Elisha Sarikiel
JF-Expert Member
- Aug 29, 2020
- 889
- 1,515
YALIYOJIRI KONGAMANO LA WATUMISHI WA MUNGU KUMWOMBA NA KUMSHUKURU MUNGU KWA SIKU 100 ZA MHESHIMIWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KUWA MADARAKANI KUONGOZA NCHI YA TANZANIA
Kongamano lilianzia kwa maneno ya salamu za viongozi mbalimbali wa dini sawa na kusudi la kongamanona sambamba na mada kuu maalum zilizotolewa katika kutafakari siku 100 za Rais wetu, mhe.Samia Suluhu Hassan. Kongamano lilifanyika mubashara kupitia vyombo vya habari na mitandao ya jamii kama YouTube ! Unaweza kutazama video zenye ujumbe kamili kwa ufunguo huu >>> Kongamano la viongozi wa dini leo ! Kongamano hili lilifanyika ukumbi wa Kisenga,Millenium Tower;Dar Es Salaam tarehe 26/Juni/2021 siku ya Jumamosi asubuhi.
Miongoni mwa waliotoa mada kwa walihudhuria na watanzania kwa ujumla, ni askofu mkuu Zachary Kakobe; ambaye alijibu minong'ono iliyojitokeza katika jamii yetu baada ya kuapishwa mhe.Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kufariki kwa mpendwa wetu Rais mhe.Dkt.John J.P.Magufuli ! Askofu Kakobe alisema kwamba 'tulipomchagua Rais Magufuli, kimsingi tulimchagua Samia vilevile.' Kama mtu anafikiri alimchagua Magufuli kuwa Rais lakini hakumchagua mhe.Samia Suluhu Hassan ni upungufu wa elimu ya Uraia !
Katika uchaguzi wetu mkuu wa Rais haiwezekani kufanyika bila mgombea mwenza (Makamu wa Rais). Kwa wale wanaokumbuka mwaka 2005,ulikuwa ufanyike uchaguzi mkuu tarehe 30/Oktoba/2005; lakini ulihairishwa kwa sababu ya kufariki kwa mgombea mwenza wa kutoka Chadema, aliyeitwa Jumbe Rajabu Jumbe aliyefariki tarehe 26/Oktoba/2005 siku nne tu kabla ya kupiga ya kura uliofanyika tarehe 18/Desemba/2005. Mgombea wa urais wa Chadema wakati huo alikuwa ni Freeman Aikaeli Mbowe ambaye aliyesonga mbele na ANNA KOMU baada kuchaguliwa kuwa mgombea mwenza wake.Aliendelea kusema askofu mkuu Kakobe "Mgombea mwenza si tu anashika madaraka ya makamu wa Rais, lakini ilivyo katika KATIBA katika ibara ya 37, ibara ndogo 35 inaelekeza wazi kwamba Rais atakapofariki, anayechukua nafasi yake ni makamu wa Rais." Hivyo, kimsingi tunapokwenda katika uchaguzi mkuu wa Rais; tunamchagua Rais wa nchi na tunamchagua Rais mtarajiwa ! Kwa hiyo, tulipomchagua Rais Magufuli mpendwa wetu; tumemchagua na makamu wa Rais, yaani Mgombea mwenza. Ni kweli wananchi tulipomchagua Rais Magufuli tulimchagua Mama Samia vilevile kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu.
Pia, askofu Kakobe aligusia tofauti ya mtindo wa kufanya kazi kwa aliyekuwa Rais Magufuli na Rais Samia katika siku 100 madarakani. Alisema kuna watu wanauliza mbona hafanyi kama mpendwa wetu Magufuli ? Hii ni shida ! Aliendelea kufafanua kwa kusema:
- Alama za kipekee katika kila kidole (finger print) cha mkono wa mwanadamu ni tofauti.
- Alama za kipekee katika ulimi (Tongue Print) mwanadamu ni tofauti na ulimi wa mwenzake.
- Alama ya kipekee katika mboni ya jicho ni tofauti mwanadamu mwingine.
- Lips print
- Alama ya kipekee katika vidole vya miguu kati mwanadamu
- Kuna alama ya kipekee Retina kwenye jicho
- Seti za meno maumbo na namna yalivyo tofauti kati mwanadamu na mwanadamu.
- Kuna tofauti iliyopo ya sauti kisayansi.
- Alama nyingine ya tofauti ni "harufu" kati ya mwanadamu na mwanadamu.
Askofu Kakobe alisema "Samia wewe ni Rais si msanii au mwigizaji na kwa sababu hii; tuongoze kwa style yako mwenyewe. Nikuombe Rais utuongoze vile ulivyo kwa asili yako katika mpango wa Mungu; maana hataki kumwona Magufuli mwingine; bali Rais Samia kwa kuwa kila jambo lina kusudi la Mungu." Nasi tukubali atuongoze kwa style yake; kwa kuwa hakuna Magufuli mwingine atakayekuwepo; na atakayejaribu kuwa kama Magufuli atakuwa mwingizaji. Nia ni moja ya kazi iendelee kwa kuwa ilani ya uchaguzi mkuu ni ileile bali mtindo wa kuongoza ni tofauti kati yao.
Askofu Kakobe, alisema Tumpe ushirikiano mia kwa mia Rais Samia Suluhu Hassan. Na watu wote walisimama ukumbini na kuadhimiwa leo katika kongamano na kusema kwamba '"MHESHIMIWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN TUONGOZE KWA STYLE YAKO USIWE MWIGIZAJI WALA MSANII. TUONGOZE VILEVILE ULIVYOUMBWA. TULIVYOKUCHAGUA MGOMBEA MWENZA, TULIKUCHAGUA KAMA RAIS MTARAJIWA. TUNAMSHUKURU KWA SIKU 100, TUNAMTUKUZA KUKUUMBA VILE ULIVYO. "
Mwisho wa Kongamano alipata nafasi Askofu mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship naye kuongoza maombi maalum kwa Rais Samia Suluhu Hassan; na taifa letu kulibariki sawa sawa na mapenzi ya Mungu aliyeumba mbingu na nchi. Kauli ya askofu mkuu Zachary Kakobe alipopewa nafasi alisema "TUMESHINDA NA ZAIDI YA KUSHINDA "Tazama video clip hapa chini kwa ufupi.