Askofu Kanisa Katoliki Iringa fuatilia chuo cha Tosamaganga

Rocky City

JF-Expert Member
Nov 22, 2017
768
1,000
Wakuu,

Niende moja kwa moja kwenye hoja. Imezoeleka kwa muda mrefu sana kuwa vyou vinavyo milikiwa na makanisa ni vyuo bora vyenye kujali utu na malezi bora. lakini ukweli ni kwamba baadhi ya vyuo hivi vya dini vina uovu mwingi usioelezeka.
Chuo cha Tosamaganga Iringa ni moja ya chuo chenye uongozi mbaya sana hasa baadhi ya wasimamizi wake wakuu yani Masister.

Askofu wa jimbo hili jaribu kutenganisha uongozi wa chuo (administration) na umiliki hiki. Chuo kipo chini yako sisi wazazi tunatoa pesa zetu lakini wanachuo wanaishi ovyo sana pale. Chakula wanacho kula hakikidhi kabisa vigezo pamoja na mambo mengine.

Wanachuo wamekuwa na malalamiko kwa muda mrefu mno. Kinaonekana chuo cha kanisa lakini kinavyo endeshwa ni moja ya chuo cha ovyo sana. Malalamiko haya ya watoto wetu ina maana hamjayapata kweli? Kuna nini hapa kati na Ma sisister wale na waendeshaji wakuu kwa maana ya jimbo la Iringa?

Tunakusihihi askofu ,chuo hicho kichunguzwe kuna mambo mengi yako pele yanasikitisha mno ni suala la kufuatilia tu na ikumbukwe ni chuo kilicho chini ya kanisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chakochangu

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
2,630
2,000
Chuo cha kiwango gani ? Yaani kinatoa elimu ya kiwango gani ? Cheti?
Astashahada?Shahada? Digirii(1,2.....,)?
 
sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
737
1,000
Tatizo la vyuo vyinavyomilikiwa na makanisa ni kuwa na utawala wa hovyo wa kidini pia. Pale RUCU kuna jamaa mmoja ni mhasibu anaitwa Msilu anafanya kazi hovyo na kwa kujisikia sana lakini haonywi wala kuwajibishwa anapolalamikiwa, inasemekana sababu ni mkatoliki sijui alikuwa mhudumu wa askofu nk

Unaweza fuatilia cheti baada ya kumaliza akakuweka Iringa siku 2 au 3 eti anahakiki risiti zako na hataki wahasibu wengine kusaini clearance. Mpaka department za masomo, madean wanaogopa kumgusa.

Nakubaliana hoja na mleta mada, kuna matatizo kwenye utawala wa hivi vyuo vya kidini, wanaweka watu kwa misingi ya dini na sio weledi, salamu ziwafikie.
 
VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
3,890
2,000
Hoja yake kubwa ni chakula! Huenda mnakula kadiri ya bajeti yenu. Ni aibu sana kuandika wito kwa Kiongozi kizembe namna hiyo.Unashusha hadhi ya JF.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
jd41

JF-Expert Member
Aug 23, 2015
3,758
2,000
Sijakuelewa vizuri, tatizo ni chakula au masister?! au masister ndio wanasababisha mtoto wako asile pilau sio?japo sidhani km itawezekana chakula cha shuleni kifanane na cha nyumbani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
3,721
2,000
Ninachojua masista wapo creative sana, kama kuna eneo kubwa lazima watakuwa na ufugaji wa ngo'mbe na kitimoto. Kwa hiyo ni swala la wanachuo kuwaambia tu kwamba wana hamu ya kugonga kitimoto na maziwa mgando halafu utaona shughuli itakavyokuwa.
 
Rocky City

JF-Expert Member
Nov 22, 2017
768
1,000
Tatizo la vyuo vyinavyomilikiwa na makanisa ni kuwa na utawala wa hovyo wa kidini pia. Pale RUCU kuna jamaa mmoja ni mhasibu anaitwa Msilu anafanya kazi hovyo na kwa kujisikia sana lakini haonywi wala kuwajibishwa anapolalamikiwa, inasemekana sababu ni mkatoliki sijui alikuwa mhudumu wa askofu nk

Unaweza fuatilia cheti baada ya kumaliza akakuweka Iringa siku 2 au 3 eti anahakiki risiti zako na hataki wahasibu wengine kusaini clearance. Mpaka department za masomo, madean wanaogopa kumgusa.

