimu hapa ni huyu Askofu kwa nini aongelea siasa ambazo amedai haziwahusu viongozi wa dini?

  Na ni lini Askofu huyu kawasiliana na Mwenyezi Mungu ili kufahamishwa chaguo la Mungu ni lipi na mbona hakulitaja ukiachia mbali kuwa hata yeye anafanya makosa yale yale anayowatuhumu wenzie ya kumpigia mgombea ambaye ni chaguo lake binafsi?

  Uhuru imemnukuu kuwa ametoa maelekezo kwa waaumini wake ambaye yanakinzana na azma yake ya kuondoa kanisa kutoka kwenye ulingo wa siasa.

  Vile vile kauli hii ni ya kibaguzi kwa sababu Askofu Kolola amejikita kwa wakristu bila kukemea dini nyinginezo ambazo nazo zimekuwa mstari wa mbele katika kuhubiri siasa na kumpigia debe mgombea wa madhehebu lao............

  Ni vyema Askofu Kolola akajitokeza na kufafanua haya maswala ambayo gazeti la Uhuru imeliyaibua kama ni kweli au la.......
   
 20. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #20
  Oct 22, 2010
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mbona mjukuu wake Flora Mbasha mwimba gospel yupo kwenye kampeni za Muungwana watu hawasemi. Huyo Kulola ni mnafiki
   
Loading...