Nakubaliana hoja na mleta mada, kuna matatizo kwenye utawala wa hivi vyuo vya kidini, wanaweka watu kwa misingi ya dini na sio weledi, salamu ziwafikie.
Mkuu ni moja ya mambo pia yaliyo pale..muhasibu wa pale sister huyo ana majibu ya ovyo mno kwa watoto.anatukana watoto tena wanachuo hakuna anaye mgusa hata viongoz wa chuo pale wanamuogopa.hakuna wa kumgusa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rocky City

JF-Expert Member
Nov 22, 2017
768
1,000
Ninachojua masista wapo creative sana, kama kuna eneo kubwa lazima watakuwa na ufugaji wa ngo'mbe na kitimoto. Kwa hiyo ni swala la wanachuo kuwaambia tu kwamba wana hamu ya kugonga kitimoto na maziwa mgando halafu utaona shughuli itakavyokuwa.
Umeunganisha kwa ujumla ila siyp kama unavyo dhani boss,ni kweli lakini si kw ma sister walio pale wanamajibu mabaya kwa wanachuo.wako juu ya kila kitu hadi uongozi wa chuo hakuna wa kuwahoji pale.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rocky City

JF-Expert Member
Nov 22, 2017
768
1,000
Sijakuelewa vizuri, tatizo ni chakula au masister?! au masister ndio wanasababisha mtoto wako asile pilau sio?japo sidhani km itawezekana chakula cha shuleni kifanane na cha nyumbani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umejibu vyema mno,lakini ni kweli kuna mzazi anampeleka mtoto akale pilau chuo??mkuu mambo yaliyo pale ni magumu mno mbali na chakula,chakula ni sehem ndogo sana ya matatizo hayo.kuna mengi nyuma ya pazia pale mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rocky City

JF-Expert Member
Nov 22, 2017
768
1,000
anataka askofu aache kazi zake akawaulize wanachuo kama wameshiba au la !!!!!!!!!!
Mkuu,sizan kama mtu mzima kweli anaweza kuwaza hivyo.yule ndiye msimamizi mkuu wa taasisi zote zilizo chini ya kanisa.chakula ni sehem ndogo ya malalamiko makubwa pale,kuna watu pale hasa hawa ma sister hakuna wa kumgusa pale.yupo juu ya kila kitu sasa nn maana ya kuwa na uongozi wa chuo mkuu.fuatilia mdau mwingine kasema habar za chuo kingine cha hapo juu.napo ni chakula?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
5,512
2,000
Serikali isipoingilia na kutoa mwongozo unaoeleweka,na usimamizi imara,kuna baadhi ya vyuo vya dini wanafanya mambo ya hovyo sana.
Kuwe na mikataba ya Huduma kwa mteja.Hii mikataba ni mizuri sana na inaweza kuzuia hawa viongozi wa dini kuingilia shughuli za kitaaluma na kupunguza aina za watu wasiogusika kida eti ni watu wa askofu.

Vinginevyo,napendekeza vyuo vinavyosabsbisha changamoto kwa sababu ya kuingiza udini na usimamizi mmbovu kama wanavyosimamia sadaka,vifutwe tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mrsleo

JF-Expert Member
Jan 13, 2014
2,423
2,000
ungeandika basi hayo mapungufu unayolalamikia, sasa wewe unalalamika tu bila maelezo
 
mkumbwa junior

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
342
500
Kwanza hili andiko linaonyesha wewe ni mwanafunzi w hapo wala sio mzazi kama ulivyokitambulisha na ndio maana ukalalamikia msosi,,pambana umalize masomo hizi kuku,piza,matonge utayakuta tu ukiwa na kazi yakoo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom